Ningekuwa mimi ndio Waziri wa Michezo ningejikita kujenga vyuo vya mpira wa miguu vitakavyo simamiwa na Taifa stars

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Kwanza kabisa mikakati yangu ingekua ni kuifanya Taifa starts ijitegemee kwa kujiingizia kipato chake yenyewe.

Ningefanyeje kufanikisha hilo ningeomba bajeti kwaajili ya Taifa stars ijenge vyuo (Football academies) vya mpira wa miguu kila wilaya. Vyuo vitakavyo fundisha soka kwa watoto wadogo hadi vijana wa miaka 18. Walimu watakao fundisha soka wangetoka nchi za nje na wengine wangetoka Taifa stars.

Mapato ya ada zitakazo lipwa na wanafunzi yangeingia moja kwa moja kwenye mfuko wa taifa stars.

Vijana wakisha kuhitimu masomo ya nadharia na vitendo wangeuzwa moja kwa moja kwenye vilabu vya mpira wa miguu vya ndani na nje ya nchi na mapato yote yangeingia moja kwa moja kwenye mfuko wa Taifa Stars.

Ningeiwezesha taifa stars kwa kuajiri wahandisi wanamichezo watakao husika na kujenga miundombinu yote ya michezo ikiwemo viwanja vya mpira wa miguu, shule za michezo na vyuo vyuo vya michezo (Football Academies). Miradi yote ya ujenzi wa miundombinu ya mpira wa miguu ingepitia kwanza Taifa Stars ndipo ujenzi uendelee.

Kupitia hivyo ingechukua miaka 20 tu kukuza mpira wa miguu kwa wachezaji wa ndani nchini. Vipaji vyote vya mpira wa miguu vilivyopo vijijini na mijini vingesajiliwa kusoma vyuo vilivyojengwa na Taifa Stars kwa ufadhili wa wizara.

Inaonesha hujui hata Taifa Stars ni kitu gani. Taifa Stars ni timu yenye wachezaji wanaochaguliwa kuiwakilisha nchi kwenye mashindano husika.
Timu huchaguliwa na kocha nae huchaguliwa na kufukuzwa kila mara
Sasa timu itasimamiaje chuo?
 
Huo utaratibu unaweza kubadilishwa mkuu. Kila jambo huwekwa na watu na watu haohao wanaweza kuliondoa. Taifa stars inaweza kutengeneza jezi na kuuza, Taifa stars inaweza kuuza wachezaji, Taifa stars inaweza kumiliki vyuo na pia inaweza kumiliki viwanja.
 
Kwanza kabisa mikakati yangu ingekua ni kuifanya Taifa starts ijitegemee kwa kujiingizia kipato chake yenyewe.

Ningefanyeje kufanikisha hilo ningeomba bajeti kwaajili ya Taifa stars ijenge vyuo vya mpira wa miguu kila wilaya. Vyuo vitakavyo fundisha soka kwa watoto wadogo hadi vijana wa miaka 18. Walimu watakao fundisha soka wangetoka nchi za nje na wengine wangetoka Taifa stars.

Mapato ya ada zitakazo lipwa na wanafunzi yangeingi moja kwa moja kwenye mfuko wa taifa stars.

Vijana wakisha kuhitimu masomo ya nadharia na vitendo wangeuzwa moja kwenye vilabu vya mpira wa miguu vya ndani na nje ya nchi na mapato yote yangeingia moja kwa moja kwenye mfuko wa Taifa Stars.

Ningeiwezesha taifa stars kwa kuajiri wahandisi wanamichezo watakao husika na kujenga miundombinu yote ya michezo ikiwemo viwanja, shule na vyuo. Miradi yote ya ujenzi wa miundombinu ya mpira wa miguu ingepitia kwanza Taifa Stars.

Kupitia hivyo ingechukua miaka 20 tu kukuza mpira wa miguu kwa wachezaji wa ndani nchini.

Hapo kwenye kusimamiwa na taifa stars sijaelewa kabisa
 
Nilifikiri ungetumia hela zako, kumbe hadi uombe bajeti

Kwa pesa gani?? Pesa ya kujenga shule na madawati (basic needs) tunakopa na kusaidiwa, tutakuwa na pesa ya kujenga hivyo?
 
Mkuu kila wizara hutengewa bajeti hiyo ni sehemu ya maendeleo
 
Taifa stars ndio taasisi gani?, Duniani kote mpira unaendeshwa na sekta binafsi, serikali inatengeneza mazingira mazuri...!!.
 
Back
Top Bottom