In the mean time hata sisi wenye vipesa vya ESCROW tunaweza kuweka magari yetu barabarani tukapeleka mzigo congo.
Itabidi tufanye hivo ila tutafute capital kama ya M 100 hivi maana kwa kweli hii biashara mtaji wake bila kitu kama M 100 utakuwa undercapitalised na utashindwa.
Itabidi tufanye hivo ila tutafute capital kama ya M 100 hivi maana kwa kweli hii biashara mtaji wake bila kitu kama M 100 utakuwa undercapitalised na utashindwa.
kuna vituo vingine napita naona hakuna magari yanajaza mafuta, kuna kituo fulani pale ............. wakati mwignien ukipita asubuhi utakuwa wamechinja makafara ya damu za kuku....fungukeni zaidi. usijejaza mafuta yako kwenye kisima halafu wenzio wanakuja kuyachota kimazingara ikizingatia wafanya biashara wengi wa haya makitu ni waarabu tunaojua wanafuga majini kama desturi ya uarabuni.
Duh kweli hii biashara kasheshe. Kwa hiyo truck moja la mafuta inaweza ikafika bei kiasi gani?milion 100 mbona hela ndogo sana hata truck moja na trailer lake haitoshi..
m100 hela ndogo sana na sana na sana
Mpaka truck ikae barabarani na vibali vyote sio chini ya million 100Duh kweli hii biashara kasheshe. Kwa hiyo truck moja la mafuta inaweza ikafika bei kiasi gani?
Ni biashara inayolipa sana na haina hasara kamwe ila changamoto yake inataka mtaji mkubwa sana. Mathalani ukataka kufungua sheli moja ya kawaida kabisa yenye pump mbili tu moja ya petrol na nyingine diesel. Na sheli isiyo na mbwembwe itakugharimu kati ya million 450 hadi 500.
Kwa upande wa faida utapata kuanzia sh 130 hadi 210 kwa lita moja itategemea na supplier aliyekuuzia. Mfano PUMA energy wana bei nzuri sana hivyo faida kua kubwa.
So ukiwa na possibility angalau ya kuuza lita 10,000 kwa siku utajikuta unapata faida zaidi ya million 35 kwa mwezi, hapo umeshatoa expenditures zote so hyo ni net profit . So inshort yanalipa sana ila pia ujipange mtaji.
Kwa upande wa vibali waone TRA, EWURA, OSHA na wakala wa mafuta wa serikali. Ukifanikiwa kuwekeza within a year pesa yako yote itarudi na utaanza kula faida.
Mwisho kabisa mafuta hasa petrol yana tabia ya kupotea kwenye kisima kwa njia ya evaporation hasa nyakati za joto kali, so loss za lita 100 hadi 1000 kwa mwezi ni jambo la kawaida, hilo utaliona ukiwa unafanya deeping. Nakutakia kila la heri na biashara njema!
Ukitaka maelezo zaidi PM
Nisaidie kidogo.
Truck moja linauzwaje? Na trela lake?
Mafuta bei ya jumla kwa Diesel ni 1641 na Petrol ni 1792 kwa Dar, Tanga ni bei rahisi zaidi maana diesel ni 1628 petrol imepungua kwahio chukua i.e. 1641x 5000 na 1792 x 5000 utapata uwe na angalau mtaji wa shillingi ngapi ila faida ni 105.37 kwa kila lita utakayo uza....
Na kwa kuanzia nadhani kama anataka kumiliki petrol station awe na capital ya kujenga visima pamoja na mtaji wa kununulia hayo mafuta. Magari aanze na ya kukodi kwanza baadae ndo mtaji ukikua ununue magari yako