Nini hatima ya watanzania, Inatosha sasa! Yaliyosemwa na Dkt. Slaa na Polepole yanaumiza

Nini hatima ya watanzania, Inatosha sasa! Yaliyosemwa na Dkt. Slaa na Polepole yanaumiza

Kwa haya yanayoendelea nchini vyombo vyote vya ulinzi na usalama wanatakiwa wajitafakari sana. Haiwezekani taifa lifanyiwe mambo ya kipumbavu namna hii halafu tuamini mzalendo wa kweli nchi hii ni Polepole pekee
Sasa kama IJP anafanya miamala ya billions of money hapo hujaongelea sdf atakuwa na mabilion mangapi. Sasa wote mafisadi hawana lakuongea ukiwa fisadi, mwizi dhulumati., hutaweza kemea dhambi.
 
Ameandika Rais wangu wa TLS
BADALA YA KUTUNIA NGUVU KUBWA KUBAMBIKANA MA KESI YA UHAINI NGUVU HII TUNGETUMIA KULINDA RASLIMALI ZA TAIFA.

Ulinzi na usimamizi endelevu wa rasilimali za asili za Tanganyika ni suala la kufa na kupona.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria zilizopitishwa na Bunge zinatambua mamlaka ya kudumu ya wananchi juu ya utajiri na rasilimali za asili. Hivyo basi, ni wajibu wa kila chombo cha dola na kila Mtanzania kuhakikisha kuwa rasilimali hizi haziuzwi, hazinyonywi, wala hazisimamiwi kwa njia inayodhuru taifa.

SHERIA NA ULINZI WA RASLIMALI ASILI.

Sheria mbili za mwaka 2017 ndizo ngao kuu za kulinda rasilimali za asili:

1. Sheria ya Umiliki wa Kudumu wa Rasilimali za Taifa, 2017 (Sheria Na. 5 ya 2017):

Inatamka kwamba rasilimali zote za taifa ni mali ya kudumu ya wananchi wa Tanzania na zinashikiliwa na Serikali kwa niaba yao.

sheria inataka mikataba yoyote inayohusu rasilimali za taifa kuhakikisha faida kubwa inabaki kwa Watanzania.

Inatoa masharti kwamba migogoro yote kuhusu rasilimali za asili lazima isikilizwe ndani ya Mahakama za Tanzania na siyo mbele ya mabaraza ya usuluhishi ya nje.

2. Sheria ya Mapitio na Majadiliano Upya ya Masharti Kandamizi, 2017 (Sheria Na. 6 ya 2017):

Inalipa Bunge mamlaka ya kupitia na kujadili upya mikataba yenye masharti kandamizi, ya kinyonyaji au yenye kwenda kinyume na maslahi ya taifa. Je tunalo Bunge la namna hii?

Sheria inataka kuwepo kwa uwazi na uwajibikaji katika mazungumzo, usimamizi na utekelezaji wa mikataba inayohusu rasilimali za asili.Hivi hili la Makaa ya Mawe liliwahi kujadiliwa au kutangazwa wapi na nani aliyezuia Serikali Kununua Hisa husika?

Kusimamia kwa uthabiti utekelezaji wa Sheria Na. 5 na Na. 6 ya mwaka 2017 kama kinga ya mwisho ya kisheria dhidi ya unyonyaji na uporaji wa rasilimali ndiyo kingekuwa kipaumbele chetu

Utajiri wa asili ndiyo uti wa mgongo wa uhuru wa Tanganyika kuulinda si hiari bali ni jukumu la kikatiba, kisheria na kizalendo.
BAK MWABUKUSI.
 
Hivi wakati huu wa UCHAGUZI mkuu, SERIKALI si imeshavunjwa na wagombea si wapo kwenye mchakato wa kuomba ridhaa ya kuchaguliwa. Je, amiri jeshi Kwa sasa ni nani?
Kutokana na unyeti wa nafasi ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu, kwa dunia nzima, anayeshikilia nafasi hiyo HAACHII nafasi hiyo hadi mtu mwingine atakapoapishwa kuishika nafasi hiyo. Ila sikuzuii kunipa mfano wa nchi ambayo Rais aliyekuwa madarakani aliacha mamlaka kisa anagombea mara ya pili.
 
Bado nina imani na CDF wangu kwa mahaba makubwa juu yake na jeshi lake. Mwenyezi Mungu awatangulie katika majukumu yao mema.
CDF na yeye ni wale wale tu, nchi watu wanauziana migodi rasimali za Taifa kwa pesa ya madafu, yupo kimya , gwanda zake zinasaidia nini Taifa?
 
Kwa yanayoendelea huko kwenye mitandao ya kijamii CDF nakuita kwa mara nyingine take over now.
 
Fanya kazi
Jali familia yako na maisha yako
Watanzania waache kama walivyo wamesharidhika na yanayofanywa sio wa kuwatetea..wewe endelea kila nchi kula ugali na wali na nyama na kila ulitakalo
Wajinga wwanapeana ushauri wa kufikiria ugali kuliko kesho ya vizazi vyao! Upumbavu mkubwa sana! Au mnadhani wataacha tukikaaa kimya?
 
Wajinga wwanapeana ushauri wa kufikiria ugali kuliko kesho ya vizazi vyao! Upumbavu mkubwa sana! Au mnadhani wataacha tukikaaa kimya?
Ndo watafutie maisha kizazi chako achana na vizazi vyao.kama NI ardhi watafutie majumba wajengee na uwaoe elimu Bora..in short tafuta hela brother
 
Inasikitisha sana!! Huyu mama kauza Kila kitu!! Halafu watu wanamchekea TU!! Watanganyika tumelogwa na nani!? Tuache tabia za Kisukuma bhana!! Msukuma utamuona na pingu mkononi, ukimuliza, "Maduhu Nini shida mbona umefungwa pingu? Yeye anajibu Ndohoo tabu! Huku ana pingu !?" Tuache ujimga nchi ni yetu sote. Haiwezekani wao wanufaike na familia zao, sisi tuwe wasindikizaji!! Naomba kama Kuna mtu yoyote wenye kujua naweza pata silaha , anielekeze! Niko Benako hapa.
mwenye hasira haombi silaha si unaona Kenya? chukua mawe anza kazi.kila la kheri
 
Ndugu zangu Watanzania ama watanganyika,naona vibaya hata kuandika hii barua kutokana na mambo yanavyoendelea kutoka kwa wadau mbali mbali na pia naweza kuwaita wazalendo waliojitolea kututoa matongotongo machoni,na kutuzibua masikio.

Sasa naweza kusema inatosha kwa sasa viongozi hawana nia nzuri na hii nchi na hawana ni huruma na watanzania wapo kwa maslahi ya familia zao.

Laiti kama jeshi letu linajitambia na lipo kwa maslahi ya taifa letu basi leo tulipaswa kuona wale wote waliotajwa kwenye kashfa na mh. Polepole wakichukuliwa hatua kabla ya kuchakachua taarifa.

Taarifa muhimu kama kuchezewa mifumo ya uchaguzi ni zaidi ya uahini na watu kama mh jk kuwa sehemu ya serikali ni mbaya sana,kutokana na yanyoendele katika taifa letu.

Pia nimemsikiliza Mh. Dr. Slaa kiukweli inaumiza nikiwa raia wa hii nchi.
Naliamuru jeshi lijitafakari na wananchi tunapaswa kutafakari pia si kila kitu kusubiri ngoja tuone itakuwaje,hawa watu wamejipanga aswa na wameamua kushika utawala ili kuendelea kuficha wizi wao.

Pia nasikia yule bwana anaitwa asasi mwenye dipromatic passport ni mkwe na mh jk. Ambaye ni alitambulishwa na Rais wetu ye ndiyo Boss wake tofauti na sisi kwa mujibu wa katiba.View attachment 3452130View attachment 3452132
Huu mchoro urekebishwe Kuna macable mengine kutoka ccm yanaenda TRA kupora kodi za watanzania usiku na mchana na mengine yanaenda IMF na World bank kukopa matilioni we unafikiri deni la taifa limefikaje tilioni 116 huku wamenunua mabasi utitiri yaani lukuki huku watoto wao wakiendesha magari ya kifahari ya milioni 500 na wake zao bado mahawara.
 
kwani 2020 kulikuwa na uchaguzi kweli? walikuwa wapi hao kina polepole. kinachofanya polepole apuuzwe ni historia yake.
Walau ametambua makosa yake na kisha ameomba radhi kwa watanzania. Kwa hiyo hatupaswi kumpuuza kama wewe
 
mwenye hasira haombi silaha si unaona Kenya? chukua mawe anza kazi.kila la kheri
Kutokana na uchungu na uzalendo tulitamani kuona wakijichukulia sheria baada ya kuona wamekosea
 
Hii post inatakiwa KUFUTWA haraka sana kwani Jeshi letu lenye nidhamu na weledi wa hali ya juu linapokea Amri na maelekezo kutoka kwa mtu mmoja tu ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu na si vinginevyo!!
Naye ni ROSTAM AZIZI huyu akitoa amri kesho wewe ufe utakufa huku ukiimba ccm oyee, ccm oyee. Zidumu fikra za tostam kuhusu makaa yetu ya mawe huko mchuchuma
 
Hakuna wakutusaidia watanzania bali sisi wenywe sasa tuchague moja!Mama huyu akipita huu mwaka tumeisha huyu mama sio mtu wa kawaida!
 
Back
Top Bottom