Kwani hapa mnaongelea mafanikio gani? Labda tuanzie hapo!
1. Nyimbo zake hazihit kivile
2. Hapati show nyingi kihivo
3. Sijasikia akipiga show kubwa ndani or nje ya nchi yeye kama yeye, yaani sio kama Fiesta show inayohusisha wasanii wengi. But nimekuwa nikipita U-Tube naona show anazofanya Diamond kwa jina lake na kujaza kumbi kubwa/uwanja.
4. Ngoma zake ni marachache kuzisikia kitaani zikichezwa eg. kwenye bodaboda, bajaj,daladala, etc or sehemu zinazohusisha mikusanyiko ya watu wengi kama vile harusi/clubs. Yaani nyimbo nyingi alizotoa miaka ya hivi karibuni hazijafanikiwa kukick kwa mtaa kiasi cha kuwa gumzo japo anainvest kuliko zamani. Mfano hazijafikia level ya kubamba kama 'HABARI NDO HIYO' aliyoshirikiana na FA.
5. Ana tuzo kadhaa but sio nyingi kihivo kama ambavyo anadeserve kuwa nazo kutokana na jitihada zake.
6. Hayuko powerful sana U-TUBE, hiki ni kitu ambacho zamani hakikuwepo/wasanii walikuwa hawakitilii maanani sana, but nowdays wasanii wako serious nayo sana kwa ajili ya promo, na pia inasaidia sana msanii kujijua unakubalika kiasi gani/ Or una fanbase kiasi gani/ Unafatiliwa kiasi gani. Nimejaribu kufanya research nimegundua kwa Africa Mashariki Diamond ndo anaongoza kwa kufuatiliwa, karibu kila video aliyorelease YOU TUBE imejizolea viewers wengi.
**INSHORT: Kwa watu tuliosoma Physics tungeweza kusema
JITIHADA ZA AY is Inversely Proportional to his SUCCESS/ACHIEVEMENTS