Nini kifanyike ili ubaguzi wa aina hii uondoke? Je, Afrika tunaweza jitegemea?

Hapa ndio utawakubali mwamba kama Idd Amin Dada upumbavu kama huo alikuwa avumilii.
Nyie endeleeni kuwanyenyekea mtawalamba hadi *****
 
Hapo ni rangi tu, haijalishi kama uchumi ni mzuri au mbaya.
Mpaka kufikia kuwa katika hayo mashindano, nina uhakika wazazi wa huyo binti kama wa hao wenzake, pesa zimewatoka kuwaandaa.
Mfano Africa ndio tungekuwa tunawapa misaada na uchumi uko vizuri hali hiyo ingekuwepo ?
 
Mfano Africa ndio tungekuwa tunawapa misaada na uchumi uko vizuri hali hiyo ingekuwepo ?
Uchumi ungekuwa vizuri, pengine tusingekuwa katika nchi zao, ila kubaguliwa kungekuwepo, kwani rangi, au pengine sijui wanafikiri ni uchafu ingekuwepo kama sasa.
 
Ubaguzi ni asili ya viumbe vyovyote visivyofanana,hata sisi tunawabagua wenzetu
 
Imeniuma maana binti yangu kaanza maisha na hao wabaguzi akiwa 3 years! Ni miaka 30 iliyopita, si ajabu naye aliumizwa hivyo
 
Hii imenifanya nichukie sana hii ngozi nyeupe.
Ingawa hata sisi waafrika ni watu wa hivyo sana,ila nimeumia huyo mtoto kubaguliwa.Bora angekuwa mtu mzima.
 
Hapa ndio utawakubali mwamba kama Idd Amin Dada upumbavu kama huo alikuwa avumilii.
Nyie endeleeni kuwanyenyekea mtawalamba hadi *****
IDD Amini sio mfano mzuri kabisa maana yeye pia aliramba makalio ya waarabu.
Ni ujinga juu ya ujinga
 
AU wametoa tamko lolote kuhusu hili jambo?

Huyo mtoa medali amewajibishwa Kwa namna yoyote na chombo kinachosimamia hiyo michezo?

Ubaguzi unaweza kuwepo lakini kitendo kama hicho kufanyika hadharani Tena vyombo vya habari, ni zaidi ya ubaguzi, ni dharau. Na kama Hadi mwisho hakuna kitu kilifanyika kuhakikisha huyo Binti anapewa medal japo Kwa kuchelewa, hata waandaji wa hayo mashindano nao wamekubaliana na hicho kitendo alichofanyiwa huyo binti mweusi.
 
Ubaguz hauwez kuisha kama jamii yako inaemtegemea kiuchumi kiteknolojoa na kiutamadun jamii nyingine. Jikomboe kwanza kwenye hayo matatu then the rest inajisolve yenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…