#COVID19 Nini hasa lilikuwa kosa la Hayati Magufuli kwenye ishu ya COVID-19 ?

#COVID19 Nini hasa lilikuwa kosa la Hayati Magufuli kwenye ishu ya COVID-19 ?

Ni kinga inayopatikana kwa kundi kubwa la watu kutokana na watu wachache kupata chanjo hivyo kuzuia ueneaji wa ugonjwa( transmission). Protection of unvaccinated from vaccinated.
Baada ya kupata kinga sio chanjo
 
Habari JF,

JPM aliamini corona itaendelea kuwepo na tutaishi nayo kama yalivyo magonjwa mengine, kiuhalisia ndivyo ilivyo corona ipo na idadi ya watu waliopata chanjo ni ndogo sana na watu walishapata kinga asilia sasa hivi sio tishio tena. Lakini bado watu wakiwemo madaktari wanalaumu approach yake kwenye ishu.

Swali langu ni lipi lilikuwa kosa lake?

Je, ni kutoweka lock down?

Je, ni kupinga chanjo?

Je, ni kupinga njia za kitaalamu kama kuvaa barakoa na njia hizi zilisaidia kwa kiasi gani sehemu nyingine ?

Kwangu Mimi mnyonge mnyongeni katika hili alistahili tuzo.
Swali lako ni rahisi sana kama unao msingi wowote wa sayansi.

Magufuli alidai au alidaiwa kuwa mwanasayannsi ambaye hakujua chochote kuhusu sayansi.

Magufuli hakuwa na ufahamu wowote, wala ushahidi wowote juu ya ugonjwa huo mpya, ambao habari zake zilikuwa hazifahamiki kabisa.

Magufuli hakuwa na ushahidi wowote kuhusu hatari au kutokuwepo kwa hatari kutokana na athari ambazo zingetokana na ugonjwa huo. Hakujua kitu chochote juu yake.

Kwa hiyo maamuzi yote aliyofanya yalikuwa ni maamuzi hatarishi kabisa kwa taifa.

Hatua zilizochukuliwa na nchi nyingine karibu zote duniani, ni hatua zinazofahamika kisayansi na zinatumika mara zote kufubasha uenezi wa magonjwa hatari ya milipuko. Njia hizi hazikuwa mpya, ni njia za kawaida.

Leo hii unapokuja na kujigamba juu ya ushujaa/ihodari wa Magufuli ni kukosa uelewa. Sisi tulicheza kamali, na bahati yetu ikawa kwamba Corona, pamoja na kutofahamika kwake katika mambo mengi, haikuwa na uhatari uliotegemewa kutokea; hiyo ndiyo ikawa bahati yetu, na kuanza majigambo mengi kama haya unayoyaleta hapa kwenye mada yako.

Lakini, kama ingetokea Corona ikawa ni hatarishi zaidi, Tanzania tungelia kutokana na maamuzi ya kijinga tu yaliyofanywa na kiongozi wa nchi bila ya kutumia akili, wala kusikiliza maoni ya wataalam waliosomea fani katika eneo hilo.

Hadi leo hii kuna mambo mengi yasiyofahamika kuhusu Corona, kwa mfano, kwa nini mahali pengine ilikuwa hatari zaidi kuliko sehemu zingine. Hii ndiyo kazi inayofanyika katika sayansi kujaribu kupata majibu kama hayo.

Sasa nimalizie kwa kukupa tahadhari hii katika kusifu kwako mambo usiyoyajuwa.
Hivi Magufuli leo hii yupo wapi? Pasingekuwepo na Corona, inawezekana Magufuli hadi leo hii angekuwa anadunda! Na wengi wengine tuwajuao ambao maisha yao yalikatishwa kabla ya wakati wao, kwa sababu tu ya ujio wa corona, na kudharauliwa na Magufuli huyo huyo.
Sijui kama utanielewa nilichokueleza hapa.
 
Nikuulize Swali Unajua Russian Roullette...

Unachukua pistol unaweka risasi moja unazungusha ile cyclinder chamber alafu mnapeana zamu kila mtu kujipiga risasi kichwani...,

Hata ukibahatisha usipokufa lakini gamble kama hio ni hatari ukiendelea namna hiyo uwezekano mkubwa kuna siku utateleza....

Maana yangu ni kwamba kuna mambo hayawezekaniki (total lockdown especially kwa nchi kama Tanzania) LAKINI tahadhari haimaanishi Total Lockdown pekee bali kuwa serious na kuacha mzaha......; In Hindsight kilichofanyika huenda kilikuwa better option, ila sababu hatukujua reaction itakuwa vipi kwahio haikuwa busara ku-gamble na jambo hatari ingawa baada ya kupata more facts ndio inabidi tu-act accordingly ila kabla ya facts kwa mambo ya afya ni vema kuwasikiliza wataalamu na hapa kwenye hili wataalamu ni watu wa afya na sio wanasiasa
Sasa sijui kama huyo mtu RNA atakusoma na kukuelewa hapa kwa mfano mzuri kabisa uliomtolea hapa.

Kwa jina anajitambulisha kama RNA, matumaini yangu ni kwamba anayo maana ya Ribonucleic Acid (RNA), na kama hivyo ndivyo, pengine anao msingi kiasi wa kujuwa hatari iliyokuwa ikilikabili taifa, kwa maamuzi ya mtu mmoja tu, ambaye alifanya maamuzi juu ya jambo ambalo hakuwa na taarifa zozote juu yake.

Wengine wote, karibu dunia nzima wakawa wamekosea, ila yeye ndiye akawa na ufahamu!
 
Unajua herd immunity ni mini ?
Magufuli aliijua hii 'herd immunity' alipochukua uamzi? Aliijuwa kutoka wapi?
Na ilikuwaje wengine wote wasiifahamu, ila yeye tu ndiye akawa mjuaji?
 
Kwa kuzuia kuvaa barakoa tuu yeye Kijazi na watu wengi tuu wamekufa kwa ujuaji wake usio na mantiki

Chanjo imeleta herd immunity kwa nchi zote duniani na kupunguza rate of infection

Muulize Dr Mpango alirudia wapi kwenye ambukizo

Mkuu kachemshe viazi ule ukishiba kalale.

Siku ukija kuelewa haya mambo utajiona kulundu sana.
 
Idadi ya waliopata chanjo halisi sidhani kama inafika 200k kwa nchi nzima watu tunavyeti na hatukuruhusu hayo matakataka kuingia miilini. JPM hakuwa na kosa na hatakuwa na kosa kwa namna alivyoiongoza nchi wakati dunia haijui cha kufanya... most of critics are haters hawaoni jema lolote la JPM kwa hiyo hutaweza kuwaelewa.
 
1. Vyeti feki
2. Ubadhirifu
3. Urasimu
4. Safari
5. Uadilifu kazini
6. Usharika na msoga
7. Poda na yafananayo
8. Uchawa
9. Kuishi kimalaika isivyo halali bila kuvuja jasho
10. Wakina Fatuma,Maria, Ridhi na the like

Wapi hapo ulidondokea mkuu?
Hayo yako wewe, ila Watanzania tunajua Mungu katuondolea ile laana basi
 
Habari JF,

JPM aliamini corona itaendelea kuwepo na tutaishi nayo kama yalivyo magonjwa mengine, kiuhalisia ndivyo ilivyo corona ipo na idadi ya watu waliopata chanjo ni ndogo sana na watu walishapata kinga asilia sasa hivi sio tishio tena. Lakini bado watu wakiwemo madaktari wanalaumu approach yake kwenye ishu.

Swali langu ni lipi lilikuwa kosa lake?

Je, ni kutoweka lock down?

Je, ni kupinga chanjo?

Je, ni kupinga njia za kitaalamu kama kuvaa barakoa na njia hizi zilisaidia kwa kiasi gani sehemu nyingine ?

Kwangu Mimi mnyonge mnyongeni katika hili alistahili tuzo.
Hivi ule uchawi aliomtuma prof wa jalalani akachukue Madagascar uliponesha wangapi?
 
Kudanganya wtz kuwa covid ipo hata kwenye mapapai dah...
Yule Mzee alikuwa 'fix' sana. Alidanganya kwamba watu wake walipima sampuli za mbuzi, papai na oil chafu zikakutwa na virusi vya corona. Alikuwa anajaribu ku-justify uamuzi wake wa kupuuza protocols za WHO.
 
Back
Top Bottom