Ningejua nisingewalea watoto wangu wa kufikia. Najuta!

Ningejua nisingewalea watoto wangu wa kufikia. Najuta!

Ndoa yenye watoto huwa haivunjiki. Ukimpenda mama yao, kula kilicho kitamu kwa wakati huo na hakikisha watoto wanamjua na kuhudumiwa na baba yao.
Nilimuoa mke wangu miaka 30 iliyopita. Alikuja na Watoto wake wawili wa ndoa yake ya awali.
Niliwapenda sana na nikawakubali na kuwafanya kama watoto wangu kwani sikubahatika kuwa Na Mtoto Wangu mwenyewe.

Tulianza Maisha Yetu, Tulikaa kwa amani katika nyumba ya kupanga. Nilikuwa nikifanya kazi wakati huo na nilihakikisha kuwa ninawapeleka watoto Hao shule. baba yao hakuwahi kuja kuwaona wala kutoa Huduma Zozote.

Watoto Hao walikuwa Wapo Vizuri Sana Katika Masomo Yao Shuleni. Walisoma Hadi Chuo Na Kubahatika kuajiriwa Mmoja Ni Daktari Ambaye Alipata Udhamini wa kumaliza masomo yake huko USA.

Amerudi na tayari ameshaajiriwa, kijana wa pili ni rubani ambaye nilitumia akiba yangu yote kumlipia kozi yake huko Afrika Kusini, pia amerudi na ameajiriwa pia.

Furaha yangu ni kwamba watoto wangu wamefanikiwa na wamenunua nyumba kubwa, shida yangu ni kwamba mke wangu na watoto hao wawili wameungana na baba yao na sasa wanaishi pamoja kwa furaha kama familia.

Wamenitelekeza hapa, siwezi hata kulipa kodi tena, nilistaafu zamani, nimekuwa nikiomba omba kwa Watu Wanisaidie Hela kwa watu nipate chakula na Hata sehemu Ya kulala. Sasa hivi hata simu yangu hawapokei tena na wameniblock.
 
liwe funzo na kwa wengine usioe single maza otherwise umeona kaburi la mmewake,ukiamua kuoa do it at your own risk
 
Gahawa
JamiiForums-1886462678.jpg
 
Huu ni uongo.... story yako imeajca gapes nyingi Sana ...kajipange
 
Mke mwenye watoto ntaoa sana/na weye oa tu... ili mradi awe mtamuuuu. Watoto kupeleka shule ni hiari yako...pima kwanza je mama yao anakismart na weye? Km kipo wapeleke shule tu...na wewe jiweke sawa kiuchumi mnooo.. kupitia nyota yake huyo Mama yao...so wakija sawa wasopo kuja sawa tu kula maisha kwa kwenda mbele....mleta mada hajui kuwa alipata hela kupitia kismart cha Mama yao..... Sasa mama hayupo analalama......amini usiamini kuna ke ukikaa nao unapata hela mingi si kawaida hata za kununua Meli ya mizigo.....ndo maana watu hatu waachi ke wa ivo hata km amepinda miguu...kiwete......zeruzeru...hatujali ili mradi nyota ya mafanikio inatuwakia kupitia yeye......si mnamuona Mengi alijichanganya akamuacha yule Mama cheupe!! Peeee!!! akafa kizembe sana. Unakumbuka???
Kuna ukweli hapa. Kuna ndito nilikua nayo zamani, mzaramo elimu ya msingi lkn bwana utafikiri mto wa pesa ulikua unapitia chumbani kwangu. Kuja kumuacha pesa ilikatika huwezi kuamini. Mimi Tena nikarudi kupanda uda na daladala, kunywa beer local na kuanza kujifunza kuongea kiswahili.
 
Katiba Mpya itasimamia haki za WAZAZI KWA kuwalea Watoto WAO KWA kuhakikisha wananwalea WAZAZI WAO wanapokuwa WAZEE na kutojiweza !!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA!!!
 
Hao watoto nao watalipwa na watoto wao. Karma is real
 
Bora hata n ya kutunga maana iliniumiza sana[emoji2955]
 
Back
Top Bottom