Si kila mtoto kapatikana ndani ya ndoa
Nafikiri huja nielewa ngoja niku eleweshe
Kuowa ni lazima kwa sababu ni asiri yetu kuishi na wenza wetu
*Huwezi kuitambua thamani ya mke Kama uhuni haujakutoka kichwani bado
*Huwezi kuitambua thamani ya mke Kama hakiri yako bado haija wai kujutia kutumia pesa vibaya,kwa Mambo ya kipuuzi kwani utakuwa bado huja kuwa
Mambo haya huja yenyewe tu
Utaanza kuwaza kuwa na nyumba/kwako baadae utaanza kuchoka kupika na kufua
Huku mtaani watu Wana kuuliza unamke?unajibu hapana wana kuuliza kwanini na uzee wote huo?
Hapo ndipo unakuja kugundua kwamba daah kumbe mi mzee tayari? Unaona Bora uwai kuowa wanawake wasije kukataa uka zeheka pasipo mke
Baadae ya kuowa una jikuta unaanza kutamani mtoto unaanza kumtafutia una mpata BAADA ya hapo gafra tu unaanza kutoka kazini unaenda moja kwa moja nyumbani
Yale Mambo ya mademu,viwanja,pombe Sana una Anza kuyaona zilipendwa uzee una kufika unaanza kushinda nyumbani
baada ya hapo una Anza kuiona faida ya kuowa unapo watuma watoto na kuheshimiwa na watoto wa wenzio sababu ya watoto wako
Hapo unaanza kuitambua faida ya kumlea mtoto ndani ya ndoa na hasara ya mtoto kuto kulelewa na wewe
Baada ya hapo una chomoka watoto Kama uliwalea vizuri watamtunza mama yao. unajua kwanini nime sema mama yao?
Ni kwasababu wanaume tuna wai kufa
Lakini Kama ulizalisha nje yaka lelewa na mama zao na akina mjomba wa kitaani Basi ukifa Yana mfukuza mkeo yana uza nyumba yanaenda kula bata pesa yote kwa siku moja
Iko hivyo bwana mda ukifika utaowa tu utake usitake