Ningekuwa Rais Samia nisingewachukulia poa tena Watanzania

Ningekuwa Rais Samia nisingewachukulia poa tena Watanzania

Mnada wa Mhunze

Senior Member
Joined
Mar 1, 2023
Posts
168
Reaction score
819
Ningekuwa Samia hilo la BANDARI kuhojiwa kwa zaidi ya wiki 2 na Watanzania isivyotarajiwa hakika ningeshtuka na kuwa upande wao kwa kuwasikiliza, kujibu hoja zao mimi mwenyewe na ningetafuta namna bora ya kuliweka ili kuondoa SINTOFAHAMU kubwa nchini!

Ukweli ni kwamba Watanzania wamebadirika si Watanzania wale wa ndiyooo kila kitu.

Huwezi amini wapo watu tena wasiotarajiwa kabisa kwalo wamethubutu kuhoji!

Samia na hasa CCM ishtuke kwa sababu zama za ndiyoooo rasmi kupitia hilo la BANDARI ni wazi zinaelekea ukingoni.
 
Yupo kimya kwasababu hana majibu, ni hivyo tu, kwa maana nyingine anajua kila ubaya waliotufanyia watanganyika kwenye ule mkataba ndio maana yupo kimya.
 
Ningekuwa Samia hilo la BANDARI kuhojiwa kwa zaidi ya wiki 2 na Watanzania isivyotarajiwa hakika ningeshtuka na kuwa upande wao kwa kuwasikiliza, kujibu hoja zao mimi mwenyewe na ningetafuta namna bora ya kuliweka ili kuondoa SINTOFAHAMU kubwa nchini!

Ukweli ni kwamba Watanzania wamebadirika si Watanzania wale ndiyooo kila kitu.

Samia na hasa CCM ishtuke kwa sababu zama za ndiyoooo rasmi kupitia hilo la BANDARI ni wazi zinaelekea ukingoni.
Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, angeshalitolea ufafanuzi kwenye hotuba zake za kila mwezi!
Yule mwamba Mungu amlaze mahali pema peponi!
 
Kwaiyo wew unapenda uchumi wa bandari za kenya ufe ukuze wa dubai .
 
Back
Top Bottom