Ni biashara inayolipa sana na haina hasara kamwe ila changamoto yake inataka mtaji mkubwa sana. Mathalani ukataka kufungua sheli moja ya kawaida kabisa yenye pump mbili tu moja ya petrol na nyingine diesel. Na sheli isiyo na mbwembwe itakugharimu kati ya million 450 hadi 500.
Kwa upande wa faida utapata kuanzia sh 130 hadi 210 kwa lita moja itategemea na supplier aliyekuuzia. Mfano PUMA energy wana bei nzuri sana hivyo faida kua kubwa.
So ukiwa na possibility angalau ya kuuza lita 10,000 kwa siku utajikuta unapata faida zaidi ya million 35 kwa mwezi, hapo umeshatoa expenditures zote so hyo ni net profit . So inshort yanalipa sana ila pia ujipange mtaji.
Kwa upande wa vibali waone TRA, EWURA, OSHA na wakala wa mafuta wa serikali. Ukifanikiwa kuwekeza within a year pesa yako yote itarudi na utaanza kula faida.
Mwisho kabisa mafuta hasa petrol yana tabia ya kupotea kwenye kisima kwa njia ya evaporation hasa nyakati za joto kali, so loss za lita 100 hadi 1000 kwa mwezi ni jambo la kawaida, hilo utaliona ukiwa unafanya deeping. Nakutakia kila la heri na biashara njema!
Ukitaka maelezo zaidi PM