Nilitaka kuuliza hapo.
Nimeona trela za Bhachu na Superdoll zinabeba mafuta mengi kuliko Serin au OKT. Hapo una mawazo gani?
Mkuu Bavaria, kwangu mm kwa kuwa si mtaalamu sana wa mambo haya nadhani moja ya sababu tankers za Bhachu au Superdoll zinabeba zaidi ni sababu ya wepesi wake. Ziko designed kwa ajili ya kazi si mbwembwe kama hizo za Serin ambazo kwangu mimi naona kama zina madoido mengine ambayo si ya muhimu yanaongeza tu uzito bila sababu japo kwa macho zinavutia zaidi. Jaribu kuzifuatilia tankers mpya za Bhachu utagundua zinatofauti kubwa sana na za awali.
Nimeona umeulizia pia khs ubora wa brands mbalimbali za trucks. Tuwe wakweli kama tunazungumzia trucks mpya zote then Scania ni the best ila issue iko kwenye bei ndio maana transporters wakubwa kama Super Star hawacompromise kwenye hili. Scania truck mpya moja unaweza kununua trucks nne za kichina na ukabaki na balance ya kuanzia. So kwa sababu ya changamoto ya bei watu wengi wana opt Mchina. On the other hand, unapolinganisha used scania na mchina mpya then mimi nitaopt Mchina mpya kwani gari mpya ni mpya tu huwezi kulinganisha na used ambayo huna hata historia yake vizuri so kuna kuna risk za kutosha ndani yake.
Mimi pia niko kwenye trucking business ila si tankers ambako nimetokea kuwa na interest ya kutosha hivi karibuni na kwa kiasi fulani nimeanza kuulizia baadhi ya mambo ili Mungu akiniwezesha niingie huko pia. So nikipata data zaidi nitashare na ww pia nitashukuru kama ukishare ili mwisho wa siku wote kwa pamoja tusogee hatua angalau moja mbele.