COMORIENNE
JF-Expert Member
- Dec 25, 2022
- 923
- 1,054
Tupe mawasiliano mkuu mahala nilipo maji ni issue kubwa mnooooWale jamaa survey wao ni mchina mwenyewe..kabla awajachimba unapewa details zote tena kwa uhakika..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tupe mawasiliano mkuu mahala nilipo maji ni issue kubwa mnooooWale jamaa survey wao ni mchina mwenyewe..kabla awajachimba unapewa details zote tena kwa uhakika..
Halafu wakikutana na mwamba wanasepa wanakuachia shimo!Serious??? Laki tatu hii hii?? Wanatumia machine au ni wale wa kuchimba na sururu???
Msaada mkuu wa contact huku tuna shida ya maji zaidi ya jangwani mkuuKuna bei za vitu vya ajabu ajabu sana bongo,
Kuna huu urembo wa Tv shiw case kwa kutumia panel kuna mdau pale sinza alisema kazi yote ni 6m
Nikaingia mtaani nikanumua material na fundi iligota laki 8.
Chamber zisizo jaa kuna fundi famous mtandaoni akasema 4m, nikasaka fundi wengine wakafanya 1m
Kisima niliambuwa futi 12 milion 9,
Kuna fundi wengine wakaja na kimtambo chao wanazunguka nacho kinachimba, nikapata maji ya kutosha hayasumbui niliwapa laki 6
Hao Nao wamekua kama wenye nyumba za kupangisha hawafanyi.kazi Bila Dalali inchi hii wananchi wanapigwa sanaKazi ya uchimbaji visima imejaa udalali mkubwa wa kupindukia, ukitaka kuchimbiwa kisima kwa bei ambayo ni rahisi na halali bila ya kuwepo mtu wa katikati hakikisha unachimbiwa na kampuni ya mwenye mashine au unafanya biashara noja kwa moja na mmiliki wa mashine ya uchimbaji.
Omba namba zao bossBei za wapi izo njoo Tabata kuna kampuni ya kichina million 4 tu unachimbiwa mpaka mita 60..wanakuja na wataalamu wao wanapima kabisa..usifanye mchezo na wachina..wanachimba mpaka kwa mkopo unatoa 2million inayobaki mnaandikishinana unaimalizia lini..Watu mambo ya dawasco tulishayasahau.
Mzee Si utoke Namba uwasaidie wadauFilter wapi wachina wanadawa zao wanamwagia kwenye kisima sema inatakiwa wiki 1 kisima kisitumike toka muda walipoweka dawa..baada ya apo ukikutana na chumvi sijui magadi niite mbwa..mimi nilishawai kumchukua senior graduated kutoka chuo cha maji aje anipigie survey kabla ya kuchimba akasema apa maji yapo kuanzia mita 100 na kuendelea..kuna jamaa yangu akaniletea survey wa iyo kampuni ya kichina MR LIU akasema apa tunachimba mita30 tu maji yapo ya kumwaga..
Filter wapi wachina wanadawa zao wanamwagia kwenye kisima sema inatakiwa wiki 1 kisima kisitumike toka muda walipoweka dawa..baada ya apo ukikutana na chumvi sijui magadi niite mbwa..mimi nilishawai kumchukua senior graduated kutoka chuo cha maji aje anipigie survey kabla ya kuchimba akasema apa maji yapo kuanzia mita 100 na kuendelea..kuna jamaa yangu akaniletea survey wa iyo kampuni ya kichina MR LIU akasema apa tunachimba mita30 tu maji yapo ya kumwaga..
Matope ya kuchimbia? Mzee hii ndio kitu gani pamoja na yote uliposema still gharama za kuchimba ziko juu sanaGharama ya kuchimba kisima inategemea aina ya kisima, kina (urefu kwenda chini), aina ya mwamba eneo la kisima (geology), aina ya mashine itakayochimba na mabomba yatakayotumika.
VISIMA VIFUPI
Visima hivi huchimbwa kwenye michanga/udongo
1. Kisima kifupi aina ya ring well ndiyo bei rahisi kuliko vyote kwani uchimbaji wake ni wa mikono. Bei ni kama laki tano na kushuka chini.
2. Kisima kifupi aina ya tube well inaweza kuchimbwa kwa mashine ya mkono au ya mafuta (diesel/petroli). Kina cha kisima ni chini ya mita 20. Bei ni kama 2 milioni inategemea kina na mabomba yatakayotumika.
VISIMA VYA KATI
Visima hivi huchimbwa kwa mashine (rig) kwenye mchanga (Maeneo ya pwani na mabonde/mbuga na miamba laini)
Visima vya aina hii hufikia kina cha mita 50. Bei yake hufikia milioni 5.
VISIMA VIREFU
Visima hivi huchimbwa kwa mashine kubwa (rig) kwenye michanga, miamba laini na miamba migumu. Kwa Tanzania visima hivi hufikia kina cha mita mpaka 300. Bei ya kuchimba kisima hufikia hadi zaidi ya milioni 20.
Sababu kubwa ya bei ya visima kuwa ghali ni kwa kuwa vifaa vya kuchimbia ni kubwa. Vifaa hivyo ni Rig, mabomba ya chuma, mabomba ya kuweka ndani ya kisima, bits za kuchimbia, hammer, bentonite (matope ya kuchimbia), diesel na mafuta mengine kama hydraulic oil nk.
Unapochimba sehemu yenye mchanga wenye maji ni dhahiri kuwa mchanga utakuwa unabomokea ndani ya kisima. Ili kuzuia mchanga usibomokee ndani ya shimo la kisima, matope (drilling mud inayotengenezwa kwa mchanganyiko wa maji na bentonite) hutumika kusiliba kingo za shimo la kisima. Baada ya kukamilika uchimbaji na maeneo yenye maji kuainishwa mabomba (casings na screens) huwekwa na kazi ya kusafisha tope lililosiliba kingo za kisima huanza. Tope likiisha na maji kuwa masafi na upimaji wa wingi wa maji (pumping test) kufanyika ndipo tunasema kisima kimekamilika na miundombinu ya ku-pump maji inaweza kujengwa.Matope ya kuchimbia? Mzee hii ndio kitu gani pamoja na yote uliposema still gharama za kuchimba ziko juu sana
Wanatoboa mwamba.Halafu wakikutana na mwamba wanasepa wanakuachia shimo!
Hadi mita 80 kinachimbwa tuAmesema kisima chake kimechimbwa kwa jembe! Je unaweza kuchimba mita 35 kwa jembe?
Mpaka Mia Moja
Kilaza kama wewe ni hasara kwa Taifa!
Kuna baadhi ya maeneo hapa Dar kama ukanda wa Kimara, Mbezi, Kibamba, Ubungo usipoteze hela yako kuchimba kisima
Water table ya hayo maeneo maji yake yana magadi maana ile sio chumvi imagine hata wanyama wanayasusa
Pole sana mkuuNatamani hii comment ungeandika 2014.
Maana mwaka 2015 nilichimba kisima ubungo. Nilipata maji yana magadi balaa
Fanya Mpango nipate mawasiliano Yao bossWanatoboa mwamba.
Mwaka huu wametuchimbia home wakafika kwenye mwamba kukawa na moshi unafuka (mvuke mwingi kama moshi) wakaomba tuwatafutie mashine ya kupumulia,wakaunganisha na umeme wakashuka nayo mpaka chini wakamalizia kutoboa mwamba. Maji yakapatikana kwa wingi sana.
Gharama zao ndogo mno!!!
Sent from my SM-G970U using JamiiForums mobile app
Kumbe mwalimu wangu alikuwa boya, alinifundisha eti mita 1,000 sawa na kilomita moja! Huku nakuta watu wanachimba kisima mita 50,000! Yaani kilomita 5 kwenda chini ya ardhi! JF imenifumbua macho na masikio.Katika vitu ambavyo Kila nikifikiria nakosa majibu ni gharama ya kuchimba kisima na Ile mitambo yao kiujumla, Sote tunajua kuwa katika mitambo inayouzwa bei ghali ni mitambo ya kutengeneza Barabara na ya migodini, ikiwemo Wheel loader, Excavator, Bull dozer (mashine ya kipekee ambayo ukiwa Dar unaweza kuiwasha kuweka mafuta na kuweka gia na kuielekezea Mwanza Kisha ukapanda ndege na baada ya muda litafika tu Mwanza lenyewe maana Kila mahali linapita). Sasa hii mitambo gharama ya kukodisha Kwa siku ni kati ya laki 8 Hadi milioni.
Sasa twende huku kwenye visima vya maji, wao wanakuambia Kwa MITA 50,000 Hadi 85,000 hivyo mpaka kisima unamaliza ni milioni 10+.
Sasa je ni Nini hasa kinachokuwa gharama kwao mpaka kupelekea gharama ishoot milioni 10 Kwa kisima, maana haiingii akilini, Nilielewa hii nitakaa kimya.