Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Kipindi kinataka muendeshaji ajue kwamba unapokuwa unaandaa kipindi cha kuangaliwa na watu tofauti, angalau kiwe kinaendeshwa kwa akili, japo kidogo tu.Kwani kipindi kinataka nini mpaka useme ivyo
Fine, I get it. I may be too highbrow. Sio kila kipindi ni lazima kiwe sawa na "Hard Talk", "60 Minutes" au "Jenerali on Monday".
I get that.
Lakini Salama anaweza kuongelea habari za machotara wanavyotakiwa ku date na machotara tu, weusi hawawafai.
Kwenye hicho kipindi. Jambo la kijinga kabisa la ubaguzi wa rangi. Halafu linachukuliwa poa tu.
Halafu hili si tatizo la Salama tu, naona hata yule aliyemuhoji shoga (Zamaradi nafikiri) ingawa kimsingi sina tatizo na kumuhoji shoga (perhaps on public airwaves in such a conservative country this is controversial) lakini naye alivyokuwa anahoji tu unaona ana m treat interviewee kama mtoto, kama anamfanyia favor, na kibongobongo interviewee anakubali tu, kashazoea kuwa mnyanyapaa.
Hizi kazi zinahitaji elimu, si kazi za kufanya kwa ujanja ujanja. Ukifanya kwa ujanja ujanja wakati huna elimu, kila wiki upo kwenye kipindi unauliza maswali, watu wanaona kwamba huyu hapa anafanya kwa ujanja ujanja hana elimu.
Mtu katoka kuangalia interview ya Oprah halafu aende kuangalia ya Salama au Zamaradi, kama anajua mambo anaona tofauti kibao tu.
Kibongobongo inawezekana watu wakapotezea, lakini ukishazoea standard Fulani ya maisha na intellectual content, halafu ukashushiwa kiwango, unaona kabisa.
Ndiyo maana nashangaa hao wanaowaponda kina Muba na John wakati hata Salama mwenyewe ni fungu hilo hilo.
Labda nikienda kwa Oprah, Hard Talk na 60 Minutes mtaona kama namuonea. Angalia vipindi vya Kenya tu hapo, au linganisha na interviews za Maria Sarungi utaona tofauti kubwa ya upeo.