Nini hasa kilisababisha vurugu za Mwembechai mwaka 1998?

Ni nini kiini hasa cha vurumati lile?
 
Hakuna my take:Ukifanya fujo na umeambiwa usifanye fujo,ukajiona imara sana,mjuaji sana UTAPIGWA TU.Na mimi nasema WAPIGENI TU,maana hakuna namna nyingine.In Pinda voice.
 
Wewe ulikuwa unatengenezwa kuwa gaidi mtoto!Umekitaka ulichokuwa unakitafuta,nchi kwanza dini baadae.
Ukifanya fujo utapigwa tu!
 
Padri Luambano Parokia ya Mtakatifu Thomas Mburahati. Hahaaaaaa...huyu jamaaa sijui aliishia wapi. Ana matukio sana.
Wakati tupo wadogo hapo mtaani Mburahati ilikuwa ukishikwa na kwikwi unakunywa maji kidogo kidogo kwa awamu huku unasema Luambano....Lumbano mpaka mara saba tukiamini kuwa ndo kwikwi inakata.

Mara ya mwisho kumsikia Parokiani ni siku alipochepuka na mama mmoja nyumba ya NHC ya tano kutoka hapo Parokiani siku ya jumamosi na kupitiwa na usingizi na kuchelewa misa za kesho yake jumapili asubuhi.
Nakumbuka vizuri misa zilikuwa tatu kama sikosei asubuhi na ya jioni kwa ajili ya watoto. Lumabano mpaka misa ya tatu ya vijana hakufika. Taarifa ilifika jimboni haraka sana baada tu ya kukosa ile misa ya pili. Kufika mida ya saa tano. Pengo akaingia kusalisha...mida kama ya saa sita Luambano akaingia nakumbuka sijui ilikuwa Escudo ile ilikuwa nyekundu anaingia anakuta Askof yupo atareni.

Baada ya hapo alihamishwa akapelekwa Pwani ya Mkuranga nafkiri ndo ikawa mwisho masikioni mwetu.

Okay....tukio la Mwembe nilikuwa Mburahati. Ndiyo ilikuwa Mara yangu ya kwanza kuona moshi wa mabomu ya machozi. Nakumbuka tulikuwa tunacheza uwanja wa Santosi....mara tunaona moshi upande wa magomeni....baada ya muda kidogo watu wanakimbia....

Yakawa makundi mawili...moja linatoka upande wa magomeni kuja Mburahati...lingine linatoka majumbani linaenda barabara kuu kuona kinachokea .....nikajiunga na la pili. Tukafika maeneo ya Mburahati msikitini...kufika karibu na kituo polisi Mburahati kundi kubwa likawa linakuja kwa kasi toka upande shule ya msingiburahati...lilikuwa linatoka Mgomeni Kagera....kuja upande wa kituo cha polisi....polisi wakatoka nje...wakahamaki...wakaanza kujificha...kundi likavamia kituo cha polisi...wakaingia ndani wakakuta bunduki moja wakaichukua wakaitupa juu ya bati la Mzee Kunambi wakati huo huo wengine wakawatoa waarifu wote mule kituoni...

Wakawa wanapiga mabati ya nyumba kwa mawe huku wanakimbia kuelekea upande wa Kigogo First Inn.....

This is what I remember kuhusu zile vurugu...kiukweli it was horrible
 
Serikali ilikua inashughulikia waislam waliosema yesu sio mungu msikitini mwembechai,serikali isiyokua na dini
 
Hii ilikuwa ni suala la Bucha za nyama ya nguruwe.Mtoto alitumwa kununua nyama ya ng'ombe,kwenye bucha akapewa nyama ya nguruwe,bucha zilikuwa zinauza nyama zone mahali pamoja.Ilikuwa wakati wa Rais wa awamu ya pili,Mh Ali Hassan Mwinyi.Akatoa hutuba,ya kusema ruhsa,mtu kula chochote,hata panya mtu,ale.
 
Mimi nilikuwa bado mdogo kwahiyo napita2
Mini nilikuwa bado mdogo kwa hiyo nilishiriki kikamilifu katika hiyo rioting.(and looting of those wonderful days).
Unasema Waislamu wameonewa na Nyerere? Kwani nani alikuwa rais 1998.?
Huo mkasa wa Mwembechai nadhani ndio ulikuwa ugomvi wa mwisho kati ya Waislamu na serikali.
 

walivo kusimulia kijiweni !
 
Shangaa zaidi kusikia kwamba kuna gazeti liliripoti waziri mmoja kukimbia na kuponyoka sakata hilo. Waziri huyo yasadikiwa alikuwa Kikwete.
 
Dogo mwaka 98 ulikuwa na umri gani? Hivi unafahamu kwamba Mwinyi alistaafu mwaka 2005?

Hivi unafahamu hiyo kauli aliyosema ilikuwa miaka ya 93? Na unajua ilitokana na mabucha ya kitimoto yaliyovunjwa mwege?

Tuache wazee wako tukuelezee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…