Nini hasa kinafanya mtu anabadilika sura au mwili kwa haraka?

Mtambachuo

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
1,907
Reaction score
3,560
Wanabodi imekuwa ni jambo ambalo ni kawaida pale unapokutana na mtu ambae hamjaonana
kwa kipindi cha miaka 5 hadi 10, lakini mnapokutana baadhi wanakuwa wamebadikia sana muonekano
wa sura na mwili kwa ujumla.

Wengine wanakuwa na mvi nyingi, kipara, sura imeanza kuchoka mwili mkubwa ila mwingine anakuwa hana hivyo au vipo kidogo sana na ni watu wa rika moja labda mlisoma pamoja.

Je, ni mimi huwa najiuliza maswali hayo au na wewe pia? Sababu inaweza kuwa ni nini wanabodi ni hali kijeneti, kujipata kimaisha, au ni ugumu kwenye harakati za kujitafuta au ni nini hasa?
 
Unafkiri maisha halisi ni kama movie sio? Kwamba hata ikipita miaka zaidi ya mitano watu wanabaki vile vile.
Jiongeze.
 
1. Mchango wa ubora wa vinasaba vya kijenetiki

2. Hali ya maisha kiuchumi, maradhi, nk

3. Hali ya hewa na mazingira kiujumla

4. Lishe & matumizi ya vitu vyenye madhara (pombe, sigara, madawa ya kulevya, kamari, zinaa, nk)

5. Optimism. Watu wenye hofu na mashaka juu ya kesho au mambo yaliyowatokea zamani, hudhoofika upesi.

Watu wanaoishi kwa kumtegemea Mungu huwa na afya ya mwili, akili na roho, na huishi muda mrefu zaidi.
 
Hali wanazopitia ndizo hasa Huwa chanzo Cha kuchoka mapema. lifestyle ya watu walio Wengi ni mbovu sana. mtu Hali chakula Kwa wakati,anafanya ngono sana,pombe ndio usiseme,halali akapumzika Kwa wakati,maji hanywi,mtu kama huyo kuchoka ni haraka sana
 
1. Mchango wa ubora wa vinasaba vya kijenetiki

2. Hali ya maisha kiuchumi, maradhi, nk

3. Hali ya hewa na mazingira kiujumla

4. Lishe & matumizi ya vitu vyenye madhara (pombe, sigara, madawa ya kulevya, kamari, zinaa, nk)

5. Optimism. Watu wenye hofu na mashaka juu ya kesho au mambo yaliyowatokea zamani, hudhoofika upesi.

Watu wanaoishi kwa kutegemea Mungu huwa na afya ya mwili, akili na roho, na huishi muda mrefu zaidi.
Hapo kwenye aya ya mwisho umetupiga na kitu kizito 🤣🤣
 
Wanabodi imekuwa ni jambo ambalo ni kawaida pale unapokutana na mtu ambae hamjaonana
kwa kipindi cha miaka 5 hadi 10, lakini mnapokutana baadhi wanakuwa wamebadikia sana muonekano
wa sura na mwili kwa ujumla.

Wengine wanakuwa na mvi nyingi, kipara, sura imeanza kuchoka mwili mkubwa ila mwingine anakuwa hana hivyo au vipo kidogo sana na ni watu wa rika moja labda mlisoma pamoja.

Je, ni mimi huwa najiuliza maswali hayo au na wewe pia? Sababu inaweza kuwa ni nini wanabodi ni hali kijeneti, kujipata kimaisha, au ni ugumu kwenye harakati za kujitafuta au ni nini hasa?
Kwanza ni kujichubua, stress za maisha, madowa ya kulevya, kupigwa sana miti (kama modemu wa bongo movie na fleva).
 
Aisee hivi kwahali hii ccm itapinduliwa kweli!
Kama vijana wenywe ndio hawa!
Chakuskitisha zaidi huyu ukute nikijana alie maliza chuo kabisaa
🤔🤔🤔🤔🤔
Tena ni Degree holder kabisa anashangaa kwanini binadamu anazeeka ila hashangai maembe kukomaa kijijini kwao😂😂

Labda kuongezea tu sio Hadi mpoteane miaka 5 kaeni ndani nyumba 1 baada ya hiyo miaka 5 utapata majibu anabadirika au yupo hivyohvyo siku zote.

Tuna taifa lenye wasomi wengi wasio na maarifa
 
Mkuu hatutawaza siasa muda wote kama wewe hiyo ni kazi yako unafanya muda wote sio kwa kila mtu
 
Unafkiri maisha halisi ni kama movie sio? Kwamba hata ikipita miaka zaidi ya mitano watu wanabaki vile vile.
Jiongeze.
Maisha ni halisi ndio ila mbona watu wa rika moja wanazeka tofauti ?
 
1. Mchango wa ubora wa vinasaba vya kijenetiki

2. Hali ya maisha kiuchumi, maradhi, nk

3. Hali ya hewa na mazingira kiujumla

4. Lishe & matumizi ya vitu vyenye madhara (pombe, sigara, madawa ya kulevya, kamari, zinaa, nk)

5. Optimism. Watu wenye hofu na mashaka juu ya kesho au mambo yaliyowatokea zamani, hudhoofika upesi.

Watu wanaoishi kwa kumtegemea Mungu huwa na afya ya mwili, akili na roho, na huishi muda mrefu zaidi.
Safi umeleza vizuri sana sio hao wababaishaji wasio na hoja
 
Tena ni Degree holder kabisa anashangaa kwanini binadamu anazeeka ila hashangai maembe kukomaa kijijini kwao😂😂

Labda kuongezea tu sio Hadi mpoteane miaka 5 kaeni ndani nyumba 1 baada ya hiyo miaka 5 utapata majibu anabadirika au yupo hivyohvyo siku zote.

Tuna taifa lenye wasomi wengi wasio na maarifa
Kuzeeka ni sawa ni normal body physiology ila jiulize kwa nini watu wa umri mmoja speed yao ya kuzeeka ina tofautiana. Wewe na degree yako ya Sosholojia usitake kila mtu awe kama wewe wengine ni degree holder kwenye mambo mengine. Think Critically.
 
Kuna mambo ya kujadiliwa na mtu aliyebobea kwenye fani husika tu na yapo mambo ambayo hujadilika vilivyo bila kutegemea kiwango kikubwa cha elimu.

Hili suala linaweza kufafanuliwa vizuri na mtu mwenye kiwango cha elimu ya darasa la 6 au hata chini yake.

Inaonekana umekaririshwa sana kukariri mambo. Jipatie uhuru wa akili ili ufurahie mawanda mapana ya maarifa bora na amilini (noble and practical knowledge)
 
Back
Top Bottom