Mi mi
JF-Expert Member
- Jul 14, 2024
- 2,748
- 5,112
Nakukaribisha mwenyekiti mpya Tundu Lissu katika uongozi wako mpya ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo natumahi mengi mapya pia umekuja nayo katika nafasi yako hii mpya ya uenyekiti wa chama.
Moja ya jambo/ kauli ya msingi ningependa kusikia kutoka kwako kama msimamo wako na wa chama unacho ongoza basi ni kauli juu ya vijana wetu hawa wakina Soka na wenzake waliopotezwa toka mwaka jana.
Moyo wangu umejaa hofu yasije yakajitokeza kama yaliyo jitokeza kwa Ben mpaka leo ukimya umetawala juu ya kijana yule asiye na hatia na chama jitihada za kukata na shoka za kupambania uhai wake kutokufanyika.
Mwenyekiti una nafasi ya kufanya jambo kwa kijana wetu huyu Deusdedith naomba chama kisiingie katika historia ile ile ya kuwatupa vijana wao pale wanapo potezwa maana mpaka sasa ni kimya kingi kimepita sio kwa serikali,sio kwa jeshi la polisi wala sio kwa chama chake alichokuwa akikipambania kwa jasho lote Deusdedith, naomba sana mwenyekiti msimtupe mkono Deusdedith moyo wake na mioyo yetu inavuja damu napata nguvu kuwa msimamo thabiti kutoka kwako na kwa chama utatibu hofu hii juu ya kijana wetu.
Mwenyekiti sema neno moja tu juu ya Deusdedith na mioyo yetu itapona.