mbutamaseko
JF-Expert Member
- Nov 20, 2018
- 743
- 1,071
Chai. Sema utakuwa umepitia kitu kinachofanana na hiki af ukazingua mbeleni
Nilimwoa mke wangu miaka 30 iliyopita. Alikuja na Watoto wake wawili wa ndoa yake ya awali.
Niliwapenda sana na nikawakubali na kuwafanya kama watoto wangu kwani Sikubahatika kuwa Na Mtoto Wangu mwenyewe.
Tulianza Maisha Yetu, Tulikaa kwa amani katika nyumba Ya kupanga. Nilikuwa nikifanya kazi wakati huo na nilihakikisha kuwa ninawapeleka watoto Hao shule. baba yao hakuwahi kuja kuwaona wala kutoa Huduma Zozote.
Watoto Hao walikuwa Wapo Vizuri Sana Katika Masomo Yao Shuleni. Walisoma Hadi Chuo Na Kubahatika kuajiriwa Mmoja Ni Daktari Ambaye Alipata Udhamini wa kumaliza masomo yake huko USA.
Amerudi na tayari ameshaajiriwa, kijana wa pili ni rubani ambaye nilitumia akiba yangu yote kumlipia kozi yake huko Afrika Kusini, pia amerudi na ameajiriwa pia.
Furaha yangu ni kwamba watoto wangu wamefanikiwa na wamenunua nyumba kubwa, shida yangu ni kwamba mke wangu na watoto Hao
wawili wameungana na baba yao na sasa wanaishi pamoja kwa furaha kama familia.
Wamenitelekeza hapa, siwezi hata kulipa kodi tena, nilistaafu zamani, nimekuwa nikiomba omba Kwa Watu Wanisaidie Hela kwa watu Nipate chakula Na Hata sehemu Ya kulala. Sahizi hata simu yangu hawapokei Tena Na Wameniblock.