Macbook pro
JF-Expert Member
- Jul 15, 2020
- 722
- 1,030
Habari zenu ndugu zangu na wanajamvi letu pendwa la HHM.
Nimekuja kwenu tena kama mwanajamvi kujifunza kitu kutoka kwenu.
Kama utafuatilia hapo nyuma niliweka uzi wangu juu ya kukosa morali na mvuto na ajira yangu. Labda niweke hivi, Kabla sijaingia kwenye ajira nilikuwa na kibiashara changu ambacho kimenisaidia sana na mpaka ajira zinatoka kwamba nimepangiwa huku Mtwara nilikuwa nimeifikisha nyumba yangu katika hatua ya Mwisho kabisa. Na Biashara ipo bado inaendelea so mimi nikawa nimeiacha Biashara nikamwacha mdogo wangu wakisaidiana na mrs kusimamia biashara yetu. Yeye mdogo wangu huwa namlipa mshahara kama mfanyakazi maana natambua yeye sio mmiliki wa Biashara ila ni ndugu na anafanya vizuri.
Baada ya kuwa nimekuja huku kusema ukweli mipango yangu na mategemeo yangu yanaelekea kukwama. Suala la uhamisho ni ngoma nzito mana hizi Halmashauri hawapitishi uhamisho kama huna wa kubadilishana naye. Na sina connection ya simu moja ambayo inaweza kunisaidia kusukuma mchakato wa kuomba kuhama nirudi nikajumuike na familia. Nahisi kukata tamaa na kuchoka kuishi mbali na familia. Sokilicho tawala akili yangu ni mawazo ya kuachana na hii kazi nirudi nijumuike na familia yangu na nikaendelee kusimamia Biashara yangu na kuachana na ajira za utumishi.
Nataka kusikia kutoka kwenu, wale ambao mmewahi kuachana na ajira za serikali na kujitegemea au kufanya kazi kwenye mashirika binafsi, Ni nini ilikuwa sababu kubwa kwako hadi kuwaza kuondoka huko na nini ilikuwa changamoto baada ya wewe kuachana na ajira ya utumishi wa umma. Naomba tusaidiane mawazo.