Ugatuzi wa madaraka. Magufuli alikuwa anafanya kazi iliyokuwa ifanywe na local government institutions, ila tu yeye alipendelea eneo/wilaya moja. Kungekuwa na serikali za mitaa/mikoa ambazo ziko huru kujiamulia mambo yake na kutekeleza mipango yake mwenyewe, Magufuli asingekuwa na haja ya kufanya aliyoyafanya.
Ugatuzi wa madaraka unasaidia kukuza na kukomaza demokrasia, kugawanya na kupunguzia majukumu central government, na kusogeza maendeleo na huduma kwa wananchi, kwasababu wao ndo wanajua nini hasa wanataka kwenye maeneo wanayoishi.
Serikali iko too centralized, ndo maana hata unakuta ili kujenga zahanati, madarasa, barabara za mitaa, hata choo tu, lazima idhini itoke serikali kuu. Wakati hizo kazi na zingine nyingi zingeweza kufanyika na serikali na serikali za mitaa/mikoa.
Ni vile CCM wana-allergy na kushare madaraka kwa mfumo wa aina wowote ule ndo maana ukiwaambia waziimarishe na kuziacha huru serikali za mitaa, na kuanzisha utawala wa majimbo, wanapinga kwa nguvu zote. Wakati ni faida kwa wote.