Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
-
- #381
Mokaze,Hata Yesu alilia na kulalamika msalabani:- Eloi Eloi lamasabchtan.
Yaani; Ewe Mungu, ewe Mungu mbona waniacha.
Kama Yesu pamoja na utukufu na ukubwa wake wote alimlilia Mungu, vipi mimi mtu hohehahe nishindwe kulia???!!!.
Kuna siku kuna mtu aliuliza kwa nini watu kama Maria Nyerere wasiulizwe kama kunakuwa na utata wa baadhi ya matukio? Hii mada ilisubiri mpaka watajwa wafe?Kwa hiyo kwako wewe kipimo cha mtu kuijua historia kwa usahihi kuhusu miaka ya mwanzo ya Mwl Nyerere hapo Dar ni kuzaliwa na kukulia Dar sivyo?kuna watu wakiandika kumuhusu Nyerere kabla hata huyo mtoto wa Abdul hajazaliwa na tena amekiri wazi kwa maandishi akisema “KATIKA AKILI ZANGU ZA KITOTO”,so unapotaka wote kutubeba kwenye kapu moja kuamini kila kinachoandikwa na mtu ni sahihi jipime vizuri uelewa wako.
Kwa maneno yake mwenyewe mzee Said hapo juu amesema “Mwl Nyerere alikaa kwa Abdul miezi mitatu tu” so wa mikoani au wageni wa Dar tuamini kwamba harakati zote za Mwalimu kudai uhuru wa kitaifa alizifanya akiwa Butiama ila akaja kufanikiwa alipopata hifadhi ya miezi mitatu kwa Abdul?mkuu haupo na wajukuu zako sebuleni kwako ukiwapa hadithi hapa upo na watu wazima wanaochakata vizuri bongo zao kukubali wanachoambiwa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Devil is in the details. Hapo mtu asiyeijua Pugu kuwa iko dar anaamini moja kwa moja.Mkuu hapa ndio unawachanganya watu. Kwani pugu sio dar?
Aende akawaulize wakiwa hai hataki anasubiri mpaka wafe,unfortunately siku wakitutoka Mzee Mwinyi au Dk Jakaya tuyategemee haya yakitokea laah haijawa hivi basi zitakuwa zimewabeba imani zao coz huyu ataandika anavyoandika but akiwa ni mrengo anaoamini yeye hutamuona akiwazungumzia vibaya wahusika kasheshe uwe upande wa pili basi utajuta.Kuna siku kuna mtu aliuliza kwa nini watu kama Maria Nyerere wasiulizwe kama kunakuwa na utata wa baadhi ya matukio? Hii mada ilisubiri mpaka watajwa wafe?
Siku akifa Maria Nyerere tena atawekewa maneno maneno mdomoni. Nafkiri kuna haja ya kuyaweka haya mambo bayana kabla baadhi ya watu hawajafa. Naona Mzee Saidi anakichaka cha kujificha kuendesha agenda zake.
James...Kuna siku kuna mtu aliuliza kwa nini watu kama Maria Nyerere wasiulizwe kama kunakuwa na utata wa baadhi ya matukio? Hii mada ilisubiri mpaka watajwa wafe?
Siku akifa Maria Nyerere tena atawekewa maneno maneno mdomoni. Nafkiri kuna haja ya kuyaweka haya mambo bayana kabla baadhi ya watu hawajafa. Naona Mzee Saidi anakichaka cha kujificha kuendesha agenda zake.
I think, this is the agenda. MS hakuna anayebisha ushiriki wa mtu mmoja mmoja ktk Uhuru wa Tanganyika. Inshu kubwa hapa Nguruvi aliipambanua ni wewe kumpa jina baya Nyerere!Mokaze,
Kuna mengi najizuia kuyasema kwa kuchelea isionekane mie nimeghadhibishwa na hizi "provocations."
Chuo Cha CCM Kivukoni walitamani sana kuanza historia ya TANU na Julius Nyerere na wakafanya hivyo wakiamini kuwa historia hiyo itasimama.
Kitabu kikatoka mwaka wa 1981.
Kwa hakika kitabu hiki ni kichekesho na hawajaweza kuchapa toleo jingine la pili.
Hakuna mhadhiri yeyote Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Idara ya Historia anaefanya rejea ya kitabu hiki kwa wanafunzi wake.
Mimi nikaamua kukijibu kitabu hiki kwa namna nyingine na yenye ushahidi ambao Kivukoni hawataweza kuupata popote.
Nikaamua kutumia "biographical approach," yaani kuiandika historia ya TANU kupitia maisha ya viongozi wa African Association na TANU.
Hapa ndipo pagumu sana kwa yeyote ambae ana hamu ya kunipinga.
Tayari nilikuwa na mswada wa Kleist alioandika mwenyewe kwa mkono wake kabla hajafa mwaka wa 1949.
Mswada huu nimeshaueleza mara nyingi hapa jamvini ni mashuhuri.
Historia ya vipi yeye Kleist alihusika kama katibu katika kuunda African Association imo ndani ya mswada.
1950 Abdul Sykes akachukua uongozi wa TAA mwaka mmoja baada ya kifo cha baba yake.
Hapa napo nikawa na Nyraka za Sykes kila kitu kimo humo.
Utaona hapa baba na mwanae wote wamehusika na mwamko huu wa Waafrika wa Tanganyika kujitambua kati ya 1929 hadi uhuru unapatikana 1961.
Kivukoni wao kwa bahati mbaya sana historia yao ya TANU imeanza mwaka wa 1954 na Nyerere na kwa makusudi wakafuta historia ya Abdul Sykes.
Historia ya Mohamed Said inaanza na Kleist 1929 na kuendelea na Abdul 1950.
Hapa ndipo nilipovutia wanafunzi wa African History na historia hii ikamgusa Mwalimu Nyerere na hili ni jina kubwa sana.
Kitabu kilipotoka kiliwastua watu wengi sana kwani mengi waliyokutananayo ndani ya kitabu cha Abdul Sykes walikuwa hawajapata kuyasikia na kubwa zaidi lililowapa tabu ni mchango wa Waislam katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Tusimame hapa.
Sir...Aende akawaulize wakiwa hai hataki anasubiri mpaka wafe,unfortunately siku wakitutoka Mzee Mwinyi au Dk Jakaya tuyategemee haya yakitokea laah haijawa hivi basi zitakuwa zimewabeba imani zao coz huyu ataandika anavyoandika but akiwa ni mrengo anaoamini yeye hutamuona akiwazungumzia vibaya wahusika kasheshe uwe upande wa pili basi utajuta.
James...I think, this is the agenda. MS hakuna anayebisha ushiriki wa mtu mmoja mmoja ktk Uhuru wa Tanganyika. Inshu kubwa hapa Nguruvi aliipambanua ni wewe kumpa jina baya Nyerere!
Asante.James...
Kuna mambo inaelekea huyajui katika uandishi wa historia ya.TANU.
Mimi nimeanza kuandika historia hii kuanzia mwaka wa 1929.
Nyerere hayuko Dar es Salaam.
Nimemtia Abdul Sykes katika historia ya TANU 1942 wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia yuko Burma 6th Battalion na yuko Kalieni Camp Bombay mwaka wa 1945 baada ya vita kumalizika.
Abdul hajafahamiana na Nyerere.
Nimemtia Abdul katika historia ya TANU mwaka wa 1950 sasa yuko Dar es Salaam.
Nimewatia Abdul na Nyerere katika historia ya TANU mwaka wa 1952 baada ya hawa wawili kufahamiana.
Kama kuijua TANU basi Mwalimu hapa ndipo alipojua kuwa ipo mipango ya kuunda chama cha siasa.
Sasa mimi niwazulie watu maneno kwa kutafuta nini?
Haya yote yanafanyika babu ya na baba yangu wako Mtaa wa Kipata jirani na nyumba ya Kleist Sykes na baba yangu na Abdul wanasoma shule moja darasa moja Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Muslim School.
Wala simlazimishi yeyote kuamini niliyoandika katika.kitabu cha Abdul Sykes.
James...Asante.
Mzee Mohamedi niseme kwanza ni kweli mengi siyajui na kiukweli huwa ninajitajidi kufatilia maandiko yako humu. Lakini kuna vitu vinabangua bongo zangu. Nguruvi ameuliza juu ya kupokelewa Nyerere na Sykes ? Kuwa umempa jina baya Nyerere kwanini useme alipokelewa na Sykes wakati alifundisha Pugu siku nyingi ?
Hapa mtu anaweza kusema vile vile kama ulivyosema kwa Mkapa kuwa mwandishi nguli wa historian ya Tanganyika usingeweza kusahau taarifa muhimu kama hiyo juu ya rais wa kwanza wa Tanzania kwa kuwa wewe siyo zuzu.
Au kubali kuwa ulifanya kosa
MS kama akibadilisha mrengo wa maandishi yake atapata recognition kubwa sana.... lakini kwasababu yuko kwenye mission ya kupush ajenda ngoja tuone ..... mi nashangaa kweli ilikuwaje tena Mkapa akaja kwenye ajenda hizi.... au ndio kutafuta uhalali wa ajenda zenyeweTumefika huku kote kwa sababu ya Mzee Said. Laiti kama angezileta hizi historia za Wazee hawa bila ajenda fiche kila kitu kingebaki sawa.
Kila Mtu abaki na heshima yake kwa mchango wake lakini kamwe mambo yasipindishwe maana yanaibua hasira za wengine.
James...
Mimi si mtu wa ubishi kwani ubishi haujengi mjadala bali unabomoa.
Hivi kwa nini wewe ushughulishwe na jambo la kupokelewa?
Kwani lina kipi kikubwa sana?
Kubwa kwa Nyerere wakati ule ni yeye kupelekwa na kujulishwa kwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na Abdul Sykes.
Hili ndilo kubwa katika historia ya Nyerere.
Matu...MS kama akibadilisha mrengo wa maandishi yake atapata recognition kubwa sana.... lakini kwasababu yuko kwenye mission ya kupush ajenda ngoja tuone ..... mi nashangaa kweli ilikuwaje tena Mkapa akaja kwenye ajenda hizi.... au ndio kutafuta uhalali wa ajenda zenyewe
Muheshimiwa una ujasiri mzuri wa kuhoji japo intention yako sijajua, isije kuwa ndio hidden agenda kama anayotuhumiwa Mohamed said ya kutetea dini yake "jambo ambalo sioni ubaya wake". Hivi kweli hushangazwi na ziada ya majibu ya bwana mohMohamed ukiulizwa kitu unajibu ulichoulizwa. Nadhani hili halina shida labda kama tunalifanya shida bila sababu
Ukiniuliza, Abdul Sykes alikuwa mtoto wa Kleist? Jibu langu ni ndiyo au hapana kutegemeana
Ukiniuliza Sheikh Chambera anafahamiana na Abdul Sykes? Nitakujibu sijui au najua abcd
Nitakuwa wa ajabu kidogo ukiniuliza habari za Sheikh Chambera na Abdul halafu nikakuletea maelezo mengi na marefu ya uhusiano wa Chambera na Nyerere na alivyokwenda Lindi baada ya mwaliko.
Umeona kwanini ninashangaa? Mfano mzuri huu hapa. Mimi sijahoji source ya taarifa zako na kwamba zimepatikana wapi.
Nilichokihoji ni kitu kimoja, niwapi na ni lini Abdul Sykes alihutubia mkutano nje ya Tandamti na Kipata? Sijauliza aliwahi kusafiri kwenda wapi kumbuka hilo
Nikauliza, kadi ya Kleist Sykes ya AA ilikuwa namba ngapi? Sijauliza special branch wanasemaje
Nikauliza kadi ya Abdul Sykes ya TAA ilikuwa namba ngapi? Sijauliza special branch wanasemaje
Nimeuliza haya kwasababu wewe umebahatika kusoma makabrasha kwa mujibu wako.
Halafu nikauliza, kama TANU iliundwa 1929 na Familia ya Sykes na nadhani Nyerere alikuwa na miaka 7 Butiama, iweje basi kadi yake ya TANU iwe namba 1 na Abdul Namba 3.Sawa sawa wanatoka Ulaya, sisi ni wa hapa nyumbani na unaweza kuwatumia kutusaidia ndio maana tunahitaji ufahamu.
Kutokujua haijawa dhambi au kosa lakini kutotaka kujua au kujua kwa kububusa ni hatari kuliko kutojua.
Tuache ya Ulaya tuendelee na mnakashaHakuna aliyeyahitaji.Hapana sina husda kabisa na sina sababu za kuwa na husda, nina sababu za kukemea husdaHapana si kwenu, ni mnakasha tu. Sifa moja ya usomi ni uvumilivu wa kazi unazofanya. ukishajipambanua kama mwana historia basi daraja lako ni la juu, lakini pia daraja hilo haliji bila chujio.
Na si wote tunaoweza kumeza bila kutafuna, la hasha! si wote tunaovumilia kusikia mpapai unazaa maembe. Tutauliza, umepandikizwa ? na kwa njia gani maana chungwa na limao ni ndugu! Hapana usiwe na shaka hawezi kufutwa, mbona umejitahidi kumdunisha na kumdhalilisha Nyerere lakini kila siku anazungumzwa? Hata wangeungana woote wa Mzimama kila mmoja ana nafasi yake, na hili la husda dhidi ya Mwalimu linakera. Najiuliza hivi husda dhidi ya Nyerere ni kwa lipi?
Hii mada si ya Mkapa, Marehemu ametumika kama daraja.
mlengwa hapa ni mzee mla Mayai kwa Sykes, Mwl Nyerere! Kambarage anayekwenda sokoni bila pesa
Ni sawa na kuhoji kuonekana kwa Philip mangula majukwaani ili kuvunja hoja ya anae eleze umashuhuri wake kwenye siasa kwa miongo hii, kisha badae ukaja kuwapa mfano wa bashiru Ally kakulwa anavyo spit majukwaaniWanajamvi, hapa MS anasema ameandika historia ya Wazee wake. Hilo si tatizo kabisa na ni haki yake na awaye akitaka naye pia atende.
Mohamed anasema hakuandika historia ya Watu wa Tanganyika, bali sehemu ya watu ambao ni wazee wake.
Sina shaka ulizisoma zote na hakuna mahali ulipata ushahidi wa uwepo wa katiba ya AA au TAA.
Je, kadi ya uanachama ya Kleist ya AA 1929 ilikuwa namba ngapi?
Je, kadi ya uanachama wa Abdul Sykes ya TAA ilikuwa namba ngapi?
Umetueleza kadi ya Abdul ya TANU ni Namba 3, Nyerere ni 1. Jitihada za kum-sideline Nyerere zinaanza.
MS anaonyesha kuwa TANU iliundwa na Familia ya Sykes.
Ukweli ni kuwa TANU iliundwa na watu wengi akiwemo Nyerere.
Kama Nyerere hakuwepo Mohamed thibitisha
Lakini pia ni makosa kusema Familia ya Sykes iliyoingia nchini kama Mamluki wa kupigania na si kupinga ukoloni ilipigania Uhuru. Tunaweza kuona haya kwa ushahidi kuwa hakuna mahali popote Abdul Sykes au baba yake Kleist walikwenda mikoani kwa shughuli za siasa ukiacha Tandamti, Agrey , New street na kidongo chekundu. Well, nyaraka nyingi zinamusu Nyerere wakati akisambaza TANU.Huenda Mohamed ukawa na nyaraka za Kleist na Abdul Sykes mikoani, na hilo lingetufariji tukiziona
Mkwavingwa,Muheshimiwa una ujasiri mzuri wa kuhoji japo intention yako sijajua, isije kuwa ndio hidden agenda kama anayotuhumiwa Mohamed said ya kutetea dini yake "jambo ambalo sioni ubaya wake". Hivi kweli hushangazwi na ziada ya majibu ya bwana moh
Mokaze,
Angalia hiyo hapo chini:
file:///C:/Users/Administrator/Pictures/KLEIST%20SYKES%20DICTIONARY%20OF%20AFRICAN%20BIOGRAPHY.pdf_RFd14c353.TMP
Lakini naona ni prestige kwako kwani mijadala yako ni ya wazi na huwafokei kama namna ya wao wakufokeavyo kiasi unatambua kabisa wamekasilishwa either na ukweli au jingeneMkwavingwa,
Tatizo ni kuwa namna yangu ya kujibu maswali ni kuongeza mengi ambayo wao hawayajui.
Hiki kitu kinawapa sana shida wangependa nijibu swali kwa namna ya wao majibu yangu tayari wanayo vichwani mwao.
Lakini naona ni prestige kwako kwani mijadala yako ni ya wazi na huwafokei kama namna ya wao wakufokeavyo kiasi unatambua kabisa wamekasilishwa either na ukweli au jingeneMkwavingwa,
Tatizo ni kuwa namna yangu ya kujibu maswali ni kuongeza mengi ambayo wao hawayajui.
Hiki kitu kinawapa sana shida wangependa nijibu swali kwa namna ya wao majibu yangu tayari wanayo vichwani mwao.
Mkwaviga,Lakini naona ni prestige kwako kwani mijadala yako ni ya wazi na huwafokei kama namna ya wao wakufokeavyo kiasi unatambua kabisa wamekasilishwa either na ukweli au jingene