Nini kifanyike ili kuiondoa CCM madarakani?

Tokosoe hoja bila kuvunjiana heshima
ni muhimu sana ukweli ukasemwa,

na tabia ya ukweli huwa ni mchungu na unauma sana. Na ni jambo zuri na la maana sana ukweli huo ukapokelewa kama ilivyo.

CCM haifanani na chama chochote cha siasa barani Africa na duniani kote, na kwahivyo hakuna namna chama, watu au taasisi ya nadani au nje ya nchi, inaweza kwa namna yoyote ile kuudhoofisha ama kuiyumbusha CCM.

Forget about kuiondoa mamlakani, my friends, ladies and gentlemen 🐒
 
Kuiondoa CCM madarakani”. Hii si hoja. Ni wazo potofu. Halina maana. It’s a non-issue. Non-sense.

Hoja hasa ni jinsi ya kujenga mfumo wa demokrasia ya kweli ya vyama vingi nchini kupitia katiba mpya.

Hilo likiwezekana haijalishi chama gani kitakuwa madarakani. Kitaongoza kwa misingi ya utawala bora. Uchaguzi wa wananchi wa viongozi wao utaheshimiwa. Wananchi wataweza kuwadhibiti viongozi wao wakitenda ndivyo sivyo. Hicho ndicho wanachohitaji wananchi.

Suala la CCM ni ile hali ya kutokuwa “chama cha siasa” Bali “chama dola” kama kilivyoasisiwa na JK Nyerere. CCM inamiliki serikali, mihimili yote ya utawala na vyombo vyote vya dola. Viongozi wake wako juu ya katiba na sheria. Huu ndio MSIBA MKUU wa Taifa la Tanzania leo hii. A real national tragedy.

Unahitajika mfumo wa demokrasia ya kweli kuweka huru serikali, mihimili yote ya utawala na vyombo vya dola vitumikie wananchi kwa haki na kwa kufuata katiba na sheria.

Demokrasia ya kweli hupatikana kwa njia mbili tu: (1) kwa mazungumzo na muafaka wa kitaifa au (2) kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe. The choice is ours. Hakuna namna.
 
Kujitokeza mtaani mkuu, hii ndio njia pekee
 

Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio yatakiondoa madarakani chama hiki haramu.
 
Kuongea na madaktari huko India.
Wakienda huko ,wasirudi.
 
Kwanza Katiba mpya yenye Tume huru ya uchaguzi,Ikiwepo Mgombea Binafsi.Vyombo vya ulinzi Kazi Yao iwe ni kulima Usalama bila shinikizo la chama chochote kilichopo madarakani..
 
Ndoa bora zitakazozaa familia bora ambazo zitakuwa vyuo vya awali kwa watu.
CCM ni jina tu, ila tatizo ni watu walio CCM, ambao hata wakiwa chama kingine, wataendelea kuwa vile walivyo.
Kimsingi, Watanzania ni watu tunaozingua, haijalishi tuko chama gani.
 
Tatizo tunahalalisha wizi
Tutulie tu dawa iingie.
 
isije kuwa wewe ni TISS...
 
Kuwatoa hawa vibaka wazoefu wa KURA ni kazi ngumu - maana wapo radhi kuteka, kuua, kutesa na kupoteza as long as wao wabakie madarakani.

Ni kazi ngumu sana na mbaya zaidi JWTZ wanaona kama hawaoni.
 
ufahamu wa mambo ya siasa na athari zake katika maisha uongezeke miongoni mwa watanzania
Mi naona haya mambo tuyaache kwanza,muda ukifika yenyew tu yatajipanga

Nawashauri wakina mbowe wakalime tu maua kwanza,tukiwa tunasubir watz waamke
 
Yafanyike ya Msumbiji kwa wananchi kuandamana kupinga uchafuzi wa uchaguzi bila kikomo na maandamano yasiratibiwe na Chama chochote cha siasa.
 
Kuiondoa CCM madarakani ni hadi pale upunzani watakapo kuwa na pesa
 
Kwa vile CCM na vyombo vyake wamekataa njia ya kistaarabu ya kuleta mabadiliko ni mapinduzi ya kijeshi pekee ndiyo yanaweza kuwaondoa. Natamani JW lichukue nchi na kuvifutilia mbali vyama vyote vya siasa litawale kwa miaka mitano baada ya hapo iandikwe Katiba Mpya ndipo visajiliwe vyama upya kabisa chini ya usimamizi wa Jeshi. Hatuwezi kuendelea na hadaa ya kuwa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia ya vyama vingi wakati CCM ni chama dola, lazima tuanze upya ili vyama vyote vishindane kwenye uwanja sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…