Nini chimbuko la Vita vya Uhujumu Uchumi - 1983-84?



Mkandara:

Wewe unayezunguka bro. Wengi tunakiangalia kile kipindi cha 1979-1984.

Na wengi hapa sio wajamaa au mabepari. Na kama tungeweza kutoka katika matatizo 1979-1984 bila kolombwezo za IMF, WB na masharti ya wahisani, basi Tanzania ingekuwa nchi yenye kujitegemea.
 

Sahiba:

Katika nchi wanayoua albino kupata utajiri, kufanya vitu kwa kubahatisha ni kitu cha kawaida.

Lakini katika vitu ambavyo Mkandara na Mwanakijiji wanaviita complex, nawaambia wasicheze bahati nasibu ni maarifa tu yatakayotukwamua.
 
Kwa maoni yangu kama uzalishaji ulikuwa ni wa kukidhi demand ya Tz peke yake then hapo ndio makosa na tukiangalia kiundani basi ni sera ya ujamaa na kujitegemea ikipingana na ubepari ambao ulikuwa umetapakaa kwa majirani zetu.Ilikuwa ni vigumu sana kwa mwalimu kuweza kujenga jamii aliyokuwa akiiataka.
Mjadala huu umegusia sehemu mbali mbali zenye hoja ya msingi ila ziko scattered..Mkandara,Zakumi,Rev Kishoka wote kwa pamoja maoni yenu yamekidhi mjadala huu kwa kila namna.

Ila swali moja la msingi kabisa hapa ni je ni kwanini viwanda vyetu vilikufa? Najuwa factor ya vita ya Uganda lazima ilikuwa one of the main impacts to the economy....Ila swali kwa ndugu zangu ni hili...Ni kivipi viwanda vilikufa? Sijasikia mtu akitaja umeme,naelewa hoja hapa ni uhujumu uchumi...Lakini kama tunazungumzia bidhaa zinilizozalishwa nchini mwetu,then tukagusia viwanda hence umeme...Tatizo ambalo ni very sugu.

Mkandara umesema bidhaa zilizokuwa zinatakiwa zigawanywe kwa wananchi zilifichwa...Swali ni kuwa zilifichwa kabla ya kuuzwa ama baada ya kuuzwa?

Kama ni baada ya kuuzwa,then wenye shida watakuwa ni wananchi ambao walitakiwa wazipate bidhaa hizo...Kwa mantiki hiyo basi serikali ilishapata chake na sioni ni kivipi ilihujumiwa....Kwasababu nasikia kuna wanaosema kuwa wafanya biashara walinunuwa na kuzificha bidhaa hizo na kuzipeleka nje kwa faida zaidi.Hata hivyo kama zilifichwa na viongozi kwasababu zao binafsi then ni kivipi mwalimu alishindwa kuona hilo?

Ninavyoelewa kwa upande mwingine pia serikali ilikuwa ikihujumiwa kwa mapato ya kodi kwa kutowa bidhaa nje na kuingiza nchini kulikokuwa kukifanywa na walanguzi.
Shida kubwa hapa ni siasa,Tanzania kuingizwa vitani haikuwa bahati mbaya,na hata Kenya walifurahia kiaina.

Kwa ujumla chimbuko la vita hii ya uhujumu uchumi kwa maoni yangu limechangiwa na mgongano wa siasa za ujamaa na kujitegemea vs ubepari...Kiutaratibu tulitakiwa tupanue soko la bidhaa zetu nchi za majirani tulibahatika kuwa na TAZARA,tungekuwa mbali kama serikali ingewasaidia wananchi wake na wafanyabiashara na Tanzania labda ingekuwa mbali...Shida ni kwamba hatuwezi kujuwa...Ndugu zetu wakenya nao kama si ukabila wangekuwa mbali,matabaka ndio mojawapo ya matokeo mabaya ya ubepari sasa kwenye kutafuta balance hapo inahitaji Afrika ije pamoja.
 
Last edited:
Zakumi,
Na wengi hapa sio wajamaa au mabepari. Na kama tungeweza kutoka katika matatizo 1979-1984 bila kolombwezo za IMF, WB na masharti ya wahisani, basi Tanzania ingekuwa nchi yenye kujitegemea
Mkuu isingewezekana kwa sababu UJAMAA ulikuwa unakufa kifo cha HIV.. Utamu wa ngono ktk Ujamaa ilfikia kikomo bob haikuwa kazi ya IMF wala WB kutufuata, tulikwenda wenyewe..
Katika nchi wanayoua albino kupata utajiri, kufanya vitu kwa kubahatisha ni kitu cha kawaida.

Lakini katika vitu ambavyo Mkandara na Mwanakijiji wanaviita complex, nawaambia wasicheze bahati nasibu ni maarifa tu yatakayotukwamua.
Hapana wewe ndiye unajaribu kutumia vitabu ktk swala complex kama la kuua Albino.. unatafuta sijui motive cha chuki labda ubaguzi wa rangi na kadhalika... kjwi kwi kwi! Sisi tunaoishi na Wadanganyika wenzetu tunafahamu kuwa ni swala la imani ya Uchawi.. sasa nenda kwamwambie mchumi habari za Uchawi na Utajiri kisha unaanza ku apply maswla ya demand na supply! damn yaani ngozi za Albino zingeweza kuzalishwa zaidi bila shaka demand pia ingepungua... Mkuu wangu acha kutuweka Uchizi.. hawa watu ni criminals na motive yao kubwa ni fedha - kujenga Utajiri by all means..kama walivyokuwa mafisadi wa kuhujumu Uchumi.. books kwao haziwezi kufanya kazi..
 
Wanajamii suala la viwanda kufa Mwalimu was very smart and that is why I don't understand alot of his decisions and the problem was no one could open his/her mouth and say anything at the time.Wajameni mnamtafuta mchawi wakati mchawi mnamjua guys let's be real and just say it.I think is fare to speak out if you don't do it know then when.Mwalimu alipokwenda kudai uhuru Malkia alimuuliza Julius baada ya kukupa uhuru unataka nikusaidie nini ?na hili ndio jibu la Mwalimu 'nanukuu 'NATAKA WATU WAKO WOTE WAONDOKE'Yes ndivyo alivyojibu matokeo yake tunayaona leo.Professionals wote madoctor,engineers wote wakaondoka wakatuacha matokeo yake wanaomtetea wanasema ati kachukua nchi ikiwa na madokta wazalendo wanne,sasa si umefukuza wote ulitegemea nini waganga wa kienyeji.haya wakati wa ukoloni kulikuwa na vifo vichache na madokta wanne na sasa tuna madokta bwerere na vifo mahospitalini kila dakika hadi pamba ya kidonda uwende nayo hospitali,rushwa kibao huna mshiko utakufia reception na madokta wengine vihiyo mgonjwa wa mguu anapasuliwa kichwa wakuu hii ndiyo misingi yetu.
 
Sahiba,
Haya maneno unayazungumza kwa kunukuu maneno ya watu au unazungumza tu kufurahisha baraza..
Je, unajua ni muda gani transition ya Uhuru wetu ilichukua?.. unajua hata jeshi letu liliendelea kuwa chini na Malkia hadi kina sarakikya walipoanza kugoma na kum force mwalimu kuanzisha JWTZ..Nambie sehemu ambayo wazungu waliondoka mara tu baada ya Uhuru kwa sababu ya majibu ya mwalimu..
Mkuu ni hadi Azimio la Arusha ndipo mabadiliko mengi yalifanyika meaning up to 1967 wazungu walikuwepo nchini..
Kisha hizi Imani za wazungu. mbona ni akili za kushikiwa. hao wazungu walipoondoka sijui madoctor ulisikia tatizo la vifo au tumeshindwa kuendesha kitu...zaidi ya hapo unaweza kunambia huyo Malkia alijenga kitu gani kwetu..hao ma engineer walikuwa wakiendesha kitu gani..
Mwalimu alijenga almost everything from the ground.. kitu poekee ni reli ya Mjarumani na shirika la meli la huyo malkia na Nyerere alipoingia tuliweza kuongeza meli mara tatu ya zile alizoacha Muingereza..nambie shirika hata moja la Muingereza ambalo tulishindwa kuliendeleza toka Mkoloni alipoondoka..
Yes, tunakubali yalifanyika makosa ya kutaifisha kila kitu hata biashara binafsi ambazo hazikuwa commanding Heights, na biashara hizi hazikuwa na Muingereza ila wazungu wa kila Kabila zipo za Wataliani, Wajarumani, waarabu, wahindi na hata waafrika wenyewe.. Haya ni makosa ya siasa za Ujamaa ambazo leo unakuja jutia..lakini above all hazikutuacha vilema isipokuwa zilivunja mifupa ya uchumi wetu na tukaanza kutembelea magongo..
Toka wakati ule hatujafanya tiba yoyote kiuchumi kufikiria kuondokana na magongo...Tunachofanya leo hii ni ku hire msaidizi wa kutuburuza ktk viti vya vilema wakati mifupa imeisha unga na tunaweza kufanya therapy ya kiuchumi kutuwezesha kutembea tena bila magongo..
 


Jmushi:

Suala la umeme tumeligusa sana humu ndani. Lakini focus ilikuwa 1979-1984.

Katika kipindi hiki umeme ulikuwa sio tatizo kubwa sana. Tatizo kubwa lilikuwa ni viwanda kujengwa katika sehemu zisizo za umeme. Mfano ulikuwa nikiwanda cha nguo Musoma. Umeme wa kuzalishwa na maji ulifika Mwanza na Musoma miaka ya 90. Lakini tayari sehemu hizo zilichakuwa na viwanda vya nguo vyenye kutumia umeme mkubwa katika miaka ya 70 na 80. (najua hapa watakuja wakina Mkandara kubisha). Hivyo maamuzi ya kisiasa ya kujenga viwanda yalitawala mikakati ya kiuchumi.

Kuhusu matumizi ya reli ya TAZARA, nadhani hapo watanzania ni uzembe wetu mkubwa unaouonyesha.

China ilikuwa ndio inaanza kujitangaza duniani kuwa inaweza kufanya vitu lakini kwa sababu ya dominance ya nchi za magharibi katika masoko ya dunia ya tatu, China ilipata kazi kujitangaza. Hivyo TAZARA ni mradi wa kwanza mkubwa uliochuliwa na China ili kujitangaza nje kuwa inaweza kufanya kazi. Lakini kama kawaida yetu, tukaona kuwa KAKA zetu wajamaa wametusaidia, hivyo tukabweteka. Baada ya TAZARA, China ilianza kupata tenda kutoka katika nchi zingine za dunia ya tatu kujenga miradi mingi.

Kwa sisi tuliuchulia kama mradi wa kisiasa hili Zambia isitegemee sana South Africa. Na hatujafanya juhudi zozote zile za kufanya TAZARA itumike katika mazingira ya sasa ya kisiasa. Na vilevile reli hiyo inaathirika sana na ukiritimba wa Bandari ya DSM.

Hivyo tunaweza kujibu maswali mengi lakini tunaweza kutoka nje ya mada.
 

Sahiba:

Chunga sana unapomtaja Mwalimu. Kuna walinzi wa historia hapa.
 
Mtu anaweza kusema uongo kwa muda mrefu, akawa wa kwanza kuaamini, mwisho anauita historia!
 
Kishoka:

Anzisha topiki nyingine kama vile kuchambua paper ya Prof. Wangwe.
 
Sahiba:

Chunga sana unapomtaja Mwalimu. Kuna walinzi wa historia hapa.

Ni lazima wawepo ili kuweka historia sawa sawa.

Mkandara sina jinsi ya kukupongeza lakini wewe ni moja kati ya vichwa vinavyojua kuchambua mada na kutoa mifano barabara. Nyerere hakuwa malaika lakini alifanya mengi makubwa katika mazingira magumu ambapo hakuna raiswa tanzania tunayeweza kumlinganisha naye kwa sasa.
 

Mkandara,
Mzee naona majibu yana jazba kumbe Azimio la Arusha lilikuwa ni la kuwafukuza wazungu hilo mimi sina uhakika nalo maana asilimia kubwa sana ya mali zilizotaifishwazilimilikiwa na wahindi,waarabu na wazalendo sasa hili la wazungu vipi hapa wakubwa.Na ikiwa unasema hakuna viwanda vilivyotushinda kuviendeleza na tukaviua inabidi mjadala tuufunge maana naona Bwana mkandara mapenzi yamezidi na mwisho kama huoni walivyojenga wazungu mimi nakumbuka maana hata zile parking meter tu tulizivunja mzungu alipoondoka tu hatukujua manufaa yake na loe tunafunga magari yetu kwa machuma haya nipe logic bwana mkubwa.
 
Sahiba, mkuu sizungumzi kwa jazba hata kidogo, ndio lugha yangu na wengi hapa JF wanafahamu kuwa mimi huandika kwa msisitizo tu zaidi ya jazba kiasi kwamba ukisoma juu ya gamba unaweza fikiria ni jazba au nachoandika hakina makosa..
Huu ni mjadala ambao kila mmoja wetu huweka hoja zake pinzani au zinazokubaliana kutokana na Ufahamu wetu iwe kwa elimu au Experience...

Mimi nimejibu tu hoja yako kulingana na usemi wako kuwa mwalimu aliulizwa na Malikia asaidiwe nini akakataa, hivyo wazungu wakaondoka.. hao wazungu madaktari na wengine umewasema wewe sikuandika mimi.. Na jibu langu limekuonyesha wazungu hawakuondoka kama madai yako na mimi ndiye niliyeongeza raia wengine wa nje zaidi ya Muingereza ambao waliathirika na Azimio la Arusha..
sasa unapokuja na madai ambayo yanapindisha ukweli sijui unachojaribu kusema hapa.. Bila shaka Azimio la Arusha liliathiri watu wengi ikiwa ni pamoja na wazalendo wananchi weusi wenye mali zao.
Uendeshaji wa viwanda sio swala kabisa kwa sababu Muingereza hajkujenga kiwanda hata kimoja isipokuwa ni wafanya biashara wa mataifa tofauti.. Muingereza alikuwa akichuma kodi tu kuuza mali zetu nje.. tena basi infrustructure yote alijenga Mjarumani, hivyo kutawaliwa na Muingereza hakukuleta mafanikio yoyote ambayo leo hii tunaweza kusimama na kusema Unaona muundombinu uleee... umejengwa na Muingereza!..
Kwa hiyo mwalimu alijenga karibu kila kitu from scratch tofauti na nchi kama Kenya..inasikitisha tu Watanzania tunaposhindwa ku recognize that!...
Na uchovu kama huu ndio maana watu kama Lowassa, Chenge na Mramba wanatunukiwa na kuitwa mashujaa kwa sababu ni mila yetu kumsifia mwizi, jambazi maadam analisha familia yake kwa Ujambazi.
 


Mkandara:

Basi acha basi kuwa spin-doctor kwa muda fulani. Waingereza nao waliacha vitu tena muhimu tu. Matatizo yako unaangalia viwanda tu.

Waingereza waliongoza mfumo wa utawala unaotumika mpaka sasa. Waliacha bunge. Sheria za nchi. Serikali za mitaa zilizokuwa zinaendeshwa na wananchi wenyewe.

Hata miundo mbinu aliyoacha mjerumani, mwingereza aliisimamia vizuri tu.

Mambo yote aliyofanya Nyerere yalitegemea miundombinu aliyoacha mwingereza.
 
Zakumi,
Mkuu umesema niache kuwa spin doctor sawa!.. Na wewe umefanya nini yaani hizo sheria za nchi na sheria za mitaa ndio urithi unaweza kuuweka hapa mkuu wangu!..
Kibaya zaidi umefikia kusema Miundombinu aloacha Mjarumani ati Muingereza aliisimamia vizuri bila hata aibu mkuu wangu, Hapa unatazama kusimamia mradi au unatazama mjenzi nani..
Hivi ndivyo visingizio vya kuspin..read my lips..nimesema Muingereza hakutupa wala kutuachia kitu ambacho leo hii sisi wananchi tungeweza kujivunia hata kama tusingekuwa na Azimio la Arusha, Muingereza bila kufukuzwa, aliondoka kwa sababu muda wa Protectorate kufikia mwisho wake..hawakwa na kitu nchini zaidi ya bendera zao na kukusanya kodi za kichwa kwa Malkia..Kutawala tu kama Warumi walivyomwejka Herod kule Israel na middle east.
Sheria kitu gani cha kujivunia wakati tulijenga constitution yetu wenyewe.. Kufanana sio hoja kwani hata yeye aliiga mengi toka kwa Mfaransa! labda useme sisi Ndivyo Tulivyo mahakimu wetu waliiga hata kuvaa majoho na nywele za bandia blonde ili sijui tufanane na Wazungu...
 

Bro:

Ukishindwa lazima utafute mbaya wako na visingizio. Hizo nchi zilizoachwa pazuri ziko wapi?

Na hata kama angetuachia vitu unavyotaka wewe, unafikiri tungekuwa mbele?

Niambie kitu gani ungeachiwa ungekuwa mbali?
 


Watu tunataka good time. Hayo mambo ya rais kufanya mambo kibao na kukuacha na msuli kama mgogo, hayana mpango.
 
Zakumi,
No bob, mpango wa Ushanga theory hata haupandi! - kwi! kwi! kwi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…