Habari JF,
JPM aliamini corona itaendelea kuwepo na tutaishi nayo kama yalivyo magonjwa mengine, kiuhalisia ndivyo ilivyo corona ipo na idadi ya watu waliopata chanjo ni ndogo sana na watu walishapata kinga asilia sasa hivi sio tishio tena. Lakini bado watu wakiwemo madaktari wanalaumu approach yake kwenye ishu.
Swali langu ni lipi lilikuwa kosa lake?
Je, ni kutoweka lock down?
Je, ni kupinga chanjo?
Je, ni kupinga njia za kitaalamu kama kuvaa barakoa na njia hizi zilisaidia kwa kiasi gani sehemu nyingine ?
Kwangu Mimi mnyonge mnyongeni katika hili alistahili tuzo.
Swali lako ni rahisi sana kama unao msingi wowote wa sayansi.
Magufuli alidai au alidaiwa kuwa mwanasayannsi ambaye hakujua chochote kuhusu sayansi.
Magufuli hakuwa na ufahamu wowote, wala ushahidi wowote juu ya ugonjwa huo mpya, ambao habari zake zilikuwa hazifahamiki kabisa.
Magufuli hakuwa na ushahidi wowote kuhusu hatari au kutokuwepo kwa hatari kutokana na athari ambazo zingetokana na ugonjwa huo. Hakujua kitu chochote juu yake.
Kwa hiyo maamuzi yote aliyofanya yalikuwa ni maamuzi hatarishi kabisa kwa taifa.
Hatua zilizochukuliwa na nchi nyingine karibu zote duniani, ni hatua zinazofahamika kisayansi na zinatumika mara zote kufubasha uenezi wa magonjwa hatari ya milipuko. Njia hizi hazikuwa mpya, ni njia za kawaida.
Leo hii unapokuja na kujigamba juu ya ushujaa/ihodari wa Magufuli ni kukosa uelewa. Sisi tulicheza kamali, na bahati yetu ikawa kwamba Corona, pamoja na kutofahamika kwake katika mambo mengi, haikuwa na uhatari uliotegemewa kutokea; hiyo ndiyo ikawa bahati yetu, na kuanza majigambo mengi kama haya unayoyaleta hapa kwenye mada yako.
Lakini, kama ingetokea Corona ikawa ni hatarishi zaidi, Tanzania tungelia kutokana na maamuzi ya kijinga tu yaliyofanywa na kiongozi wa nchi bila ya kutumia akili, wala kusikiliza maoni ya wataalam waliosomea fani katika eneo hilo.
Hadi leo hii kuna mambo mengi yasiyofahamika kuhusu Corona, kwa mfano, kwa nini mahali pengine ilikuwa hatari zaidi kuliko sehemu zingine. Hii ndiyo kazi inayofanyika katika sayansi kujaribu kupata majibu kama hayo.
Sasa nimalizie kwa kukupa tahadhari hii katika kusifu kwako mambo usiyoyajuwa.
Hivi Magufuli leo hii yupo wapi? Pasingekuwepo na Corona, inawezekana Magufuli hadi leo hii angekuwa anadunda! Na wengi wengine tuwajuao ambao maisha yao yalikatishwa kabla ya wakati wao, kwa sababu tu ya ujio wa corona, na kudharauliwa na Magufuli huyo huyo.
Sijui kama utanielewa nilichokueleza hapa.