Tanzania imeendelea kuungana na mataifa mengine mengi hasa yanayo endelea kukabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira hasa Kwa vijana. Uwepo wa tatizo la ajira katika mataifa mbalimbali duniani hakuipi Tanzania uhalali wa kuto kuchukua hatua mbalimbali kuondokana na tatizo hili kwani Kuna weza hatarisha kesho yetu kama taifa. Tatizo ili linazidi kujidhihilisha kufwatia ongezeko la vijana wengine wanao maliza elimu katika ngazi mbalimbali kila mwaka pasina ajira za kutosha.
Ni kipi Chanzo Cha ukosefu wa ajira kua tatizo katika mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania. Mfumo wa elimu unao mwaandaa mwanafunzi kua wafanya kazi bora katika kampuni fulani na sio kuwa bora kuanzisha biashara ama kampuni zao pindi wanapo kosa ajira, imani ya kwamba tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri pindi fursa za ajira zinapo kosekana, kuitegemea serikali kupata ajira licha ya uwepo wa washirika binafsi, ukiachilia uwepo wa washirika binafsi ongezeko kubwa la wahitimu limezidi kuchochea ukosefo wa ajira. Kwa ufupi, utegemezi wa elimu ya kitaaluma(academic education) kama vile kujua kusoma, kuandika na kuhesabu, elimu ya kitaalamu(professional educatuon) kama vile udaktari, uanasheria, nakadhalika pasipo elimu ya kifedha ndio msingi mkuu wa tatizo la ukosefu ajira nchini, ukosefu wa elimu ya kifedha hasa elimu ya ujasiruamali Kwa vitendo ili kumwezesha mwanafunzi kuweza kujiajiri baada ya masomo kumeongeza Kasi ya ongezeko kubwa la vijana wanao maliza masomo yao na kukosa Cha kufanya. Nini kifanyike kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini.
kuweka kipaumbele katika utoaji elimu ya kukuza ujuzi wa ujasiriamali kuanzia shule za msingi, sekondari hadi vyuoni. kumekua na juhudi mbalimbali kwa serikali katika sekta ya elimu kuandaa wanafunzi wajasiriamali Kwa mfano kuanzisha masomo ya Stadi za kazi Kwa shule za msingi na taasusi ya ujasiriamali ambayo ni hiyari katika vyuo mbalimbali. Ukosefu wa mikakati madhubuti kumepelekea uanzishwaji wa hatua hizi kuto kua na mafanikio Kwa kiasi kikubwa. Ni wakati sahihi Sasa Kwa serikali kutengeneza mtaalaa wa elimu ambao utaweka kipaumbele katika masomo ya ujasiriamali kuwa ya lazima kutoka shule za msingi hadi vyuoni, Kwa mfano, ata kama mwanafunzi atasoma sayansi ya siasa na utawala chuo iwe ni lazima kusoma ujasiriamali. kufanya ivo kutaweza kupunguza kama sio kuondoa tatizo la ujasiriamali kuelekea Tanzania tuitakayo miaka kumi hadi ishirini na Tano ijayo. Tusipo ongeza Kasi ya kuwaanda vijana wa kitanzania kua wajasiriamali, tujiandae kua na ongezeko kubwa la vijana waishio makwao, tujiandae kua na nguvu kazi kubwa isiyo zalisha, tujiandae kupata changamoto kiuchumi Kwani mchango wa raia wengi unaweza kupungua katika kukuza uchumi.
Serikali isichoke kuamasisha watu wake kua wajasiliamali. Hamasa kutoka serikalini kwenda Kwa wananchi kua wajasiriamali kunaweza ongeza motisha Kwa wananchi kushiriki katika ujasiriamali. Serikali inapaswa kuwaonyesha wananchi wake umuhimu wa ujasiriamali lakini pia viongozi wanapaswa kuongoza Kwa mifano Kwa kuanzisha biashara mbalimbali kama ishara ya ujasiriamali, kwani kushindwa kufanya ivo kutaweza kutengeneza imani hafifu Kwa wananchi hivyo kupunguza Kasi ya mapokeo kuhusu umuhimu wa ujasiruamali ndani Yao hasa Kwa vijana.
Serikali inapaswa kukubali kua mafanikio na afya ya uchumi wa nchi unategemea wajasiriamali . Serikali haiwezi kuendeshwa Kwa kutegemea Kodi za waajiriwa pekee, asilimia kubwa ya wananchi wanapaswa kua wajasiriamali. Hivyo basi serikali Ina Kila sababu ya kuwaonyesha wananchi ya kwamba afya ya uchumi wa nchi unategemea wajasiriamali, kufanya hivyo kunaweza ongeza hamasa ya wananchi hasa vijana iwapo wataelimishwa vyema kua wajasiriamali. Uwepo wa mikopo ya 10%, Kila halmashauri Kwa vijana ni udhihilisho wa kua Kuna umuhimu wa vijana kua wajasiriamali lakini pia uwepo wa wajasiriamali walio wahi ajiriwa na kuacha kazi ni kiashiria pia ya kwamba Kuna umuhimu wa kutoa elimu ya ujasiriamali, kama ni hivyo kuna Kila sababu ya serikali kukubali ya kwamba afya ya uchumi wetu inategemea wajasiriamali na hamasa ya kutosha inabidi ifanyike. Mafanikio katika hili yanaweza kupunguza kama sio kuondoa tatizo la ajira nchi.
Vijana lazima waelimishwe ya kua serikali pekee hata Kwa kushirikiana na washirika binafsi hawaweza kutatua tatizo la ajira, hivyo basi ujasiriamali ni nguzo muhimu. Si vibaya kutambua ya kua Moja ya kazi ya serikali ni kutengeneza ajira kwa wananchi wake, mabadiliko ya kitekinolojia na mifumo ya kiuongozi yanabadilisha uhalisia uo Kwa Kasi na kuiacha serikali kutengeneza mazingira Kwa kiasi kikubwa kwa wananchi wake kujiajiri na si kuajiriwa. Hivyo basi Kuna Kila hitaji la kutoa elimu Kwa vijana kutambua ya kwamba serikali pekee na washirika binafsi hawaweza kutatua tatizo la ajira kwa asilimia mia hasa Kwa mataifa yanayo endelea, uamuzi wa vijana kuchangamkia fulsa zitokanazo na ujasiriamali zinaweza changia kupunguza kama sio kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira iwapo vijana wataelimishwa vyema. Vijana wakielimishwa vyema watakua mstari wa mbele kuisadia serikali kuondokana na tatizo hili, sambamba na hilo vijana wakitambua thamani itokanayo na ujasiriamali na kuamua kuwa wajasiriamali wataongeza Kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi kulikoni wakimaliza elimu zao na kurudi majumbani kwao kukaa na wazazi wakisubili kuajiriwa.
Serikali kupitia wizara ya fedha wafanye tathmini ya viwango vya mishahara Kwa waajiriwa. Iwapo Kuna waajiriwa wanalipwa zaidi ya milioni kumi na Tano Kwa mwezi na Kuna mtumishi analipwa laki nne ni vyema kukawa na punguzo la mishahara Kwa watumisha wenye viwango vikubwa vya mishahara ili kuangalia nafasi za vijana wengine kuajiriwa Kwa madhumuni ya kupunguza tatizo la ajira kama kutengeneza ajira mpya zingine ni changamoto. kufanya ivo kunaweza ongeza nafasi za ajira Kwa vijana bila kuathiri ongezeko kubwa la bajeti kwaajili ya mishahara ya watumishi, sambamba na ilo waajiriwa wenye mishahara mikubwa wakiwa na elimu ya ujasiriamali Kwa vitendo wanaweza Kwa upande mwingine kutengeneza fulsa za ajira Kwa vijana wengi.
Serikali inapaswa kuanzisha mikatati yenye uharisia kutatua changamoto za ajira. Kufwatia uanzishwaji wanmtaala mpya wa elimu unao lenga kumuandaa kijana kujitegemea, nidhahili ya kwamba, mtaala huo unaweza kushindwa kuleta mabadiliko chanya Kwa vijana kuondokana na tatizo la ajira, kwani bado kama nchi hatujaanda waalimu ama wakufunzi wa masomo ya ufundi, ujasiriamali kama mtaala huo utakavyo. Hivyo basi, ni ukweli usiopingika ya kwamba richa ya kua na mikakati mbalimbali ya kutatua changamoto ya ajira, tumeendelea kukabiliwa na changamoto ya kukosa uharisia Kwa mikakati tunayo ianzisha na rasimali tulizo nazo kufanya mikakati yetu kua ni yenye mafanikio.
Ujasiriamali, Ujasiriamali Ujasiriamali. Kwa tulipo fikia hatuwezi kuepuka umuhimu wa ujasiriamali kuelekea Tanzania tuitakayo kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira. Vijana lazima waelimishwe ya kua serikali pekee hata Kwa kushirikiana na washirika binafsi hawaweza kutatua tatizo la ajira, Serikali inapaswa kukubali kua mafanikio na afya ya uchumi wa nchi unategemea wajasiriamali, Serikali isichoke kuamasisha watu wake kua wajasiliamali na kuweka kipaumbele katika utoaji elimu ya kukuza ujuzi wa ujasiriamali kuanzia shule za msingi, sekondari hadi vyuoni, kwa kufanya hivyo kutatoa suluhu pekee tuliyo bakiwa nayo kuondokana na tatizo la ajira kuelekea Tanzania tuitakayo. Nje ya changamoto zote tulizo nazo, serikali isichoke kuamasisha wananchi wake kua wajasiriamali na izidi kutengeneza mazingira rafiki kwa wananchi wake hasa vijana kua wajasiriamali, ni njia hii pekee inaweza kupunguza kama sio kuondoa tatizo hili la ukosefu wa ajira kuelekea Tanzania tuitakayo. Kutoa mikopo kama 10% Kwa vijana Kila halmashauri pasipo kutoa elimu kuhusu ujasiriamali hasa Kwa vijana ni kuongeza changamoto ya tija Kwa mikopo hiyo Kwa serikali.

Upvote
7