Nini kifanyike ili kiongozi asipendelee kwao kama Hayati Dkt. Magufuli alivyoipendelea Chato?

Nini kifanyike ili kiongozi asipendelee kwao kama Hayati Dkt. Magufuli alivyoipendelea Chato?

Sema nini kifanyike kiongozi mzalendo kama Dkt Magufuli asije kuuawa? Maana furaha yenu ya kumuua Dkt Magufuli sasa hamfichi, mnajiachia kama vile watanzania ni vilaza hawajui, just wait 2025!
Wauaji wanajitokeza kwa sura ya kukosoa kwamba kilifanyika hiki ama kile kinyume na sheria..................Karma is revolving to trigger at the target bull!!!
 
Ni wazi kuwa rais Magufuli aliipendelea sana wilaya ya Chato katika kupeleka maendeleo. Alijenga uwanja wa ndege wa kimataifa, alijenga hospitali kubwa ya rufaa ya kanda, alijenga chuo cha Veta, alianza kujenga hoteli ya nyota tatu, mipango ya kujenga uwanja wa mpira. Na mambo mengine mengi sana.

Haya mambo hayakuanza na Rais Magufuli, ni vile tu yeye aliyafanya kwa kiwango cha kushangaza.

Sasa siku nyingine atatokea kiongozi atafanya zaidi ya Magufuli alivyofanya. Nini kifanyike ili kuzuia Rais au kiongozi yoyote asiweze kufanya kitu kama hicho?
Mnataka mtu akiwa rais mkoa wake au wilaya yake pasifanyike maendeleo yoyote? Chini ya magufuli pamefanyika maendeleo kila mahali. Mtwara kumejengwa kiwanja cha ndege na hospitali ya rufaa mbona sio kwao magufuli? Mbeya kumejengwa kiwanjwa cha ndege cha kimataifa mbona sio kwao magufuli? Mara kumejengwa hospitali ya rufaa. Ilianza miaka ya 70 magufuli kaimalizia. Mara kiwanja cha ndege kimepangwa kujengwa kuwekwa lami na magufuli. Mara sio kwao magufuli. Ni kila mahali kumejengwa na magufuli. Uwanja wa ndege chato ni wa mkoa wa geita na sera ni kila mkoa kiwepo kiwanja kizuri cha ndege. Tatizo kuna watu nchi hii wanataka maendeleo yabakie kwao tu sehemu zingine wabakie nyuma. Watu hawa wanajulikana ni nani na chama chao ni kipi.
 
Tuchague wazaramo ndio wawe marais, Dar imeshaendelea hivyo hawatakuwa na time nayo 😁😁😁
Maweee! ... kama unataka fweza yetu iishie kwenye flyover kila junction ya Dar basi endelea na wazaramo!
1f605.png
 
Mkuu miradi mingi ya Chato haikujadiliwa kabisa bungeni. Ni kama Rais mwenyewe aliamua kuitekeleza. Na si Magufuli tu. Huu utaratibu wa Marais kupendelea kwao upo siku nyingi, sema tu Magufuli aliupeleka next level, hadi uvumilivu wa watu ukavunjika.
magufuli Mwenyezi Mungu alimchukua muda muafaka, angeendlelea kutawala pengine tanzania sasa ingekuwa imegawanyika sana kikabila na kikanda
 
Wewe hupendi kwenu
Unamatatizo ya akili.
Laana ya magufuli itawatafuna sana
 
Mnataka mtu akiwa rais mkoa wake au wilaya yake pasifanyike maendeleo yoyote? Chini ya magufuli pamefanyika maendeleo kila mahali. Mtwara kumejengwa kiwanja cha ndege na hospitali ya rufaa mbona sio kwao magufuli? Mbeya kumejengwa kiwanjwa cha ndege cha kimataifa mbona sio kwao magufuli? Mara kumejengwa hospitali ya rufaa. Ilianza miaka ya 70 magufuli kaimalizia. Mara kiwanja cha ndege kimepangwa kujengwa kuwekwa lami na magufuli. Mara sio kwao magufuli. Ni kila mahali kumejengwa na magufuli. Uwanja wa ndege chato ni wa mkoa wa geita na sera ni kila mkoa kiwepo kiwanja kizuri cha ndege. Tatizo kuna watu nchi hii wanataka maendeleo yabakie kwao tu sehemu zingine wabakie nyuma. Watu hawa wanajulikana ni nani na chama chao ni kipi.
acha ukabila na kupenda vya bure
 
Ninyi mliopewa madaraka sasa hivi chuki zenu ambazo mnashindwa kuzidhibiti zitawatokea puani huko mbeleni. Ofisi ya Tanesco inayojengwa ni ya kwake binafsi au kwa matumizi ya umma? Bajeti ya fedha hizo aliidhinisha nani wakati viongozi wasimamizi wake walikuwepo na bado wako madarakani? Mnataka kuonesha chuki zenu dhidi ya JPM kwa kuonesha ni kwa jinsi gani watu wanatakiwa wahudumiwe? Mradi kama huo haupo mahali pengine Tanzania? Kwanini mnaendelea kumzonga mtu asiyekuwepo kujitetea na mnatishia kushitaki wasaidizi wake?

Anzeni kwanza na walioko juu kwa sasa kwa sababu ndio walishiriki moja kwa moja kuidhinisha mradi kama huo.

Chato ni sehemu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kama ilivyo Kizimkazi, Kiwengwa, Mkokotoni nk

Mbona Msoga kuna makazi ya rais mstaafu yenye hadhi ya Ikulu ikiwa na hospitali kubwa ambayo hata Chalinze hawana lakini hakuna kinachosemwa?

Ifike pahala chuki hizi zikome mara moja kwa sababu mnatengeneza VISASI ambavyo havitakoma. Msijidai kwamba mtabaki madarakani, mnasubiriwa chini ili muadabishwe vizuri.

Mnaachia wezi mnafungulia mashitaki feki watu wasio na hatia kwa sababu ya chuki zilizokubuhu, inda na nongwa zinazonuka uvundo wa uharifu ndani yake.

Kumbe wakati JPM analalamika hujuma kufanyika ninyi ndio mnaziongoza kwa kuzipitia kwa wapinzania ambao kimsingi hawakuwa na nia ya kukwamisha maendeleo.

Achaneni na kesi feki ya Mbowe na Sabaya ili kurejesha mstakbali huko mbeleni
Dikteta muuaji
 
Kama mradi upi hauendani na population ya kule na kwa vigezo gani?
Kwanza ile Hospital ya rufaa haikufaa kuwepo Chato, uwanja wa Ndege haukua muda sahihi kujengwa kule Mbuga ya wanyama imefuata nini kule
 
Kwanza ile Hospital ya rufaa haikufaa kuwepo Chato, uwanja wa Ndege haukua muda sahihi kujengwa kule Mbuga ya wanyama imefuata nini kule
Ukishasema “ya rufaa” suala sio iko wapi tena. Ndio sababu watu huweza kutoka Ileje wakalazimika kuja Muhimbili. Hospitali ya rufaa sio issue ya location. Ni suala la uwepo wa medical equipments na wataalam wanaendana na hadhi au rank ya hospitali.

Suala la uwanja wa ndege naweza nisiwe na uwezo wa kukubali au kukataa hoja yako. Sijui ungependa ujegwe wapi.

Mbuga ya wanyama ile ni artificial? Kwani wanyama wakiwa mbugani wanakuhusu nini wewe binadamu ambaye uko mjini? Kama ni utalii, pato sio la chato linaingia wizara ya utalii na maliasili. Na mtalii hawezi kusema mbuga iko mbali au haiko mahali sahihi maana anatoka thousands of miles ulaya au Marekani au Asia atakuja kufika Tanzania kisha aseme mbunga kwanini iko Chato? Au una concern nyingine?
 
Hospitali ya rufaa sio issue ya location. Ni suala la uwepo wa medical equipments na wataalam wanaendana na hadhi au rank ya hospitali.
Pia inatakiwa iwe eneo ambapo ni rahisi kufikiwa na wagonjwa. Mgonjwa hawezi safiri umbali mrefu kutokana na hali yake ilitakiwa Hospital kubwa km ile iwe eneo ambapo ni rahisi kufikika.

Tukiri tu kwamba JPM alikua analazimisha kuikuza Chato haraka iwezekanavyo kabla hajatoka madarakani.
 
Sawa.
 
Back
Top Bottom