Nini dhumuni la Serikali kuanzisha tahasusi hii ya biashara ikiwa na somo la 'Islamic Knowledge'?

Dini ya faida kwa mwanadamu ni ile inayohubiri KWELI na HAKi ya Mungu mwenye enzi yote.
Hii haihitaji kuwa Mkristo, Muislam, Mpentekoste, Mhindu, .....
KWELI na HAKI vinajitegemea tangu asili kinyume na hizi dini za kumtweza na kumnyonya mwanadamu kitumwa.
Chukua ile KWELI na HAKI kwenye dini za kikoloni, mengine waachie.
 
Mambo ya dini yangesimamiwa na taasisi za dini.Kwasababu serikali haina dini masomo yote ya dini yaondolewe kwenye ratiba za shule za Iman ili kila dini ibebe mzigo wake.Ili isije leta malalamiko kwenye mambo ya dini na ajira kwani inaweza fika muda watu wakalalamika kuwa walimu wa somo flan la dini wanaajiriwa kuliko wa dini nyingine.
 
Kwani dini ni uislamu tu? Samia anatafuta kujihalalisha kwa mgongo wa dini baada ya kuona viatu vya urais vinampwaya sana
 
Unamumunya maneno tu, la sivyo usingeleta hii mada. Iwe kwa ubaya tu. Kwa nini hiyo tahsusi?
 
Hakuna hoja hapo. Hapo ni kutengeneza tu matabaka. Na wanaoshauri hili wana ajenda zao.
 
Nchi ya matahasusi. Mwenzao alizilundika pamoja leo ametokea mwingine kazichangua. Eti nchi ina dira ya elimu.
 
Lengo ni kutengeneza mlango wa serikali kugharimia kusomesha watu wa dini hiyo kwa wingi wanafunzi na walimu wao na kuwaajiri kwenye taasisi za fedha kwa wingi kwa kigezo cha Islamic banking washike misingi ya uchumi na biashara na badae siasa..mko hapa endeleeni kushangaa mlishapofushwa ufahamu wenu mnasindikiza tu, tukiwaambia tokeni ccm waachieni chama Chao tuone kama watashinda hata wakiungana na TCA WASALITI..bado hamuelewi..Haya endeleeni kukodoa macho!
 
Afadhali tahasusi za sayansi zimebaki zilivyo. Lakini kwa masomo ya dini (Islamic & Bible knowledge) yangeachwa hivyo kuwa optional. Pengine Chuo Kikuu Cha Kiislamu (MMU) labda kina mahitaji hayo.
 
wataenda kufanya kazi Amana bank, Benk ya watu wa Zanzibar etc.

Fanya mambo yako sio kila kitu mnahoji wakulungwa.
 
Kama waziri ameamua kutumia mitihani kwa walimu ili kukomesha vimemo vya viongozi kutaka watoto na jamaa wa viongozi wakubwa waajiriwe, VIONGOZI WA KIISLAMU wanashindwaje kutuma vimemo kwa DADA YAO apachike elimu ya kiislamu liwe somo wakati MASHEHE WAPO JOBLESS MITAANI na wanaitwa WAALIMU.
Shuleni huko sasa zitakuwa kazu tuuuu 😁
 
Ukiona mtoto anasomea dini manake elimu imemshinda ameamua akomae tu na tamaduni za ibada kitu ambacho yeyote anakiweza akitaka kufuata mkumbo.
 
Hiyo 'ni' katikati ya nasikia...na ukimaliza umeweka ya nini Sasa?
Usimlaumu bure.

Watu wanaofanya makosa ya uandishi kama hayo, mara nyingi hufikiria zaidi akilini kuliko yale waandikayo.

Kuna tofauti kati ya kuwa na dhana fulani mawazoni, na kuiwasilisha ipasavyo.

Huwa wanadhani wameandika yote waliyokusudia akilini.

Ukiangalia vizuri, pengine alitaka kuandika:

^Nachosikia ni [kwamba] ukimaliza kusomea hii, ukienda bandarini hukosi kazi DP World.^
 
Kwani dini ni uislamu tu? Samia anatafuta kujihalalisha kwa mgongo wa dini baada ya kuona viatu vya urais vinampwaya sana
Uislamu ndio dini pekee ilokamilika, nioneshe basi benki moja tu ya Kikristo au ya kibaniani, nyinyi mnafata tu mkumbo
 
Islamic finance / economy ni somo linatolewa hata na vyuo vikuu vya nchi za magharibi
Islamic finance ni sekta ya kifedha inayokuwa sana duniani na iko nchi nyingi pia kwa hiyo mtu kufahanu ni kongeza kitu kwenye CV yako ina ongeza fursa kwa msomi.
 
Na bado
Mtasaga meno sana
Kwani ajira portal mambo yanaendaje,
Na sasa kila taasisi inaajiri yenyewe, zinakula vichwa vya juu juu
nyie kasubirieni kwenye uzi wenu wa ofisa daraja la II

 
Mbona hata sasa hivi misingi ya biashara na uchumi wa nchi hii umeshikiliwa na wao?au unataka waushikilie mara ngapi?
 
Kama kuleta mchele mbovu au ngano iliyoisha muda wa matumizi . Hawa wanafanya hivi sababu hawajui Dini. Wanaokwepa Kodi ya mafuta ya Kula na Sukari , Kwa kuleta kupitia Bandari Bibi, wauza ngada, wanaovunja Nyumba za ibada nk
 
Kuna tahasusi ya lugha na lugha sio islamic Bali ni Arabic
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…