Mgaa gaa upwa
Senior Member
- Jan 11, 2024
- 180
- 281
Poleni na majukumu ya Kila siku.
Mwezi wa tano nilimfungulia biashara ya uwakala mke wangu, nikajenga duka na lilipokamilika nikawa nimebakiwa na fedha kidogo Kama mtaji, baada ya biashara kuanza nikaona Umuhimu wa kupanua biashara.
Nikawahi Benki ya NMB na kupata mkopo wa fedha kidogo ili kukuza biashara nilichukua kidogo ili kuendana na upepo.
Upepo ukakubali hivyo nikaamua kuongeza mkopo (top up).
Hilo lilikuwa kosa kubwa kwani Mara baada ya fedha za top up kuingia tu matatizo yakaanza..
1:-Akaunti yangu ikafungiwa na kiasi changu Cha fedha zangu za akiba, matumizi binafsi na mkopo wenyewe zikafungiwa.
2:- Nikaanza kukatwa mkopo Mara mbili yaani nakatwa mkopo wa Kwanza ule mdogo nilioulipa (kwenye top up) na mkopo wa pili (mkopo mkuu uliobeba Deni lote) nakatwa pia.
3:- Mkopo wa Kwanza haujafutwa (Maana nimeulipia kwenye top up)
Nimefuatilia Sana tatizo langu hapa tawini Hadi branch manager akanichukia na kuanza kunitisha kuwa atanishtaki kwa mkurugenzi ili nifukuzwe kazi.
Nikaamua kuingia kwenye emails (NMB makao makuu,huduma kwa wateja na BOT huduma kwa wateja) nikatembelea tawi la NMB mkoani Ila tatizo lipo pale pale.
Kuanzia mwezi wa Tisa Hadi mwezi wa kumi na mbili bado namekatwa makato zaidi na fedha zangu zimezuiliwa.
Msaada wanajf maana mwaka unaelekea ukingoni na Mimi sijatimiza adhima ya kumuwezesha mke.
Nitumie mbinu gani, watu gani na njia gani kuchukua pesa zangu.
Nimeweka ushahidi wa emails hapo chini.
Emails kwenda BOT
Emails kwenda NMB