Nini kifanyike ili kiongozi asipendelee kwao kama Hayati Dkt. Magufuli alivyoipendelea Chato?

Sema nini kifanyike kiongozi mzalendo kama Dkt Magufuli asije kuuawa? Maana furaha yenu ya kumuua Dkt Magufuli sasa hamfichi, mnajiachia kama vile watanzania ni vilaza hawajui, just wait 2025!
Wauaji wanajitokeza kwa sura ya kukosoa kwamba kilifanyika hiki ama kile kinyume na sheria..................Karma is revolving to trigger at the target bull!!!
 
Mnataka mtu akiwa rais mkoa wake au wilaya yake pasifanyike maendeleo yoyote? Chini ya magufuli pamefanyika maendeleo kila mahali. Mtwara kumejengwa kiwanja cha ndege na hospitali ya rufaa mbona sio kwao magufuli? Mbeya kumejengwa kiwanjwa cha ndege cha kimataifa mbona sio kwao magufuli? Mara kumejengwa hospitali ya rufaa. Ilianza miaka ya 70 magufuli kaimalizia. Mara kiwanja cha ndege kimepangwa kujengwa kuwekwa lami na magufuli. Mara sio kwao magufuli. Ni kila mahali kumejengwa na magufuli. Uwanja wa ndege chato ni wa mkoa wa geita na sera ni kila mkoa kiwepo kiwanja kizuri cha ndege. Tatizo kuna watu nchi hii wanataka maendeleo yabakie kwao tu sehemu zingine wabakie nyuma. Watu hawa wanajulikana ni nani na chama chao ni kipi.
 
Mkuu miradi mingi ya Chato haikujadiliwa kabisa bungeni. Ni kama Rais mwenyewe aliamua kuitekeleza. Na si Magufuli tu. Huu utaratibu wa Marais kupendelea kwao upo siku nyingi, sema tu Magufuli aliupeleka next level, hadi uvumilivu wa watu ukavunjika.
magufuli Mwenyezi Mungu alimchukua muda muafaka, angeendlelea kutawala pengine tanzania sasa ingekuwa imegawanyika sana kikabila na kikanda
 
Wewe hupendi kwenu
Unamatatizo ya akili.
Laana ya magufuli itawatafuna sana
 
acha ukabila na kupenda vya bure
 
Dikteta muuaji
 
Kama mradi upi hauendani na population ya kule na kwa vigezo gani?
Kwanza ile Hospital ya rufaa haikufaa kuwepo Chato, uwanja wa Ndege haukua muda sahihi kujengwa kule Mbuga ya wanyama imefuata nini kule
 
Kwanza ile Hospital ya rufaa haikufaa kuwepo Chato, uwanja wa Ndege haukua muda sahihi kujengwa kule Mbuga ya wanyama imefuata nini kule
Ukishasema “ya rufaa” suala sio iko wapi tena. Ndio sababu watu huweza kutoka Ileje wakalazimika kuja Muhimbili. Hospitali ya rufaa sio issue ya location. Ni suala la uwepo wa medical equipments na wataalam wanaendana na hadhi au rank ya hospitali.

Suala la uwanja wa ndege naweza nisiwe na uwezo wa kukubali au kukataa hoja yako. Sijui ungependa ujegwe wapi.

Mbuga ya wanyama ile ni artificial? Kwani wanyama wakiwa mbugani wanakuhusu nini wewe binadamu ambaye uko mjini? Kama ni utalii, pato sio la chato linaingia wizara ya utalii na maliasili. Na mtalii hawezi kusema mbuga iko mbali au haiko mahali sahihi maana anatoka thousands of miles ulaya au Marekani au Asia atakuja kufika Tanzania kisha aseme mbunga kwanini iko Chato? Au una concern nyingine?
 
Hospitali ya rufaa sio issue ya location. Ni suala la uwepo wa medical equipments na wataalam wanaendana na hadhi au rank ya hospitali.
Pia inatakiwa iwe eneo ambapo ni rahisi kufikiwa na wagonjwa. Mgonjwa hawezi safiri umbali mrefu kutokana na hali yake ilitakiwa Hospital kubwa km ile iwe eneo ambapo ni rahisi kufikika.

Tukiri tu kwamba JPM alikua analazimisha kuikuza Chato haraka iwezekanavyo kabla hajatoka madarakani.
 
Sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…