Nini hasa kilisababisha vurugu za Mwembechai mwaka 1998?

Shida kulikuwa na rumous kuwa hao jamaa walikuwa wanapata mafunzo baada ya ibada na dhana zipo chini ya mikeka, sasa, lilipoanza lile vuguvugu bas ndio watu wakapatia kick ya kuwabidua mitama na kuwafyeturia risasi za moto wahakikishe ni kweli wameiva kwenye taikondo na matumizi ya silaha kumbe ni kama Marekani ilipovamia Iraq tu. Ulikuwa ni ukatili kweli.
Dunia haina huruma.
 
Ni kweli kabisa hawa madogo wanaovaa jeans za kamatia chini hawawezi kujadili lolote kuhusiana na huu uzi.
 
Nakuhakikishia kuna watu wangebahatika kuwa viongozi wa kwanza hii nchi km wale mzee Mohamed anatulisha matango pori

Tungekuwa na mpasuko zaidi ya Nigeria

Nadhani unajua Rais wa kwanza wa Nigeria alikuwa mtu wa aina gani
 
Sio rumours mambo mengi yalikuwa yanaendelea
 
Na hao wakristo waliokamatwa walipewa majina ya kiislam, mfanyakazi mwenzetu naye alikamatwa baada ya kutemka ktk gari ya kazini alipofika polisi magomeni akapewa jina la kiislam ofisi ilipomfuata siku ya pili hawakumpata Hadi baadaye ikaja taarifa kazini akifuatwa wataje jina X. ndio wakampa wakamtoa na kesi haikuendelea
 
Aisee!!! Kitambo sana, na hii hairuhusiwi kujadiliwa popote na haitakiwai uujue ukweli, kulikuwa na kitabu kinacho zungumzia hii kadhia lakini naskia hakiruhusiwi nchini...
Nakumbuka Waziri wa Mambo ya Ndani, alikuwa Bw. Ali Ameir, na waziri mkuu mkuu alikuwa F.Sumaye..

Hhaah!! Mzee kipindi hicho alikuwa Waziri, dah maisha yapo fasta.....
 
Halafu Pengo alipouzwa anasemaje kuhusu mauaji ya Mwembechai akajibu acha wauawe tu, tangu nilivyomsikia akijibu hivyo huyu Mzee nilimtoa thamani. Napenda Sana kusikiliza mahubiri ya dini zote lakini nikimkuta Pengo nabadilisha au nazima kabisa
 
S
Unyama uliofanywa na Serkal I hata wakikukuta na casset ya mkasa wa mwembe Chai wana deal na wewe
Sio unyama tatizo wananchi wa tz mnavoishi kwa amani hivi na uhuru wote mlionao wa kutukana, kudharau mamlaka na mengine meengi hadi mnajipa kiburi dawa yenu ilikua ni kukumbushwa kwa stahili ile ya mwembe chai kuwa amani ya nchi huwa haichezewi! Kwani baada ya pale somo si lilieleweka vizuri sana hadi leo na ndio maana bado tunakumbushana kwa mada kama hizi kuwa serikali ipo. Ungekuwa unaishi zenye vurugu huko waliozoea vichapo leo usingehoji elimu ile mubashara ya mwembe yanga.
 
Watu wameshasema aliyelianzisha ni Askofu Lwambano. Ukitaka kujuwa zaidi kitabu cha Hamza Njozi kimetajwa juu huko, kitafute, kipo cha bure kwenye mtandao.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Bibi acha kupotosha, Lwambano hajawahi kuwa Askofu, pia mseme tu ukweli karate zilikuwa hazifundishwi? Je mihadhara yenu haikuwa chanzo pia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…