Karibu sana Bro,
Natamani upone ili Mungu akutumia kuwashauri na kuwatoa vijana wengi wanaopotea siku hadi siku. Wengi tumeshindwa kujikwamua kutoka katika hali ngumu tulizonazo kwa kuamninishwa kuwa hadi mtu akakuombee au mtu akusaidie ndo unatoka.
nimeona vingi na nimeshuhudia unafiki mwingi sana wa watu niliodhani wangeweza kunikwamua kutoka point A to B, na mara zote ilishindikana. Nilipopata fursa ya kujijua na kujua uwezo mtu alio nao ndani yake, nimejijenga sana kuchuja ni nini cha kuamini na nini ambacho sio cha kuamini.
maandiko yanasema ''MUNGU HUFANYA KAZI KWA KADIRI YA NGUVU ILIYO NDANI YA MTU'' kwa hiyo inamaana ili upate mabadiliko chanya kwa namna yeyote ni lazima uanze kuyakubali ndani ya akili na mawazo yako. ''kwa maana ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo'' yasema maandiko. kwa namna yeyote mabadiliko chanya yataanza na mtazamo na nia yako utakayoiweka. na bado hujachelewa bro, kwa usianze kukataa hiyo hali leo, kwa nini watu wakuamninishe hadi ukaombewe ndio utapona, kwa nini uone ni kawaida ati kwa sababu umefanya kwa muda mrefu? kwa nini uweze kuacha vingine then hiko ushindwe? LA HASHA, UWEZO UKO NDANI YAKO kazi yako ni kuugundua na kuutumia kwa manufaa yako na ya watoto wako na familia yako ambayo utaijenga kwa neema inayotenda kazi ndani yetu.
God Bless.