Nini kilikuwa chanzo cha mapato ya Bwana Yesu?

Hii thread iende Jamii Intelligence ndiko size yake huko. Umeongea vitu vigumu na vikubwa sana ambapo sisi watu wa kawaida inakuwa ngumu kukuelewa.
Mkuu hii ya kawaida ila inawatoa wengi nje ya kasha.

Maana waislam wanampenda na wanamjua wanamuita nabii, na wakristo ndio kiini ila Leo tunataka tumjadili katika angle ya kiuchumi.
 
Maria Magdalena.
Maria Magdalena alikiwa ni miongoni mwa masponsa wa nguvu wa Yesu Kristo wa Nazareti.
Dada huyu,alikiwa ni malkia wa eneo liitwalo Magdala( Hata jina lake, Maria Magdalena aliitwa kwa sababu hiyo,Maria ndo lilikiwa jina lake na Magdala ndo sehemu alipokiwa anatoka.Ifahamike hii ilikuwa ni desturi ya watu wa kale kuwaita majina watu wengine kwa kuzingatia majina yao na sehemu walipotoka,kwa mfano: Simoni Mkirene,kirene ni mji uliopo ALGERIA) Hivyo basi,ilifika kipindi Maria Magdalena aliamua kuachana na habari za kuongoza na kumua kumfuata Yesu Kristo.Kwa kuwa alikiwa ni malkia,ni wazi alikiwa na pesa ya kutosha na kitendo cha yeye kuanza kumfuata Yesu Kristo wa Nazareti,kilimfanya atumie pesa yake yote kuchangia na huduma ambazo Yesu Kristo wa Nazareti alikiwa akizifanya.
 
Hapa nadhani ni pale alipotaka Punda kuingia Naye Yeriko Kifalme. Aliwaambia mumchukue mkimkuta mwenye Naye akiwauliza wamwambie Yesu anamtaka.


Hapa nadhani alimrudisha na hakuwa na haja ya kumiliki punda wakati kesho yake anaanza suluba.
Ndio, lakini huo ndio ulikuwa mfumo wa maisha yake......
Alipowatuma wanafunzi wake kuhubiri, aliwaambia wasibebe chochote watakula kwa hao hao wanaowahubiria.
Alikuwa na Jina, ilikuwa ni fahari kuwa naye nyumbani kwako kwa ajili ya kalamu.

Pia maria Magdanalena na kundi la wanawake waliokuwa wakimfuata Yesu kila aliko, walikuwa wakiwahudumia.
 
Hivi hizi missile enzi za Yesu si ilikuwa ndio mishale
Miaka zaidi ya 1000 kabla ya Yesu kuna mfalme mmoja wa Israel alibuni silaha za hatari sana. Japo vita vyao havikuwa vya masafa marefu ila enzi za Yesu Warumi walikuwa na silaha kalikali hapo sioadvanced kama hizi.

Kuna Bomu flani ambalo linategeswa kwenye projectile flank likrushwa linatua na kuteketeza kabisa hilo eneo. Warumi walikuwa na hizo tech.

Pale enzi za Yesu walikuwa wanachungwa na Mikuki na Majambia sanasana. Hadi vita ndio mrumi alishusha vitu heavy.
 
Yesu hakuwa na pesa.

Kwanza pesa ya Nini?

Maana walikuwa wanatembea kwa miguu mwanzo mwisho.

Walikuwa wanakula kwa wafuasi ( kualikwa nyumbani kwa watu )

Ukitaka kujua hakuwa na pesa, Kuna siku Yesu alidaiwa Kodi akawa Hana na hata wanafunzi wake hawakuwa na kitu.

Akaamua kumtuma mwanafunzi wake aende mtoni akatupe ndoano, samaki was kwanza atakayetoa amcheck mdomoni atakuta sarafu. Hiyo sarafu ndio alilipa Kodi.

Hakuma sehemu inayoonesha kiwa Yesu alikuwa na wahasibu kwaajili ya kutembea na pesa
 
Sasa vyanzo vya mapato si samaki wenye pesa tumboni, unajijibu afu unauliza teena.
Hilo ni tukio moja tu, na alishtukizwa na ilikuwa agome Kutoa. Na inaonekana mlengwa alikuwa yeye na petro tu labda na Yuda myudea. Maana ile kodi walitoa waliozidi miaka 20. Wanafunzi wa Yesu wengi walikuwa mateens umasikini ambao wazazi wao hawakuwa na Pesa za kuwalipia kwenye Shule za kibishoo za wakina Shemmai.

Ndio maana walikuwa wavuvi tu.

Kiasi alicholeta petro kilikuwa ndicho kinahitajika hakikubaki. Na hakutumia hiyo mbinu tena kuraise fund.
 
Nimeanzia kusoma chini kuja juu.

Para ya chini inapotosha. Yuda iskariyote alikuwa mtunza fedha na alikuwa anabeba mkoba.


Angekuwa Yesu anaungunga bado angetembea na mkoba wa magombo ya Isaya.
 
Acha uongo ndugu yangu
 
Wakuu nawakumbusha nimepata point nyingine.

Story na mahubiri yake mengi alizungumzia Pesa/mali kuliko hata kumuamini. Shida kubwa ilikuwa ni Pesa.



Nadhani lazima na yeye alikuwa nazo ili hoja zake zisikilizwe. Siamini kama Yesu alikuwa motivational speaker ambaye hakuwa na mfano kwa alichofundisha.
 
Nafuatilia story kwa umakini napata mambo mengi ambayo nilikua siyajui
Nafuatilia story kwa umakini napata mambo mengi ambayo nilikua siyajui
Fuatilia Mkuu.
Yesu alitembea na pochi/mkoba wa Pesa/ATM cardza wakati huo na hakuwa na gombo wala kitabu. Hivyo alikuwa anavisomea hekaluni.

Maneno ya Mungu walikuwa kichwani tu
 
This was emergency.
Labda Yuda alikuwa katoka kidogo ikabidi atumie mbinu mbadala
 
Mkuu ubarikiwe sana.
Hili nilikuwa sijui.

Kumbe wazee wa upako wako sahihi kuchukua misaada yetu ya sadaka hadi wananunua maJet.

Ila walikuwa wanampe Pesa nyingi sana hadi kutembea na mtunza Pesa???
Any organization.(taasisi) lazima iwe na utaratibu. Hivyo Yesu alikuwa complete ndiyo maana aliandaa na viongozi baada yake . Petro juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, Yuda ambaye ni mhasibu and etc. Kikundi kilikuwa kamili kanisa.

Luka 22:24(struggling ya madalaka)
[24]Yakatokea mashindano kati yao, kwamba ni nani anayehesabiwa kuwa mkubwa.
And there was also a strife among them, which of them should be accounted the greatest.

Yesu alikuwa na mfumo kamili wa kiutawala.katika kikundi chake. Hata baada yake utaratibu uliendelea
Matendo ya Mitume 4:34-35
[34]Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa,
Neither was there any among them that lacked: for as many as were possessors of lands or houses sold them, and brought the prices of the things that were sold,
[35]wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji.
And laid them down at the apostles' feet: and distribution was made unto every man according as he had need.

Hata hivyo miujiza mingi ilifanyika ili kupata mahitaji yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…