SoC02 Nini kifanyike kwa viongozi wetu tupate timu bora ya taifa letu la Tanzania?

SoC02 Nini kifanyike kwa viongozi wetu tupate timu bora ya taifa letu la Tanzania?

Stories of Change - 2022 Competition

Nasibu hemedi

Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
11
Reaction score
4
Kwa jina naitwa Ramadhani Selemani Ramadhani ni kijana wa kitanzania nina umri wa miaka 28 kwa sasa leo ningependa nizungumzie mambo mbalimbali yanayo weza kufanyika ilimradi kuweza kufanikiwa kufika mbali katika timu yetu ya taifa.

Mpira ni mchezo wenye washabiki wengi sana duniani kote na nimchezo unaopendwa sana na wenye uwekezaji kubwa huenda kuliko michezo yote duniani. Kwa taifaletu la tanzania pia mchezo huo wa mpira upo na unawashabiki wengi kuliko mchezo wowote uliopo ndani ya taifa letu.

Kwenye nchi yangu ya tanzania kuna michezo mingi sana kama vilbo netbol na kuruka ukamba ila leo mimi napenda kuzungumzia mchezo maarufu sana unaoitwa mpira wa miguu kwa upande wa wanaume na kwa upande wawanawake.


Faida za mpira kwa taifa letu
(i) Kutangaza taifa letu. Mfano tunapoenda kucheza nje ya tanzania tunapaya furusa ya kutangaza taifa letu.
(ii) Huwapa vijana ajira. Kwakua mpira ni kipaji unaweza kuwa hujasoma au umesoma lakini hujafanikiwa kupata kipato kizuri kupitia mpira wa miguu.
(iii) Mpira hujenga mwili. Kwakuwa mpira ni mchezo unahusisha sana mazoezi ya viungo kama kukimbia kuruka na kupiga pushapu kwahio ni mazoezi muhimu kwa mwili.
(iv) Mpira unaingizia taifa kipato. Pale wanapokuja wachezaji kutoka njee kucheza hulipa kodi na hata vilabu vilivyopo vinalipa kodi kwahio taifa linapata faida kupitia mpira wa miguu.

Leo ningependa mada yangu ijikite kwenye timu yetu ya taifa kwanini haifanyi vizuri na je nini kifanyike ili ifanye vizuri tuwe maarufu karibu funiani kote.


Je, Nini kinafanya timu yetu ishindwa kufanya vizuri?

(i) Aina ya wachezaji tulio nao kwenye timu ya taifa ni wachezaji wazuri lakini muunganiko wao sio bora kwakuwa kila mchezaji ana clabu yake na kila clabu inamwalimu wake na kila mwalimu anamfumo wake hivyo wanapo kusanywa kucheza timu ya taifa hawapati muunganiko bora.

(ii) Muda wanao kaa kambini huwa unakuwa ni mdogo sana hivyo hupelekea maandalizi ambayo sio bora kwa kiasi kikubwa.

(iii) Posho ndogo kulinganisha na posho wanazo pata kwenye clabu zao kwahio wachezaji wanacheza kwakuto kujitolea kwakuwa kipato ni kidogo hata wanapo umia inakuwa shida kuupata huduma bora kutoka kwenye timu ya taifa ukilinganisha na clabu zao.

(iv) Miundombinu mibaya ya timu ya taifa ukilinganisha na kwenye timu wanazo cheza wachezaji moja moja.


Je, Nini kifanyike ili kufanya vizuri zaidi na kupata timu iliyo bora?

Viongozi wa TFF na viongozi wa nchi kushirikiana na waziri wa michezo hawa ndio wanao weza kufanya tupate timu bora ambayo itatutambulisha duniani na kutupa heshima kwa sababu ili timu ya taifa ifanye vizuri lazima iandaliwe na ijengewe mipango kwa kuda kidogo.

Hii timu ya taifa tulio nayo ibaki hivi hivi ila kuteuliwe kamati izunguke tanzania nzima itafite vijana wadogo kuanzia miaka 6 na mpaka 14 tupate vijana 50 wenye umri kuanzia miaka 6 mpaka 14 tuwakusanye sehemu moja tuwatengee majeti yao nziri tuwapeleke nchi za ulaya mfano uingereza au ufaransa tuwatafutie akademiki nzuri wasomee mpira tu ndani ya miaka 7 wakae huko huko wacheze mechi nyingi huko ulaya baada ya miaka 7 tuchague vijana walio fikia umri wa kucheza timu za watu wazima. Tuchukue vijana 24 wengine wadogo tuwaache waendelee kukaa hukohuko njee wajifue zaidi. Alafu hawa 24 wawe timu ya taifa tu basi yani wao kazi yao ni kucheza timu ya taifa tu maisha yao yote mimi nina uhakika miaka 7 ya mbele tungekuwa na timu hatari na tishio duniani .

Kama suala la bajeti litakuwa na shida kidogo basi tuteuwe rasilimali moja iliopo nchini kwetu iwe maalumu kwa timu ya taifa mfano tutoe mgodi moja kilakinacho patikana hapo basi nikwaajili ya timu ya taifa tu au tuteuwe mbuga moja mfano mikumi iwe ni kwa ajili ya taifa stars tu hakika tutafanikiwa na tutatangaza haifa letu na kupitia huo mchezo wa mpira tutatangaza sana vivutio vyetu vya utalii na tutaingiza kipato kikubwa sana zaidi ya sasa .

Jambo la mwisho napenda kuwashauri watanzania wenzangu kwa ujumla kuwa watoto wetu tuwape elimu juu ya michezo na tuwaunge mkono ili wafike malengo yao elimu ni bora sana lakini kipaji nibora na kipaji ni ariza pia watambue kuwa michezo ni utajiri michezo ni ajira huria kwahio wazazi na vijana wenzangu tuwape moyo watoto wetu pale tinapogundua kuwa wanavipaji .

Vipaji sio mpira pekeake hapana. Kuna kuimba kucheza mziki kucheza ngoma, kuruka kamba, na mingineyo mingi .

Michezo haijalishi mtu ni mlemavu au ni mzima kuna michezo mpaka ya walemavi kwahio wote kwa pamoja tuungane tutafanikiwa .

Tusisahau kuwa michezo pia ni chanzo na kivutio cha watalii ndani ya taifa mfano kucheza ngoma za asili kama wamasai, wagogo, wahaya, wadigo na makabila mengine yenye utamaduni wa kucheza kiasili huvutia sana watalii wanapo waona na kivuyiwa kuja nchini kwetu na wanapokuja nchi inaingiza kipato kutokana na kodi zinazo lipwa. Michezo ikizorota tunao umia ni sisi wenyewe wananchi na haibu inaingia taifa letu kwa pamoja.

Asanteni sana na naombeni msamaha kama kuna sehemu nimeongea vibaya haya ni mawazo yangu tu. Mwandishi ni mimi mwenyewe ramadhani selemani
 
Upvote 1
Kuwekeza kwenye soka kuanzia academy, vipaji na rasilimali fedha, mtaani kuna vipaji vingi lakini vinaendelezwaje?

Kuacha siasa kuanzia TFF yao imejaa siasa tu kuanzia huyo Rais wao, pia kuwa na uthubutu wa kuacha usimba na uyanga piga chini wachezaji wanaojifanya mapro
 
Tatizo la kwanza ni kwamba tuna watu ambao hawajui mpira wanataka kutoa ushauri kuhusu mpira, wewe ni mmoja wapo! U dnt understand the football industry at all! 🤣🤣🤣🤣

Yaani sababu mbili za kwanza ulizotoa za kwa nini timu ya taifa haifanyi vizuri imeonyesha kuwa huna knowledge ya kutosha kuhusu mpira.
Timu haina muunganiko eti kwa sababu wachezaji wanatoka timu tofauti zenye makocha tofauti🤣🤣🤣. Hivyo ndivho timu ya taifa inavyopatikana bwana wewe. Ni mara chache sana unakuta timu kwa asilimia kubwa wachezaji wengi wanatoka timu moja, spain ya 2010 ni mfano. Timu ilija barca players.

Sababu ya pili ya muda mdogo nayo haina mashiko. Timu ya taifa ya bongo wanasimamisha ligi ili kocha apate muda wa kufundisha timu. Asili ya kazi ya timu ya taifa ni kwamba hupati muda mwingi na wachezaji. Hapo kinachoangaliwa ni kwamba kocha atizama ni njia gani bora ya kuwatumia wachezaji aliowaita ili kujenga timu. Pili mbinu za kukabiliana na wapinzani tunao enda kucheza nao.

Kitu kikubwa ni kwamba tayari una wachezaji ambao wana ufundi wa hali ya juu na uelewa wa mbinu mbali mbali zinazotumika katika mpira wa kisasa. Sisi je hao wachezaji wetu wana ufundi wa hali ya juu? Utaona basi kuwa kazi kubwa inatakiwa ifanyike huko kwenye vilabu na makocha wa vilabu maana wao ndio wanakuwa na wachezaji hawa kwa muda mrefu. Swali la kujiuliza huko vilabu i wanapata kufundishwa vizuri?

Tukija suala la maslahi, sio jambo geni kwa timu za taifa za africa kutokuwathamini wachezaji. Mifano ipo, mambo ya nigeria kugomea kicheza wakati bonus hazijalipwa. Rais wa shirikisho kusafiri yeye na familia yake first class wakati wachezaji wao economy wakati wao ndio watendaji wakuu. Hizo zote zinaongesha kuwa sie hatuwajali wachezaji wetu.

Unasema kwamba tutafute vijana 50 tuwapelekea ulaya kwenye academies huko. Kwanza selection ya wachezaji inagubikwa na mambo ya ajabu....mtoto wa mjomba ataenda wakati hana kipaji. Pili sie tunadanganya sana umri. Mfano mashindano ya u20 mijeba ya miaka 24 wanacheza alafu tunategemea kufika mbali...kujidanganya.
Anagalia records za worldcup ya vijana u20 huko utaona timu za africa zimeshinda, sasa fast forward miaka mtano mbele, hao wachezaji huwaoni. Hiyo ndio africa kaka.

Tukiendelea kiufundi zaidi, je unajua ni wachezaji wangapi wanapata professional contract kutoka kwenye academies? 0.5% yaani 1/200 players ndio wanafanikiwa. Sasa unaposema upeleke wachezaji 50 means unaweza usipate ata mmoja🤣🤣🤣🤣🤣. Hii industry usichukulie poa mzeya.ni wachezaji wachache sana wanaweza che professional football.

Sie tungefuata kile walichofanya ndugu zetu uganda. Tufanye kazi kwenye mashule. Huko tutakuwa na uhakika kwamba wachezaji wenye umri sahihi na watakuwa na elimu pia.
 
Ukumbuke nimesema ni umawazo yangu na sio kuwa nimesema ndio ilivyo kwahii wewe kama wewe unapoona labda mimi nimeandika hovyo basi ni nafasi na wewe ukaeleza yaliyo sahihi ili usaidie nasio kukosoa lengo ni kufabikiwa sasa ukikosoa haliakua wewe hukutoa wazo lolote unakuwa bado hujajenga
 
Back
Top Bottom