Nini kifanyike kuharakisha uokoaji Kariakoo

don-mike

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2011
Posts
600
Reaction score
1,178
Niende moja kwa moja kwenye mada.

1. Zije tipper trucks 10, mizigo yote iliyopo ndani ya jengo na nje ya jengo yote itolewe. Hili zoezi lingeweza fanyika toka jana, ila limezembewa, huwezi fanya uokozi na mzigo mzito bado upo juu ya jengo, jengo litaendelea titia.

2. Matofali, mabati, mbao, na vyote ambavyo viko loose kwenye jengo hadi sasa ilibidi viwe vimeshatolewa, hii pia inapunguza uzito wa jengo, jambo hili ilibidi liwe limeisha toka jana, ila bado hatujachelewa.

Kuondoka vitu tajwa hapo juu, kutapunguza uzito wa jengo kwa tani 50 hadi tani 100. Huo uzito ukitoka hutosikia tena jengo linatitia. Pia hata usafi wa sehemu husika utakuwepo.

Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye juzi ametoka kuwa waziri wa mazingira sijui anawezaje kuacha eneo la uokozi chafu kiasi hicho, hata wanaoololewa watapatikana vipi katika hali kama hiyo.
 
Wewe hujasoma fizikia!

Newton First law of Motion.....

An object at rest remains at rest, and an object in motion remains in motion at constant speed and in a straight line unless acted on by an unbalanced force!!

kwa kukufafanulia kwa muktadha wa kwa nini grader halitakiwi sasa....

#kitu chochote kilichotulia kitaendelea kutulia hadi pale kitakapo sukumwa(kusumbuliwa)#

Ukitumia grader yafuatayo yatatokea

👉Kipande kilichoegemea pale Tony Touch kitaporomoka kwa kasi
👉 Mzigo uliopo juu na kasi utapelekea kuvunjika zaidi kwa vyumba vilivyopo chini
👉 Madhara ya mivunjiko au kubanwa kwa watu yatatokea(Yaani utakuwa umetengeneza 2nd collapse)
👉 kwa hiyo badala ya kuokoa utakuwa umewamalizia survivals
 
Hakuna sehemu nimeweka neno excavatoor wala wheel loader. Pia hapa jua unaongea na PEng, nna uzoefu mkubwa kwenye dismantling and demolition plus material handling.

Hiyo kazi inahitaji tu jack hammer, grinder yenye discs za zege na chuma plus manpower. Yani wangeshinda na hivyo vitu usiku, leo jengo lote tayari lingekuwa lishatoka hapo.
 
wizara ya ujenzi na RC awaambie makampuni yote ujenzi makubwa yalete mawinji yao makubwa ,scavetors za kutoboa nk.
mkuu wa mkoa aite vikosi vyake vyote vya ulinzi iwe jkt,jwtz,police,magerez na raia wa eneo hilo. kwenye kambi waache walinzi wa zamu tu.
mkuu wa mkoa aende kwa wenye maduka ya vifaa kama nyundo kubwa,vifaa vya vya kukatia nondo na kuta.ajaze kwenye kilikuu apeleke hapo. hiyo kazi ya mwenzo wa saa2 tu jengo zima linakua nimemwagwa na watu wanatoka hapo.
 
Ukweli ni kwamba
wananchi ndio kundi pekee linaloweza kufanya kazi hiyo kwa weledi na hamasa kubwa kuliko hivyo vikosi ulivyovitaja. Japokuwa wananchi wanapuuzwa.

mambo ya serikali huwa ni kujivuta vuta sana na protocol nyingi zinzopelekea kuchelewesha Zoezi.

Ukisikia tuna mfumo mbovu haya ndio matokeo yake. Wengi wenye nafasi hawana uwezo, ujuzi na ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.

Itoshe kusema. Kama kodi inakusanywa kariakoo inashindwa kutumika ipasavyo kuweka mazingira ya hata kununua vifaa vya uokoaji you ni changamoto sana.

NB. Ifikie watanzani tuache ujinga na tabia za kipumbavu hasa linapokuja swala la kuchagua nani awe kiongozi kwenye jamii yetu.

Kila mtu akiwajibika ipasavyo tutapunguza baadhi ya matatizo madogo madogo.
 
Jambo la kushangaza eti traffic wapo barabarani wanakusanya hela za kubrashia badala ya hawa wote wangepelekwa kwenye uokozi

Yangekuwa maandamano ya cdm usingewaona barabarani wote wangepelekwa kukabiliana na waandamanaji na wengine wangetolewa hadi mikoani ila uhai wa watu hakuna anayejali
 
Tanzania Imekata Pumzi Sasa
 
Hakuna sehemu nimeweka neno excavatoor wala wheel loader. Pia hapa jua unaongea na PEng, nna uzoefu mkubwa kwenye dismantling and demolition plus material handling.

Hiyo kazi inahitaji tu jack hammer, grinder yenye discs za zege na chuma plus manpower. Yani wangeshinda na hivyo vitu usiku, leo jengo lote tayari lingekuwa lishatoka hapo.
Kumbuka kuna watu chini wanaopumua ....hiyo approach yako ingewaacha wakiwa taabani zaidi.
Nondo na matofali yananunulika ila uhai haupo dukani.

Iangalie operesheni kwa jicho la uokozi sio uopoaji miili
 
Jambo la kushangaza eti traffic wapo barabarani wanakusanya hela za kubrashia badala ya hawa wote wangepelekwa kwenye uokozi

Yangekuwa maandamano ya cdm usingewaona barabarani wote wangepelekwa kukabiliana na waandamanaji na wengine wangetolewa hadi mikoani ila uhai wa watu hakuna anayejali
Sio kazi ya traffic police kuokoa kwenye janga la kuanguka kwa jengo at least ungeniambia bus lililopata ajali.
Hivi ulipataje simu ya kujiunga JF ?huku kwenye GTs???
 
Wale wananchi wanaosaidia kwenye uokozi ni kazi yao kwenye janga unaangalia nani mtaalamu si wangeachiwa jeshi la zimamoto peke yao au ndiyo jina lako linasadifu uwezo wako wa kufikiria

Hapo ni kuangalia manpower au hao traffic ikitokea ajali barabarani hawawezi kuokoa kisa wao kazi yao ni kuongoza magari

Wewe kweli jingalao
 
Kumbuka kuna watu chini wanaopumua ....hiyo approach yako ingewaacha wakiwa taabani zaidi.
Nondo na matofali yananunulika ila uhai haupo dukani.

Iangalie operesheni kwa jicho la uokozi sio uopoaji miili
Anachoongelea mtoa uzi ni kupunguza imposed load
 
Kumbuka kuna watu chini wanaopumua ....hiyo approach yako ingewaacha wakiwa taabani zaidi.
Nondo na matofali yananunulika ila uhai haupo dukani.

Iangalie operesheni kwa jicho la uokozi sio uopoaji miili
Screenshot_20241117_185619_Instagram.jpg

Hiki kinachofanyika sasa ndio kitu sahihi na ilibidi jana asubuhi kianze fanyika leo hii ilo jengo lote ilibidi liwe chini tayari, zingukuwa zimebaki nondo tu zimezimama, zege lote lingekuwa lishatinduliwa na jack hammer kuanzia juu kushuka chini.
 
1. Barabara moja iachwe wazi kuwezesha malori kuingia na kutoka eneo la tukio haraka
2. Yawepo malori mengi yamejipanga kuchukua mali na vifusi
3. Vifusi na mali vingekuwa vinapelekwa hapo jirani uwanja wa shule ya Uhuru mchanganyiko (kwa muda viwekwe hapo)
4. Kuondoa mali na vifusi ianzie juu
5. Ni kweli vifaa vikubwa vya ujenzi na ubomoaji vilitakiwa viletwe tangia jana
6. Ulinzi uimarishwe vifusi na mali vinakopelekwa
 
View attachment 3154753
Hiki kinachofanyika sasa ndio kitu sahihi na ilibidi jana asubuhi kianze fanyika leo hii ilo jengo lote ilibidi liwe chini tayari, zingukuwa zimebaki nondo tu zimezimama, zege lote lingekuwa lishatinduliwa na jack hammer kuanzia juu kushuka chini.
hujamsikia shuhuda aliyeokolewa anavyoeleza namna kifusi kilivyokuwa kinashuka kadri wanavyotindua?kama hakuna anayeitikia kwa sasa unaweza kuanza hiyo approach ambayo sasa itakuwa ni uopoaji wa miili na sio uokozi wa ambaye yupo hai.
 
Dead load ni kubwa sana kwenye jengo.
Hapo kuna dead load ya almost tani 150, hiyo deadload inatoka tu bila hata kutindua. Baada ya kutoa deadload ndio uunatumia jack hammer kutindua, hakuna kitachotitia.
 
Nimekumbuka wabunge wote wakiwemo madaktari WA binadamu walivyokuwa wananyunyiziwa Methylated spirit hapo Dodoma kabla ya kuingia bungeni eti wanajitakasa na virus vya covid 19 hadi Shujaa, mkemia JPM akaingilia kati na kuwaambia kirusi hicho akifi kwa spirit!
 
Back
Top Bottom