Ninawezaje kuifungulia mashtaka Benki ya NMB kwa dhuluma hii ya fedha zangu?

Ninawezaje kuifungulia mashtaka Benki ya NMB kwa dhuluma hii ya fedha zangu?

Unamkumbuka kuna mfanyabiashara fulani pale kariakoo alikuwa na kesi na TRA? Alitumia media mwisho wa siku hamna alichokipata.
Alikurupuka. Taasisi za Benk ziko very sensitive kurespond malalamiko yoyote dhidi Yao especially Yale amboyo yako public (social media)

Why ? : Msingi wa Mafanikio ya bank yanatokana na reputation.

Hii ni Golden Chance kwa huyu mwamba.
 
Lazima hapa kuna kitu hakiko sawa eidha kwa upande wa benki au upande wako. Kama huna au hujawahi kuwa na tatizo lolote na hiyo benki na marejesho ya mkopo wao ulikuwa unalipa kwa wakati bila kupitiliza muda wa malipo nakushauri umwandikie yule CEO wao atakusaidia. Ni mama mwelewa sana atakupa nushirikiano mzuri tu
 
Kwanza Pole sana

nilichochogundua kuwa wewe ni mtumishi wa Umma na ndo maana Huyo manager amesema arakushitak kwa mkurugenzi wako

Kwa ushauri wangu kwenye kutafuta haki usiogope wala nini anza kwanza kwa huyo mkurugenzi wako muelezee na HR manager wako.

pia omba kuhama bank ya kupokea mshahara kutoka NMB kwenda bank Nyingine mfano CRBD au NBC

Tatu andika barua kwa HR manager kuwaomba wache kufanya makato ya mkopo wako kwa kuwa NMB wamekiuka makubaliano ya makato.

Elewa kwamba NMB hawawez kukata makato toka hazina moja kwa moja bila wao huwasilisha madai ya makato kwa muajiri wako ili uanze kukatwa hivo kwa scenario hiyo anza kwa muajiri wako.

Mwisho tafuta nauli uende NMB makao makuu kwa afisa mikopo mkuu na mwanasheria wa NMB wakupe ufafanuzi wa kisheria kuhus makato unayokatwa na mpate muafaka wa kuondolewa hayo makato ambayo sio halali.

Hakikisha unapoenda tafuta mwanasheria wako mlipe kwa siku hiyo moja muende wote.

Beba ushahidi wa kina wenye uzito.

Mwisho usiogope kutafuta haki yako vitisho vya aina yoyote ile usiogope kwa kuwa mkopo unaokopa upo kisheria na una taratibu zake hivo kama wamekiuka taratibu hata wakishutaki kwa muajiri wako hawawez kukuletea madhara.

Ajira za serikali sio kama private huwez kufuzwa kwa sababu za kipuuzi kama hizo.

Zinagatizo usirudie tena kufanya topup ya mkopo wa aina yoyote ile ni hatar sana
 
NMB!!!
Hawa jamaa wababaishaji sana, nakupa mfano mdogo, pale Dumila Morogoro wamefungua tawi lao, ukitokea Dodoma wameweka kakibao kao NMB 5KM Ahead wakati bank ipo 1.5Km toka kibao kilipo, sasa kama hawawezi kujua distance ndogo tu ya mita 1500 unategemea utendaji wao ukoje humo kwenye mabilioni
 
Poleni na majukumu ya Kila siku.

Mwezi wa tano nilimfungulia biashara ya uwakala mke wangu, nikajenga duka na lilipokamilika nikawa nimebakiwa na fedha kidogo Kama mtaji, baada ya biashara kuanza nikaona Umuhimu wa kupanua biashara.

Nikawahi Benki ya NMB na kupata mkopo wa fedha kidogo ili kukuza biashara nilichukua kidogo ili kuendana na upepo.

Upepo ukakubali hivyo nikaamua kuongeza mkopo (top up).

Hilo lilikuwa kosa kubwa kwani Mara baada ya fedha za top up kuingia tu matatizo yakaanza..

1:-Akaunti yangu ikafungiwa na kiasi changu Cha fedha zangu za akiba, matumizi binafsi na mkopo wenyewe zikafungiwa.

2:- Nikaanza kukatwa mkopo Mara mbili yaani nakatwa mkopo wa Kwanza ule mdogo nilioulipa (kwenye top up) na mkopo wa pili (mkopo mkuu uliobeba Deni lote) nakatwa pia.

3:- Mkopo wa Kwanza haujafutwa (Maana nimeulipia kwenye top up)

Nimefuatilia Sana tatizo langu hapa tawini Hadi branch manager akanichukia na kuanza kunitisha kuwa atanishtaki kwa mkurugenzi ili nifukuzwe kazi.

Nikaamua kuingia kwenye emails (NMB makao makuu,huduma kwa wateja na BOT huduma kwa wateja) nikatembelea tawi la NMB mkoani Ila tatizo lipo pale pale.

Kuanzia mwezi wa Tisa Hadi mwezi wa kumi na mbili bado namekatwa makato zaidi na fedha zangu zimezuiliwa.

Msaada wanajf maana mwaka unaelekea ukingoni na Mimi sijatimiza adhima ya kumuwezesha mke.

Nitumie mbinu gani, watu gani na njia gani kuchukua pesa zangu.

Nimeweka ushahidi wa emails hapo chini.
Nenda FCC ,wana dirisha la Consumer protection .nazani ni suluhisho na wana wanasheria watakusaidia .

Lakini bado hujashindwa ,NMB wenyewe watakusaidia ongea na credit manager wa HQ .

lakini kuna kitu haujatuambia kama unaficha .hawawezi fanya hivo tu bila taratibu ,labda kuna udanganyifu ulifanya tupe maelezo mazuri
 
Hilo ndilo tatizo

(NMB Wana wanasheria pia wakubwa tu).

Na tena nimeshuhudia mtu akinyimwa haki yake zaidi ya miaka 30, napata Shaka kuu.

Ila penye Nia Pana njia ngoja niwacheki wanasheria Kwanza.
Mbona kuna kesi nyingi banks kama NMB zinashindwa tu? usimuogopeshe .fuatilia kesi nyingi tu tena advocates wadogo wanashinda .

Kama ni Haki yako Mungu atakuongoza
 
Nenda FCC ,wana dirisha la Consumer protection .nazani ni suluhisho na wana wanasheria watakusaidia .

Lakini bado hujashindwa ,NMB wenyewe watakusaidia ongea na credit manager wa HQ .

lakini kuna kitu haujatuambia kama unaficha .hawawezi fanya hivo tu bila taratibu ,labda kuna udanganyifu ulifanya tupe maelezo mazuri
Uliza chochote kama unahisi nakudanganya nitakujibu.
 
Lazima hapa kuna kitu hakiko sawa eidha kwa upande wa benki au upande wako. Kama huna au hujawahi kuwa na tatizo lolote na hiyo benki na marejesho ya mkopo wao ulikuwa unalipa kwa wakati bila kupitiliza muda wa malipo nakushauri umwandikie yule CEO wao atakusaidia. Ni mama mwelewa sana atakupa nushirikiano mzuri tu
Naomba email yake nimuandikie maana Nina uhakika Sina tatizo na mtu ndiyo maana nimeamua kujishusha ili nipate haki yangu.

Mimi siyo wa kukaripiwa Kama mtoto mdogo eti kisa ni Branch manager
 
Back
Top Bottom