Bei ya mkulima iko vile vile chini. Hizi ni bei za wafanyabiashara wanaokusanya vyakula hivi kwa bei ndogo sana kutoka kwa wakulima, na kuvisafirisha nje ya nchi na kuziuza kwa bei kubwa sana au kutumia sisi kwa bei hiyo hiyo. Pia ni bei za wakulima wakubwa kama akina Bashe wenye mashamba makubwa (farmers not peasants) kwa ajili ya ku export. Mkulima (peasant) wetu yuko vile vile. Inabidi tuzuie hawa wafanya biashara walanguzi. Tunaweza kuruhusu wakulima wakubwa tu kusafirisha mazao waliyo yazalisha wenyewe, si yale waliyoyalangula.
Huo ni utaratibu unaotumiwa na ccm kuhadaa wananchi ili kuonyesha kwamba uchumi unakua sasa walivyo wajinga wanashindwa kuelewa kwamba hali halisi inapingana vibaya na hizo takwimu zao feki.