Ningekuwa na maamuzi kwenye club ya Simba, ningemuondoa msemaji wa club ya Simba, Ahmed Ally

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
8,581
Reaction score
15,618
Inasemwa kwamba kazi ya afisa uhusiano ndio kazi ngumu kabisa huku duniani. Kazi hii inahitaji mtu mwenye uelewa wa mambo haswa yale ambayo atakuwa akiwashirikisha watu kuhusu kampuni, taasisi na mashirika ambayo ndio anafanyia kazi.

Kwa mfano. Afisa uhusiano wa jeshi la polisi. Msemaji wa jeshi la wananchi. Afisa habari wa TRA. Msemaji wa ikulu nk.

Unapokuwa kwenye nafasi ya afisa uhusiano wa taasisi yoyote unaweza kuifanya taasisi ikaonekana inafanya mambo hake vizuri au vibaya. Ndivyo ilivyo kwa msemaji wa klabu ya simba ya dar es salaam ndungu Ahmed Ally.

Kupitia mitandao ya kijamii, Ahmed Ally amekuwa akionekana akiizungumzia Club ya Simba kimzaha mzaha, kiasi kwamba Club ya Simba inaonekana kituko kupitia yeye.

Kwa jinsi navyomwona, yeye ndio ananufaika zaidi kuliko Club ya Simba. Taarifa zake nyingi zimekuwa ni za kimipasho zaidi kuliko zile official club statement ambazo uwasilishaji wake pia unatakiwa kuwa na nidhamu.
Uwasilishaji wake wa taarifa umekaa kitambotambo na kujidaijidai na ni kwa sababu ya kukosa ubunifu na matokeo ya kuigaiga watu wa aina ya kina Hadji Manara.

Ahmed Ally anajinufaisha yeye kwa mgongo wa club ya simba kwa kutaka sifa hata kama ni za kijinga ili mradi apate follers wengi huko insta na facebook.

Ningekuwa na mamlaka, ningempiga chini huyu jamaa.
 
GENTAMYCINE a.k.a AKili Kubwa na Tajiri wa Maono nimeandika sana hapa kuhusu Mapungufu yake mkaniipuza. Pole!!
 
Sawa Ally Kamweeee
Hawa wote Mm nawaona ni wale wale, hivyo naona mtoa mada ni shabiki wa Yanga hvy hawezi kuona tatizo kwa Kamwe.
Ila binafsi hao wote Kamwe na Ahmed wanafanya kazi zao vzr mana ndivyo mashabiki wao wanavyotaka.
 
Inasemwa kwamba kazi ya afisa uhusiano ndio kazi ngumu kabisa huku duniani. Kazi hii inahitaji mtu mwenye uelewa wa mambo haswa yale ambayo atakuwa akiwashirikisha watu kuhusu kampuni, taasisi na mashirika ambayo ndio anafanyia kazi.

Kwa mfano. Afisa uhusiano wa jeshi la polisi. Msemaji wa jeshi la wananchi. Afisa habari wa TRA. Msemaji wa ikulu nk.

Unapokuwa kwenye nafasi ya afisa uhusiano wa taasisi yoyote unaweza kuifanya taasisi ikaonekana inafanya mambo hake vizuri au vibaya. Ndivyo ilivyo kwa msemaji wa klabu ya simba ya dar es salaam ndungu Ahmed Ally.

Kupitia mitandao ya kijamii, Ahmed Ally amekuwa akionekana akiizungumzia Club ya Simba kimzaha mzaha, kiasi kwamba Club ya Simba inaonekana kituko kupitia yeye.

Kwa jinsi navyomwona, yeye ndio ananufaika zaidi kuliko Club ya Simba. Taarifa zake nyingi zimekuwa ni za kimipasho zaidi kuliko zile official club statement ambazo uwasilishaji wake pia unatakiwa kuwa na nidhamu.
Uwasilishaji wake wa taarifa umekaa kitambotambo na kujidaijidai na ni kwa sababu ya kukosa ubunifu na matokeo ya kuigaiga watu wa aina ya kina Hadji Manara.

Ahmed Ally anajinufaisha yeye kwa mgongo wa club ya simba kwa kutaka sifa hata kama ni za kijinga ili mradi apate follers wengi huko insta na facebook.

Ningekuwa na mamlaka, ningempiga chini huyu jamaa.
Subirieni mpaka striker mwenye manguvu na mrefu kuliko goli afike. Baada ya hapo ndio mumtimue 😅
 
Hawa wote Mm nawaona ni wale wale, hivyo naona mtoa mada ni shabiki wa Yanga hvy hawezi kuona tatizo kwa Kamwe.
Ila binafsi hao wote Kamwe na Ahmed wanafanya kazi zao vzr mana ndivyo mashabiki wao wanataka.
Tangu hizi nafasi za usemaji wa vilabu kuanza tuna msemaji mmoja tu ambaye amefit kwenye hiyo nafasi.
Thobias Kifaru wa kule Manungu Turiani.

Wote wengine, Ally Kamwe, Ahmed Ally na Hadji Manara ni watu wa taarabu na mipasho.
 
Tatizo n mashabiki na sio hao, ukiwa simba na Yanga afu ukifanya kazi yako kimya kimya unaonekana huendani na position yako hvy unatolewa na mashabiki/viongozi, kwahy mm nasapoti kila wanachofanya Kamwe na Ahmed mana ndicho mashabiki wanataka hvy.
 
Mbona wao walimtoa Antonio Nugaz..sijui ndo jina lake..kaka alikua amepoaa analeta ushekhe kwny club wakamtoa wakamleta njiti...kazi yake 24 hrs ili apate content ni kusema mambo ya Simba..yani huyo Ali kamwe ndo mjinga na mpuuzi page yake imejaa Simba...ni mipasho tuu
 
Nugaz alijifanya mzungu kwenye mitaa ya uswahilini, simba bila kumsema Yanga and verse versa lazima kibarua kiote nyasi unaonekana hujui kazi na ndicho watu wanataka hvy.

Kwahy kamwe na Ahmed nawaunga mkono 😂
 
Hiyo ni kweli kabisaa, Haki Manara amefanya vijana watafute umaarufu badala ya kutangaza timu zao
Saivi utasikia kati ya Ahmed na Kamwe nani babalao?? Baba lao kwa lipi yaaan bas tu
 
Tatizo ni aina ya mashabaiki wa hizi timu. Ukifanya kazi kiprofessional bila blabla itaonekana hufanyi lazi. Mashabiki wa simba na Yanga wanataka mtu ambae 24/7 atakuwa anaisema timu pinzani na kuikejeli na wao wanafollow kwa wingi na kusapoti hizo kejeli
Hao vijana wasilaumiwe mfumo ndo unaowaforce kufanya wanavyofanya na wao wanapita na upepo huo kujizolea followers na kupiga madili
 
Hizi ni chuki zisizo na msingi binafsi mi ni mwanayanga Lia Lia ila namkubali sana Ahmed Ally... Coz anajua sana kuburudisha we kama unayakosea Maisha makasiriko yako usituletee Sisi ..

Tunampenda Ahmed Ally VIBAYA MNO [emoji2957][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huyo comedian anaongeaga porojo tu manara amewaharibu sana
 
Back
Top Bottom