dour
Member
- Aug 7, 2017
- 7
- 9
UTANGULIZI
Ukuaji wa taifa kimaendeleo inategemea zaidi kujitegemea wa taifa kiuchumi na uzalishaji. Tanzania bado inategemea mataifa makubwa kimsaada na kukopa kama njia ya kujipatia fedha, hali hii husababisha serikali kukopa fedha kwajili ya miradi ya maendeleo ikisubiri kutumia makusanyo ya ndani kulipa deni hilo. Ingawaje uchumi wa taifa unaonekana kupanda lakini bado pato la mtu mmoja mmoja limeonekana kua chini sana.
Imerekodiwa ongezeko la deni la taifa kufikia juni 2024 ni 91.7 trilioni ukilinganisha na 77 trilioni mwaka 2023 ikionesha ongezeko la kasi la 19.1%. Ongezeko hili lina ashiria utegemezi wa hali ya juu ya taifa katka mataifa ya ulaya. Katika Tanzania niitakayo natamani kuona tanzania inakuza pato la ndani na kujitegemea au kutegemewa na mataifa mengine.
Yafuatayo ni maoni yangu katika kuitengeneza Tanzania tuitakayo inayoweza kujitegeme katika pato laka la ndani bila kukopa.
1. Kuongeza uzalishaji wa ndani.
Katika mataifa yaliyo endelea yameonekana kutegemea pato lao la ndani katika shughuli za maendeleo, lakini mataifa yanayo endelea hususani Tanzania bado tunategemea wawekezaji wakubwa kutoka mataifa makubwa, inashangaza kuona mataifa tulio wakimbiza tukiwaita wakoloni na wanyonyaji sasa tunawakaribisha kwa jina la wawekezaji.
Katika kuboresha uzalishaji wa ndani sekta hizi ziwekewe mipango hii.
A) kilimo
Japo kilimo kimekua tegemezi katika maendeleo ya taifa, bado kuna changamoto kubwa zinazowakabili wakulima kama masoko ya uhakika, pamoja na pembejeo. Nina shauri serekali ianzishe mashamba kila mkoa kulingana na hali ya hewa ya sehemu husika. Mashamba hayo makubwa yawekewe usimamizi mzuri.
B)uvuvi
Kunayo mataifa makubwa yanayo tegemea uvuvi kama mkombozi wa uchumi huku wakionesha jitihada za makusudi katika uwekezaji huo. Natoa rai kwa serikali kufuta kodi zote zinazo husu uvuvi na vifaa viingiavyo nchini vya uvuvi. Kuzalisha wataalamu na wabobevu wa uvuvi huku ikitenga bajeti kubwa kuhamasisha na kuwapa mikopo wawekezaji wandani katika sekta ya uvuvi. Serikali inapaswa kuanzisha viwanda kadhaa vya kuchakata samaki kisha wao kugeuka soko kwa wavuvi wadogo na kununua samaki zao kuzichakata na kuuza nje.
2. Ondoleo la kodi kwa wawekezaji wa ndani wanao anza.
Moja kati ya changamoto inayotajwa na wawekezaji wengi wa ndani ni kodi nyingi na kubwa pamoja na vibali vingi vya kibiashara. Nashauri kuwe na ondoleo la kodi kwa mwekezaji mpya mpaka pale atakapo imarika kiuwekezaji ndipo waanze kuchukua kodi. Pili nashauri kuwe na mfumo au ofisi moja ya kuomba vibali vya kiuwekezaji ambao mtu ataingia nakupata vibali vyote kwa wakati.
3. Kuongeza ubunifu na ukuzaji wa teknolojia nchini.
Teknolojia ni moja kati ya kichocheo kikubwa cha uchumi, Mataifa yalio endelea yameonekana yakiuza teknolojia zao kwa gharama sana. Ingawaje tanzania kuna ongezeko la wasomi walio hitimu ngazi za juu lakini ubunifu umeonekana hafifu hii ni kulingana na serikali kutowekea umakini jambo hilo. Nashauri serikali kupitia wizara ya sayansi na teknolojia kuweza kuanzisha tuzo za kitaifa za ubunifu na pia kutenga fedha na kuendeleza mawazo hayo pamoja na kununua ubunifu huo kitaifa.
4. Matumizi sahihi ya rasilimali za taifa katika kukuza uchumi.
Katika nchi ambayo imebarikiwa kua na rasilimali na vitega uchumi vingi inayo nafasi kubwa ya kukua kiuchumi na kujitegemea badala ya kutegemea mataifa mengine. Nashauri serikali kua na mkazo na msisitizo pamoja na ushirikishwaji wa wananchi, ninashauri nini kifanyike katika mifano hiyo michache ya rasilimali kama ifuatavyo
A) vivutio vya utalii
Japo serikali imeonyesha jitihada za dhati katika kukuza utalii lakini bado imejikita zaidi katika kukuza soko la nje. Napendekeza kuundwa kwa sera itakayo hamasisha utalii wa ndani kwa kutoa tamko kwamba kila taasisi hapa nchini iwe ya serikali au binafsi pamoja na taasisi za elimu zote kutembele hifadhi yeyote kwa mwaka mara mbili hii itahamasisha utalii pamoja na serikali kupata mapato mengi sana
B)Madini
Tanzania ni nchi iliyo barikiwa kuwa na rasilimali za madini mafuta na gesi ingawaje uvunaji huo unafanywa na wawekezaji wa nje huku serikali ikimiliki hisa kadhaa tu lakini bado imeonesha kutokunyanyua taifa kiuchumi. Napendekeza kua na lengo kuu la serikali kuwekeza kwenye madini, inashangaza kuona tangu tumeanza uvunaji wa madini bado hatujapata mtambo wa kuchenjua madini wala wataalamu. Serikali sasa inapaswa itenge fedha kununua mtambo huo.
C)Bandari
Serikali inakiri kua pato kubwa la taifa lina changiwa na bandari zetu tunazo zimiliki, katika kuboresha huduma serikali imeona inayo haja ya kumuweka mwekezaji kutoka nje. Napendekeza serikali kuona haja ya kusimamia bandari kwa sababu ikiwa tunapata 70% ya mapato kwenye bandari ikiwekeza yenyewe, ili tuone tunapata faida kwa mwekezaji tunatakiwa tumtoze kodi zaidi ya 70%, na kwa uwekezaji mkubwa anao ufanya itampelekea yeye nae kutoza ushuru mkubwa, hapa atakae umia ni mlaji wa mwisho.
5. Kuweka mifumo thabiti ya ukusanyaji wa kodi.
Japo serikali imekua ikifanya jitihada za makusudi katika uboreshwaji wa ukusanyaji wa kodi lakini bado kuna malalamiko mengi kuhusu ukusanyaji na ukadiriwaji wa kodi huku wanao weza kujieleza kukadiriwa kidogo na wasio weza kukadiriwa zaidi napendekeza kuwe na viwango elekezi vya kodi. Pia napendekeza kuwe na TRA KATA kila kata ili kuwafikia wafanya biashara wote kwa urahisi
6. Kupunguza matumizi ya serikali.
Mikutano ya serikali, ziara za viongozi, misafara ya viongozi, magari ya viongozi pamoja ni mishahara na posho kubwa katika taifa linalopambana kukuza uchumi haileti taswira nzuri, uwepo wa maisha ya kifahari kwa viongozi wetu kunafanya watu wengi waamini kua uongozi ni fursa. Nashauri kue kuna sheria inayo dhibiti matumizi ya serikali yatakayo pangwa kisheria
7. Kutunga sheria kali sambamba na adhabu kali zitakazodhibiti ubadhilifu wa mali za umma.
Ingawaje tunaweza kua na mipango mizuri lakini tukishindwa kudhibiti wabadhilifu bado atutapiga hatua. Inashangaza kuona baadhi ya miradi kubinafsishwa kwa kigezo cha wizi na ubadhilifu. Nashauri serikali kupitia bunge tukufu kutunga sheria yenye kutoa adhabu kali kwa kiongozi atakae kutwa na kosa la ubadhilifu ikiwezekana kufungwa jela maisha au kesi ya ubadhilifu kuingizwa kwenye kesi ya uhaini. Nashauri kuanzishwe sheria ya utekelezaji itakayo mueka kiongozi hatiani akishindwa kutekeleza majukumu ya kusimamia miradi ya maendeleo.
HITIMISHO
Kwa ujumla suala la kutoka kwenye taifa tegemezi kwenda kwenye taifa linalojitegemea ni jambo la kimkatati ambalo kama taifa tunatakiwa turidhiane kwa ujumla kupitia bunge letu tukufu. Natoa rai kwa viongozi kufanya kazi kwa uadilifu na kudhibiti ubadhilifu na rushwa. Natoa rai kwa wasomi wetu wa uchumi kulisaidia taifa ili liweze kujitegemea katika uzalishaji. Ni jukumu lakila mmoja wetu katika kila sekta kuhakikisha anafanya kazi kwa weledi katika kutoa huduma iliyo bora kitaifa na kimataifa.

Upvote
3