Nini hasa kinafanya gharama za kuchimba kisima kuwa mil 8, 10, 12? What is so special?

Msaada mkuu wa contact huku tuna shida ya maji zaidi ya jangwani mkuu
 
Hao Nao wamekua kama wenye nyumba za kupangisha hawafanyi.kazi Bila Dalali inchi hii wananchi wanapigwa sana
 
Na
Omba namba zao boss
 
Mzee sinutoe
Mzee Si utoke Namba uwasaidie wadau
 
Matope ya kuchimbia? Mzee hii ndio kitu gani pamoja na yote uliposema still gharama za kuchimba ziko juu sana
 
Matope ya kuchimbia? Mzee hii ndio kitu gani pamoja na yote uliposema still gharama za kuchimba ziko juu sana
Unapochimba sehemu yenye mchanga wenye maji ni dhahiri kuwa mchanga utakuwa unabomokea ndani ya kisima. Ili kuzuia mchanga usibomokee ndani ya shimo la kisima, matope (drilling mud inayotengenezwa kwa mchanganyiko wa maji na bentonite) hutumika kusiliba kingo za shimo la kisima. Baada ya kukamilika uchimbaji na maeneo yenye maji kuainishwa mabomba (casings na screens) huwekwa na kazi ya kusafisha tope lililosiliba kingo za kisima huanza. Tope likiisha na maji kuwa masafi na upimaji wa wingi wa maji (pumping test) kufanyika ndipo tunasema kisima kimekamilika na miundombinu ya ku-pump maji inaweza kujengwa.

Hivyo gharama hutokana na uchimbaji, tope la kuchimbia, mabomba (casings na screens), usilibaji na usafishaji wa tope na upimaji wa wingi wa maji (pumping test).
 
Halafu wakikutana na mwamba wanasepa wanakuachia shimo!
Wanatoboa mwamba.
Mwaka huu wametuchimbia home wakafika kwenye mwamba kukawa na moshi unafuka (mvuke mwingi kama moshi) wakaomba tuwatafutie mashine ya kupumulia,wakaunganisha na umeme wakashuka nayo mpaka chini wakamalizia kutoboa mwamba. Maji yakapatikana kwa wingi sana.
Gharama zao ndogo mno!!!

Sent from my SM-G970U using JamiiForums mobile app
 
Kuna baadhi ya maeneo hapa Dar kama ukanda wa Kimara, Mbezi, Kibamba, Ubungo usipoteze hela yako kuchimba kisima

Water table ya hayo maeneo maji yake yana magadi maana ile sio chumvi imagine hata wanyama wanayasusa

Natamani hii comment ungeandika 2014.

Maana mwaka 2015 nilichimba kisima ubungo. Nilipata maji yana magadi balaa
 
Kwa wakazi wa Bagamoyo na maeneo jirani tupeni uzoefu wa kuchimba visima maeneo hayo..
 
Tatizo udalali. Zamani 14+year nilichimba 3m mita 80 kila kitu kwao, mpka Leo pump inapiga kazi. Strange zamani annual service ilikuwa 200,000, latest 150,000 tu. Lakini najua bado kuna udalali tu.
 
Fanya Mpango nipate mawasiliano Yao boss
 
Kwangu mimi udalali ndio umeharibu Kwa asilimia kubwa bei za vitu na huduma,middle man ni wengi sana na hawa ndio kichefuchefu cha bei.Hata hivyo visima wamesababisha wao kupandisha bei,na Si vifaa
 
Kumbe mwalimu wangu alikuwa boya, alinifundisha eti mita 1,000 sawa na kilomita moja! Huku nakuta watu wanachimba kisima mita 50,000! Yaani kilomita 5 kwenda chini ya ardhi! JF imenifumbua macho na masikio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…