Ninayetaka kumuoa ana mchepuko mwingine

Ninayetaka kumuoa ana mchepuko mwingine

Wanaume wa skuizi huku kupenda mseleleko kutawakutanisha na mambo ya ajabu sana...
Wanawake wachapakazi watawapiga na vitu vizito sikuzote😂😂😂😂 mtu ana red flag za kutosha umekazania et mchapakazi!!! Beba majukumu mzee uepukane na dhahama kama hizo!!
 
Si kila mtoto kapatikana ndani ya ndoa
Nafikiri huja nielewa ngoja niku eleweshe

Kuowa ni lazima kwa sababu ni asiri yetu kuishi na wenza wetu

*Huwezi kuitambua thamani ya mke Kama uhuni haujakutoka kichwani bado

*Huwezi kuitambua thamani ya mke Kama hakiri yako bado haija wai kujutia kutumia pesa vibaya,kwa Mambo ya kipuuzi kwani utakuwa bado huja kuwa

Mambo haya huja yenyewe tu

Utaanza kuwaza kuwa na nyumba/kwako baadae utaanza kuchoka kupika na kufua

Huku mtaani watu Wana kuuliza unamke?unajibu hapana wana kuuliza kwanini na uzee wote huo?

Hapo ndipo unakuja kugundua kwamba daah kumbe mi mzee tayari? Unaona Bora uwai kuowa wanawake wasije kukataa uka zeheka pasipo mke

Baadae ya kuowa una jikuta unaanza kutamani mtoto unaanza kumtafutia una mpata BAADA ya hapo gafra tu unaanza kutoka kazini unaenda moja kwa moja nyumbani

Yale Mambo ya mademu,viwanja,pombe Sana una Anza kuyaona zilipendwa uzee una kufika unaanza kushinda nyumbani

baada ya hapo una Anza kuiona faida ya kuowa unapo watuma watoto na kuheshimiwa na watoto wa wenzio sababu ya watoto wako

Hapo unaanza kuitambua faida ya kumlea mtoto ndani ya ndoa na hasara ya mtoto kuto kulelewa na wewe

Baada ya hapo una chomoka watoto Kama uliwalea vizuri watamtunza mama yao. unajua kwanini nime sema mama yao?

Ni kwasababu wanaume tuna wai kufa

Lakini Kama ulizalisha nje yaka lelewa na mama zao na akina mjomba wa kitaani Basi ukifa Yana mfukuza mkeo yana uza nyumba yanaenda kula bata pesa yote kwa siku moja

Iko hivyo bwana mda ukifika utaowa tu utake usitake
 
Nimekuelewa Kwa herufi kubwa Mkuu
Umemuelewa? Mimi naomba jikwambie tu ukweli, chagua wewe usuke ama unyoe. Kama kweli umekuja huku kuomba ushauri, usichague ushauri postive tu! Sasa huyo kakwambia kama una uhakika kimba ni yako songa mbele Kila mwanamke ana mapungufu yake, umeitikia lakini ukweli ni kwamba umedanganywa. Mimi nakwambia haya kwasababu ni mwanamke. Hivi wewe hiyo mimba unayosema una uhakika ni yako? Uhakika upi? Umepima DNA tumboni ama? Anaejua ukweli ni huyo mke, hakuna njia yyte itakufanya wewe ujue ukweli. Sasa nikwambie ukiona mwanamke kafikia hatua ya ku attend sex na mwanaume mwingine tena kwa Hiali yake na mko kwenye mahusiano. Huyo ushampoteza. Trust me¡ Kwanini nakwambia hivo. Nyie wanaume mna cheat kwa tamaa ila mwanamke mpaka akucheat huyo kamaanisha. Sasa kama we uko tyar kuendelea na mtu atakae kuza biashara ila akusalit milele Go on. Ila kama unataka mke hapo huna chako, nimemaliza.
 
Kakak ukiona ivyo jua Hausimamii ukucha vizuri ipasavyo jitaidi kupeleka moto ukipata Mingina, Huyo akufai.
 
Moyo wanbinadamu ni kichaka kikubwa sana,usikute waliachana na baba mtoto kwa ajili hyo ya uchepukaji,kua making asikuletee magonjwa.
 
Kifupi unampenda na huna maamuzi sahihi, kumbuka afya njema ni mtaji wa Kwanza katika maisha. Super!!!
 
Mtu keshajifungia mwenyewe na kufuli kwa akili yake, wataka ukachonge funguo ya nini?
 
Habari zenu? Kuna single mama mmoja binti wa miaka 25, nimekuwa naye kwenye mahusiano Kwa karibu mwaka mmoja na sasa hivi ana ujauzito wangu wa miezi 5. Ila ana mtoto wa miaka mitano aliyezaa na mwanaume mwingine. Huyo mwanaume walishaachana kitambo tangu mtoto akiwa ana mwaka na jamaa huwa anatuma fedha za matumuzi tu.

Sasa Mimi nikawa nimevitiwa na huyo dada kutokana na uchapakazi wake, na hata dukani ana kauli NZURI Kwa wateja na ana mkono wa Biashara kweli kweli. Nikaona huyu ndiye mwanamke wa kuanza naye maisha japo nawaogopa ma single mother ila nikaamua Nile ngumu.

Cha ajabu majuzi nimekuta msg za mwanaume mwingine kwenye simu, Tena sio baba mtoto wake ila mwanaume mwingine kabisa na walikuwa wnapanga miadi ya kuonana waka vunje amri ya sita. Sasa kilichonishitua zaidi ni binti huyu kuwa na uthibutu wa kuchepuka akiwa mjamzito Tena Tumbo tayari limeanza kuonekana. Hivi akishajifingua itakuwaje?

Sasa hapa niko dilema sijui nifanyaje coz ujauzito ni kweli WA kwangu Nina uhakika asilimia 98, na binti ni mchapa kazi Yana ana sifa zote za kuwa mke. Ila kilichonishitua ni hiyo tabia yake. Najiuliza kama itakuwa sahihi kumuacha akiwa mjamzito?

Na pia nilipomuuliza kuhusu huyo MCHEPUKO alijotetea akasema ilikuwa ni chatting tu, coz ni mwanaume wake wa zamani sana ila hawajafanya chochote, na ameshamwambia kuwa yeye ni mchumba WA mtu hivyo hakuna kinacho endelea kati yao.

Mnanishaurije hapo wadau?
Achana nae na we pia lea mtoto kama una hakika ni wako. Kama ni duka unaweza kusimamia hata wewe.
 
1petro3.7

"Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili" ✍️

Me nawashangaa sana vijana wanaokimbilia kuoa eti kwasababu wanao uwezo wa pay bills na mahitaji mengine kwa mwanamke so sadness 😢

Ni wanawake wangapi tunashuhudia kwake kuna kila kitu hakosi chochote na gari kanunuliwa lakini anatoka nje ya NDOA yake na dereva bodaboda

Kijana Pesa, magari, na mali sio hitaji la kwanza kwa mwanamke na ukimtangulizia mwanamke hivyo vitu umekwisha takakuja akufanye kitu kibaya sana hata ikapelekea kumtenda ubaya na kuishia jera

Hitaji la kwanza kwa mwanamke ni kumfanya awe Bora na hili ndo hitaji muhimu na kubwa kwa mwanamke yoyote

Kitu ambacho wengi hawajui hata wanawake wenyewe hawajui hi Siri ni kwamba MUNGU ameweka kila kitu NDANI ya MWANAMKE, kuna hadhina kubwa sana NDANI ya MWANAMKE yoyote kwa familia na ndoa yake ila tatizo Wengi hawajui jinsi ya kudispay hi hadhina kwa NDOA, familia Hadi katika jamii inayowazunguka

Kizazi cha Leo cha jinsia ya kike kilivyopotoka na kukosa maarifa eti unakuta MWANAMKE anatafuta MTU mwenye Pesa au KAZI au tajiri ndo aolewe nae 😢..... Wakati hivi vyote hawafahamu kua MUNGU ameviweka NDANI yao kwaajili ya familia na NDOA zao

Kijana mke katika NDOA utampata ukiwa huna kitu chochote Kwaiyo tafuta Mwanamke ambae atakuvumilia ukiwa zero wapo wengi na huyo ndiye mke bora, ...

Ukitaka kupata Mwanamke katika NDOA we tafuta binti ukiwa tayari na kitu mkononi hawa viumbe wanaongozwa na tamaa afu ngojea itokee siku hicho kitu kimeondoka ndo utamuona sura yake

KUNA TOFAUTI KATI YA MKE NA MWANAMKE ,

👉AKILI ITAMBADILISHA MWANAMKE KUA MKE B'SE UNAPOKUTANA NA BINTI AT FIRST TIME HUYO NI MWANAMKE SASA NI JUKUMU LAKO KIJANA KUMBADILISHA HUYO MWANAMKE KUA MKE NA SIO KAZI NYEPESI HATA KIDOGO INAHITAJI HEKIMA NA AKILI


MWANAUME Ukitaka kuona dunia chungu na upoteze Radha ya MAISHA ya hapa duniani oa kiumbe kinachoitwa MWANAMKE ndo utaona shughuli yake

Na hapa ndo utaukumbuka ule msemo wa kiswahili usemao " kosea vitu vyotee..! ila usikosee kuoa"😀

Niwaibieni Siri wana mama na dada zangu👉 MWANAUME anaekupenda ni yule anaekufanya wewe uwe BORA na si yule anaekupa vitu ✍️
Hakika umenena vizuri Sana mkuu
 
Back
Top Bottom