Nini kifanyike kukuza uzalendo miongoni mwa Watanzania?

Nini kifanyike kukuza uzalendo miongoni mwa Watanzania?

Amani Msumari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
1,830
Reaction score
972
Wanajamvi,

Ili nchi yoyote iweze kiendelea inahitaji wananchi wake wawe na uzalendo. Kwa maoni yenu, nini Kifanyike ili kukuza uzalendo miongoni mwetu sisi raia wa Tanzania?
 
Tatizo ni serikali yetu walivyotutoa kwenye reli na kutuaminisha uzalendo ni kuipenda serikali iliopo madarakani na sio kwa nchi au taifa
Mada hii ni muhimu sana kwa mustakabali wetu kama taifa. Nini Kifanyike?
 
Tafuta clip moja ipo youtube magufuli alipoonana na viongozi wakuu wastaafu. Kuna maneno aliambiwa na Majaji wakuu wastaafu Augustino Ramadhan (Mungu amrehemu) na Barnabas Samata. Majibu ya hilo swali lako yapo kwenye michango yao kwenye kile kikao

Kama huwezi kuiona mwambie mkuu bagamoyo akuletee ile clip humu
 
Binafsi nafikiri Serikali ivisimamie vyama vyote sawa, ila visivyo na wabunge vifutwe. Tume iwe huru na ishirikishe vyama vya siasa ili kujenga uaminifu
 
Tafuta clip moja ipo youtube magufuli alipoonana na viongozi wakuu wastaafu. Kuna maneno aliambiwa na Majaji wakuu wastaafu Augustino Ramadhan (Mungu amrehemu) na Barnabas Samata. Majibu ya hilo swali lako yapo kwenye michango yao kwenye kile kikao

Kama huwezi kuiona mwambie mkuu bagamoyo akuletee ile clip humu

5 July 2018
Jaji mstaafu amkosoa Magufuli Ikulu

Wanajamvi.

Ili nchi yoyote iweze kiendelea inahitaji wananchi wake wawe na uzalendo. Kwa maoni yenu, nini Kifanyike ili kukuza uzalendo miongoni mwetu sisi raia wa Tanzania?
Cha kwanza na muhimu kuliko vyote katika kukuza uzalendo wa kweli , sio wa sasa wa kumsifia rais kila baada ya sentensi moja ni kuitoa ccm madarakani na mwishoe kukifuta kabisa chama kinachoitwa ccm.
 
Wanajamvi.

Ili nchi yoyote iweze kiendelea inahitaji wananchi wake wawe na uzalendo. Kwa maoni yenu, nini Kifanyike ili kukuza uzalendo miongoni mwetu sisi raia wa Tanzania?
Kwanza tuwe na rais asiye mkabila, pili tuwe na katiba mpya, tatu tuwe na tume huru ya uchaguzi, tano kusiwe na udikteta, sita watumishi wa serikali wawe na mishahara mizuri, na saba serikali iweke wazi takwimu mbalimbali za kiuchumi, nk
 
Usawa katika keki ya taifa ni muhimu, unakuta sehemu kuna huduma zote za kijamii pamoja na maji, umeme, afya, barabara safi, hospitali, shule nk na upande wa pili hakuna kitu chochote lakini ikitokea ikaja miradi ya maendeleo baada ya serikali walau ifikirie hata walau kusaidia maeneo ambayo hayana huduma hata moja basi inaongeza sehemu ambazo hizo huduma zipo. Baadhi ya Ajira na nafasi mbalimbali hutolewa kwa kuangalia we u nani. Mwingine anakesi ya trions of money anapewa uhuru na anawekewa dhamana ndo imetoka, mwingine anatoa maoni kinyume na matakwa ya watawala anatupwa jera maisha.Hapa uzalendo utatoka wapi?
 
Alipata wapi huo ujasiri, huwa tunawaona wakina Ibrahim Jay na wenzake , wao kazi yao kuimba mapambio tu.
Hawa ndo walikuwa majaji ndugu. Sio hawa wa sasaivi ambao wanamuogopa raisi kama Mungu. Hawa walikuwa ndo majaji wanaojua nafasi zao kama majaji. Na magufuli angewasikiliza hawa asingekuwa na hizi shida anazopata saivi
 
Magufuli alishasema ukimshauri ndio unaharibu zaidi, in short hapokei ushauri wa mtu.
 
Magufuli alishasema ukimshauri ndio unaharibu zaidi, in short hapokei ushauri wa mtu.
Na Ndo mana tunamstaafisha rasmi siasa mwaka huu 2020 hapo October kwa kuliweka Tundu Antipas Lissu ikulu.

Miaka 5 inamtosha sana Magufili tena Hii ni kwa sababu hapa ni Tanzania tu. Angekuwa nchi z watu wenye akili lile blanda la kutoa tamko na bei ya sukari kupanda tu lingemtoa madarakani
 
Asante sana mkuu Bagamoyo. Uko sehemu sahihi wakati sahihi

JULAI 2018

Hii hapa kwa urefu zaidi Mkutano wa Viongozi wastaafu Majaji, Mawaziri Wakuu, Maspika

4 Jul 2018
Hii ni mara ya kwanza kwa Mhe. Rais kukutana na viongozi hao wakuu wastaafu na kupokea ushauri na maoni yao juu ya uendeshaji wa Serikali na mustakabali wa Taifa. Katika mkutano huo viongozi hao wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwaita kwa lengo la kusikiliza ushauri na maoni yao, na wamempongeza kwa kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi kifupi cha miaka miwili na nusu tangu ilipoingia madarakani.
 
I
JULAI 2018

Hii hapa kwa urefu zaidi Mkutano wa Viongozi wastaafu Majaji, Mawaziri Wakuu, Maspika

4 Jul 2018
Hii ni mara ya kwanza kwa Mhe. Rais kukutana na viongozi hao wakuu wastaafu na kupokea ushauri na maoni yao juu ya uendeshaji wa Serikali na mustakabali wa Taifa. Katika mkutano huo tu hao wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwaita kwa lengo la kusikiliza ushauri na maoni yao, na wamempongeza kwa kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi kifupi cha miaka miwili na nusu tangu ilipoingia madarakani.

Asante mkuu Bagamoyo. Kwenye huu mkutano mie niliwapenda hao majaji wastaafu tu. Ndo mana mpaka kesho hamna watu ninaowaona wa kipekee kama majaji. Hawa watu huwa wana logic sana. Nakumbuka walimuonya vizuri sana magufuli ila akashupaza shingo. Mwaka huu sasa lazima ale kiburi chake kwa kukataa ushauri mzuri
 
Hawa walikuwa biased haki kila kitu haki, kwa nini hawasemi kinachozuia/kwamisha haki ni rushwa? Walijitoa ufahamu.
 
Back
Top Bottom