Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?

Nguruvi...
Unayoandika yana maana sana kwangu na nayasoma na nakujibu kwa adabu.

Nimekwambia unanifurahisha sana.

Hakika naamini watu wengi wanatusoma na wananufaika na majadiliano yetu.
 
Nguruvi...
Unayoandika yana maana sana kwangu na nayasoma na nakujibu kwa adabu.

Nimekwambia unanifurahisha sana.

Hakika naamini watu wengi wanatusoma na wananufaika na majadiliano yetu.

HISTORIA YA TANU KUTOKA NYARAKA ZA SYKES

KISA CHA ALLY SYKES, DENIS PHOMBEAH NA KENNETH KAUNDA TANGANYIKA NA MKUTANO WA WAPIGANIA UHURU KUSINI YA SAHARA 1953

SEHEMU YA KWANZA

Mwaka wa 1953 Harry Nkumbula alikuwa amechaguliwa rais wa African National Congress (ANC) na Kenneth Kaunda aliteuliwa Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kaskazini, Northern Rhodesia sasa Zambia.

Mwezi Agosti Kaunda akawa Katibu Mkuu wa ANC. Haukupita muda Kaunda akaanza kupeleka barua Nairobi, Dar es Salaam na Johannesburg akiitikia rai ya Kenya African Union na chama cha African National Congresss (ANC) cha Afrika ya Kusini kualikwa vyama vya ukombozi kuja Lusaka kwenye mkutano wa vyama vya siasa vya wazalendo kutoka nchi zilizo Kusini mwa Sahara.

Hivi ndivyo ilivyokuwa kuwa ujumbe wa watu watatu wa TAA ukaalikwa na Kenneth Kaunda, kuhudhuria mkutano wa Pan African Congress (ANC) mjini Lusaka.

Mwezi wa Novemba, 1953 Ally Sykes alipokea barua kutoka kwa Kaunda akimwalika kuhudhuria mkutano huo.

Wakati ule ANC ilikuwa na manung'uniko kadhaa dhidi ya Waingereza na ilikuwa imeamua katika mapambamo yake kutumia njia za amani ambayo katika barua ambayo Kaunda alimpelekea Ally Sykes aliielezea njia hizo za amani kama hivi, ‘’Hutashirikiana na mtu yoyote katika shauri lolote litakalokuwa na madhara kwa maslahi ya Waafrika.’’

Waafrika nchini Rhodesia Kaskazini walikuwa wanapambana dhidi ya mfumo wa kura tatu ambao baadaye ulitwishwa Tanganyika na Gavana Edward Twining wa 1958.

Baadhi ya malalamiko ambayo Kaunda na ANC iliyoyaona kuwa ni madhara kwa maslahi ya Waafrika ilikuwa uendelezaji wa mashamba na nyumba za Wazungu katika nchi yao.

Lakini suala lililokuwa likiwashughulisha sana watu wengi lilikuwa ni ule msimamo dhidi ya muungano wa nchi yao yaani Northern Rhodesia na Southern Rhodesia.

Kaunda alikuwa akifanya mpango wa kuchukua hatua dhidi ya muungano huo kwa kuwaondosha wafanyakazi wa Kiafrika kutoka kwenye mashamba ya Wazungu na makandarasi wa ujenzi waliokuwa wakifanyakazi za ujenzi wa nyumba za walowezi.

Halikadhalika Kaunda alikuwa akifanya kampeni dhidi ya ubaguzi wa Waafrika.

Kaunda na chama cha ANC kilikuwa kinakusudia kuziunganisha jumuiya zote za Waafrika zilizokuwa zinapinga ukoloni na kuunda Baraza la Waafrika wote kwa ajili ya Afrika iliyo Kusini mwa Sahara ili kuwa na nguvu za umoja wa Waafrika.

Katika kutayarisha mkutano huo mkuu Kaunda alipanga kuvishirikisha Chuo Kikuu cha Makerere Uganda, Achimota Ghana, Fort Hare Afrika ya Kusini na baadhi ya vyuo vikuu nchini Uingereza, India na Marekani.

ANC ilikuwa na mpango wa kuyashughulikia maswala saba katika mkutano huo.

Katika kutayarisha mkutano ule Kaunda alifanya kazi na Rev. Michael Scott na pia alikuwa akitafuta msaada wa Canon Raven wa Maddingley Hall Cambridge na Arthur Lewis, mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Manchester.

Baada ya kupokea mwaliko ule tarehe 12 Novemba, Ally Sykes alimwandikia barua Kaunda akimthibitishia kushiriki kwa chama Tanganyika African Governemt Servant Association (TAGSA) na TAA kwenye mkutano huo.

Denis Phombeah na Bhoke Munanka, katibu wa TAA Jimbo la Ziwa walikuwa walichaguliwa kuwa wawakilishi wa TAA.

Tarehe 1 Desemba, Alexander Tobias aliyekuwa katibu wa TAA alimwandikia barua Kamishina wa Kazi, G, A. Bennet akimuombea ruhusa Ally Sykes ahudhurie mkutano huo wa Lusaka.

Bhoke Munanka alinyimwa pasi ya kusafiria na serikali na kwa hivyo hakuweza kusafiri. Tarehe 10 Desemba, Ally Sykes na Phombeah baada ya kupewa ruhusa na serikali kuhudhuria mkutano huo waliondoka kwa ndege ya aina ya Dakota ya Central African Airways kwenda Lusaka kupitia Salisbury, Southern Rhodesia.

Ally na Phombeah walikuwa ndiyo Waafrika pekee ndani ya ndege hiyo.

Walikuwa wasimame Salisbury na kisha waondoke kwenda Lusaka siku iliyofuata.

Wazalendo hawa wawili wajumbe wa mkutano ule walikuwa wamepanga kufikia Ambassador Hotel, Salisbury, kwa usiku ule na hoteli ilikuwa imethibitisha kuwa imekwisha tayarisha malazi yao.


Image may contain: 2 people, people sitting, text that says 'LIFE'
 
Basi kijana unapoanza kuandika anza na introduction siyo unarukia katikati kama kila mtu anajua unachoandika ni nini.
 
Basi kijana unapoanza kuandika anza na introduction siyo unarukia katikati kama kila mtu anajua unachoandika ni nini.
Kiranga,
Mimi ni mtu mzima ujana nimepita miaka mingi nyuma.

Mjadala umetoka mbali bahati mbaya wewe umeukuta kati ndiyo maana unauliza utangulizi.
 
Kiranga,
Mimi ni mtu mzima ujana nimepita miaka mingi nyuma.

Mjadala umetoka mbali bahati mbaya wewe umeukuta kati ndiyo maana unauliza utangulizi.
Mimi naongelea bandiko lako la kwanza kwenye uzi huu.

Yani umeanza kuendesha gari mwanzo ghafla bin vuu spidi ya maili 120 kwa saa.

Unaandika ukiwa unakimbizwa?
 
Mimi naongelea bandiko lako la kwanza kwenye uzi huu.

Yani umeanza kuendesha gari mwanzo ghafla bin vuu spidi ya maili 120 kwa saa.

Unaandika ukiwa unakimbizwa?
Kiranga,
Mbona lugha kali?

Nifahamishe tu unachotaka kufahamu kwa taratibu In Sha Allah nitakueleza.
 
Ha ha ha.
Abdul Sykes anajulikana JF. Povu la nini sasa?
Hahaha...hicho mnakisoma na kukiamini ninyi huko misikitini, madrassat na kwenye mikutano yenu ya kidini

Ila LEGACY ya Mwl. J.K Nyerere haitofutika wala kufutwa asilani.

Huyo Abdul Sykes anajulikana JF tu kwa watu wachache, tena haaminiki.
 
Kiswahili hujui Madam.
Tatizo bibie una mdomo ningekufunza kiswahili.

Kufananiza ndio nini?

Wewe usiyejua kuandika kama Mtume wako Muhammad (S.A.W) ulipaswa ukajifinze kwanza kuandika vizuri kabla ya kuja kumtetea Muumin mwenzio
 
Yego...
Akiwa na ghadhabu mtu hawezi kufikiria vizuri.

Nyerere alikuwa Pugu akisomesha na alipelekwa na Joseph Kasella Bantu nyumbani kwa Abdu Sykes.

Mwalimu alipoacha kazi ndiyo akahamia Dar es Salaan na kupokelewa na Abdul Sykes.
Nilikuja hapa kucheka na kweli nimecheka sanaaa.
 
We mzee,
Baada ya kugundua hila ovu katika maandishi yako, nayapuuza. Huwa nakuja hapa kuwatahadharisha wasio tambua hila zako.
Hapo ulivyomuovu unasubiri kwa watu usiowapenda wafe uendelee na hila zako! Uombe mungu wako safari hii usife wewe kwanza!
Anachokitafuta siku zote bahati mbaya sana kiko mbele yake kwa mabilioni ya Miles!
 
M...
Zamani nikiandika tanzia. Abdilatif Abdallah mtaalamu wa Kiswahili akaniambia hicho ni Kiswahili cha bara.

Sisi watu wa pwani tunasema "taazia," kwa kuwa neno lenyewe asili yake ni Kiarabu.
Na ukaamua ukariri alivyokuelekeza hivyo au sio? Wazanzibar na hata vijana wengi wa wenye elimu ya dini hupenda kuongea , kuandika kiswahili kwa namna flani wao kuonekana waarabu! Inastaajbisha maneno ya kiarabu yaliyoletwa kuwa ya kiswahili hayo tayari yapo katika kiswahili na haina haja ya kuyatamka, ama kuyaandika kwa namna ya lafudhi za kiarabu. Utasikia
1. Nadhwifu badala ya nadhifu
2.taazia- Tanzia. nb
 
Sela...
Naam.
 
Ilikuwaje ukashindwa kuuliza mhusika akiwepo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…