Cathode Rays,
Cathode Rays,
asante sana kwa ufafanuzi huu wa utu wa mtu ni human dignity ambamo humanity imo ndani yake.
Watetezi wa utu wa mtu ndio waliopelekea adhabu zote ambazo ni degrading kwa utu wa mtu zifutwe ikiwemo kuchapwa viboko up to death by hanging na all kinds of torture including water bording.
Tanzania bado tunatekeleza adhabu ya kifo kwa kunyongwa mpaka ufe which is really barbaric!.
Nikirudi kwenye mada ya EMT, binadamu akiwa kwenye hali ya ugonjwa, anahitaji humility na symphathy na sio kumsimanga. Mtu akiwa mgonjwa regardless anaumwa nini, sio vyema kuijadili nafasi yake kisiasa kwa vile haukuna stipulation ya sheria wala kanuni kuwa mbunge akiumwa kwa muda gani, atasita kuwa mbunge.
Mtoa mada ya afya ya mbunge yule, hakuileta in good faith, ila kwa vile jimbo hilo linashikiliwa na CCM na eneo hilo limeshapata joto la moto wa Godbless Lema, then mtoa mada ana wish the worst itokee ili Chadema walitwae jimbo.
Mimi ni miongoni mwa wanashutumu dhamira hiyo na kusema huo sio utu wa kiafrika.
Tanzania tunafuata mkondo wa sheria za Common Law, za Uingereza ambapo mtuhumiwa yuko presumed innocent until proven guilt beyond reasonable doubt in a court of law of competent jurisdiction.
Kinachofanyika nchini ni completely vice versa, kwa mujibu wa sheria zetu, hairuhusiwi kuwapiga picha wahalifu wakiwa chini ya ulinzi wa polisi wala hairuhusiwi kuwapiga picha washitakiwa wakiwa mahakamani kwani ni kuwavunjia utu wao. Kila siku tunaonyeshwa watuhumiwa wakiwa paraded vituo vya polisi na picha kibao za mahakamani ambazo zinakiuka utu wa mtu.
Niliangalia lile tukio la September 11 jinsi Western media zilitunza dignity ya miili ya watu wao, hakuna picha zilizoonyesha miili zaidi ya black bags. Ni media hizo hizo zilizoonyesha dilapidated bodies za waafrika wakati wa Rwandan Genocide, au picha za Saadam, Osama na juzi Ghadafi kwa vile kwa standard zao dignity ni kwa wazungu tuu, wengine hawastahili.
Media zetu nazo zinafuata huo huo mkumbo wa degrading human dignity kwa kuonyesha picha za miili ya marehemu mpaka nyuso zao!. Picha nyingine ni just 'morbid curiosity' tuu na hazijuwa na sababu yoyote ya msingi.
Utu wa mtu, hauna uhusiano na kitu, mtu muone kama mtu sio mpaka awe na kitu!.
Humu jf siku hizi kumevami na vichwa maji wa ajabu ambao hawana lugha za staha na kutoa matukano yanayuvunja heshima na utu wa watu bila sababu zozote za msingi. Mathalani kumtukana mtu kwa sababu ya umbile lake au sura yake ni kumvunjia heshima ya utu wake na hivyo kuishusha hadhi ya jf mbele ya jamii ya wapenda haki.