CCM haiondoki sababu hakuna chama mbadala. Ukienda ndani kabisa kwenye Mashina na mitaa utakuta chama kimoja tu chenye ofisi, viongozi na wanachama. Vyama vingine ni kelele tupu, propaganda zao wanaendesha mitandaoni badala ya kuwafuata wapiga kura walipo.
Mfano halisi uchaguzi huu wa serikali za mitaa, hali si hali vijijini hakuna chama cha upinzani kimesimamisha mgombea. Tena wananchi wengine hawajui hata kama kuna vyama vya upinzani. Imefikia hatua baadhi ya maeneo raia hawajaenda kupiga kura sio sababu wamesusia, bali wanajua na kuamini viongozi wao waliwachagua mwezi Oktoba ktk kura za maoni za CCM.
amini usiamini ni asilimia 3 tu (3%) ya wapinzani ndio waliosimama katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa leo nchi nzima. Asilimia iliyobaki (97) ni wagombea wa CCM.
Halafu kuna ng'ombe sijui nyumbu inaamini kuna nafasi ya upinzani kushika dola tz!