Issue kubwa ilikua ni Tuntemeke, kusoma Marekani kwa muda mrefu, aliamini kwamba siasa ya Ujamaa ni feki na haiwezi kuleta maendeleo na hakuwa akificha msimamo huo licha ya kuwa mwana-TANU iliyokuwa ikiamini katika Ujamaa.
Tuntemeke alieleza kwamba yeye ndio anafaa kuwa Rais hivyo Mwalimu NYERERE ampishe ili ailetee nchi maendeleo kwa falsafa za ubepari na abadili "mentality" ya wananchi wa Tanzania ambao wengi ni wavivu wapendao kujirusha na kuoneana wivu. TUNTE alidai shahada zake 7 zilimfanya awe na fikra sahihi za kuleta maendeleo kuliko Mwalimu aliyekuwa na shahada mbili tu na muumini wa ujamaa aliouona "unailostisha" nchi!.
Hiyo ilimkera mno Mwalimu ambaye, kwa kutumia "The Preventive Detention Act, 1962", alimsweka mara moja TUNTE kizuizini kijijiji kwake Bulongwa na kumuamuru kutotoka kijijini hapo hadi apate kibali maalumu.