Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #241
Nguruvi...Of course hayawezi kuwa na maana kwako kwasababu hayalingani na lengo lako.
Haya ninayoandika yanamaana sana kwa wasomaji.
Nina uhakika Prof Shivji na Prof Saida, watakaa kitako kufikiri ikiwa kauli waliyosoma kwako kwamba Abdul alimpokea Nyerere ni upotofu . Sidhani kama wanaweza kusimama mahali na kuitetea!
Wewe unaweza kwasababu huna aibu, sijui kama wao wanaweza
Kwa Wanajamvi, hasa vijana haya yana maana sana kwao.
Kwanza , wanajifunza kusoma kwa kufikiri na kuunganisha mtiririko wa habari
Pili, inawakinga kumeza uongo bila makosa , kwamba, umri wao unatumika tu kuwa 'exploit'
Tatu, inasaidia pia 'wafuasi' wako wasome maandishi kwa uangalifu, kinyume chake wanaweza kuangukia pua
Sasa kama umeshindwa kuthibitisha uwepo wa katiba ya AA na TAA ya Abdul, wao wanaweza nini?
Muhimu zaidi ni kueleza jinsi Abdul Sykes alivyokuwa overrated na vitabu vyako katika jitihada za kumdunisha Nyerere. Kwa vigezo vyote Nyerere atabaki kuwa Nyerere na sifa zake na Abdul atabaki kuwa na sifa zake.
Huwezi kumfanya Abdul awe zaidi kwa kumnyanyasa au kumdhalilisha Nyerere
Nyerere anatetewa na historia, ambayo haiandikwi , kubumbwa au kufinyangwa. Ni historia inayojidhihiri kwa muda na matokeo. Ndiyo maana miaka 20 tangu afariki bado '' historia inamtetea'' akiwa amelala kaburini tuli
Kwamba alilishwa mayai kwa Sykes, na alivaa Kaptula au alipewa pesa za kununua ng'onda, au alikwenda sokoni na kikapu bila pesa, hayo hayaondoi ukweli mwingine wowote kuhusu aliyofanya katika kuongoza harakati za uhuru
Ni Nyerere aliyebadilisha siasa za barazani na kuzipeleka majimboni , Tanganyika na UN. Siyo Abdul Sykes
Tena tukichamba zaidi, kubwa la Abdul ni kuongoza genge la wahuni kwenda kutandika wazee wake ili achukue utawala wa baba yake. Hakuandika Katiba wala baba yake hakuandika. Hawakupeleka siasa mikoani zaidi ya Tandamti na Agrey.
Historia si hisia, tenzi au simulizi. Si mahoka au ngano, ni mtiririko wa matukio usiohitaji nakshi au uvumba.
Nawahi Magila, leo tunamuoza mtoto wa baba shangazi.
Unayoandika yana maana sana kwangu na nayasoma na nakujibu kwa adabu.
Nimekwambia unanifurahisha sana.
Hakika naamini watu wengi wanatusoma na wananufaika na majadiliano yetu.