Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?

Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?

Hata Yesu alilia na kulalamika msalabani:- Eloi Eloi lamasabchtan.

Yaani; Ewe Mungu, ewe Mungu mbona waniacha.

Kama Yesu pamoja na utukufu na ukubwa wake wote alimlilia Mungu, vipi mimi mtu hohehahe nishindwe kulia???!!!.
Mokaze,
Angalia hiyo hapo chini:

file:///C:/Users/Administrator/Pictures/KLEIST%20SYKES%20DICTIONARY%20OF%20AFRICAN%20BIOGRAPHY.pdf_RFd14c353.TMP
 
Kwa hiyo kwako wewe kipimo cha mtu kuijua historia kwa usahihi kuhusu miaka ya mwanzo ya Mwl Nyerere hapo Dar ni kuzaliwa na kukulia Dar sivyo?kuna watu wakiandika kumuhusu Nyerere kabla hata huyo mtoto wa Abdul hajazaliwa na tena amekiri wazi kwa maandishi akisema “KATIKA AKILI ZANGU ZA KITOTO”,so unapotaka wote kutubeba kwenye kapu moja kuamini kila kinachoandikwa na mtu ni sahihi jipime vizuri uelewa wako.

Kwa maneno yake mwenyewe mzee Said hapo juu amesema “Mwl Nyerere alikaa kwa Abdul miezi mitatu tu” so wa mikoani au wageni wa Dar tuamini kwamba harakati zote za Mwalimu kudai uhuru wa kitaifa alizifanya akiwa Butiama ila akaja kufanikiwa alipopata hifadhi ya miezi mitatu kwa Abdul?mkuu haupo na wajukuu zako sebuleni kwako ukiwapa hadithi hapa upo na watu wazima wanaochakata vizuri bongo zao kukubali wanachoambiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna siku kuna mtu aliuliza kwa nini watu kama Maria Nyerere wasiulizwe kama kunakuwa na utata wa baadhi ya matukio? Hii mada ilisubiri mpaka watajwa wafe?
Siku akifa Maria Nyerere tena atawekewa maneno maneno mdomoni. Nafkiri kuna haja ya kuyaweka haya mambo bayana kabla baadhi ya watu hawajafa. Naona Mzee Saidi anakichaka cha kujificha kuendesha agenda zake.
 
Aende akawaulize wakiwa hai hataki anasubiri mpaka wafe,unfortunately siku wakitutoka Mzee Mwinyi au Dk Jakaya tuyategemee haya yakitokea laah haijawa hivi basi zitakuwa zimewabeba imani zao coz huyu ataandika anavyoandika but akiwa ni mrengo anaoamini yeye hutamuona akiwazungumzia vibaya wahusika kasheshe uwe upande wa pili basi utajuta.
 
James...
Kuna mambo inaelekea huyajui katika uandishi wa historia ya.TANU.

Mimi nimeanza kuandika historia hii kuanzia mwaka wa 1929.

Nyerere hayuko Dar es Salaam.

Nimemtia Abdul Sykes katika historia ya TANU 1942 wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia yuko Burma 6th Battalion na yuko Kalieni Camp Bombay mwaka wa 1945 baada ya vita kumalizika.

Abdul hajafahamiana na Nyerere.

Nimemtia Abdul katika historia ya TANU mwaka wa 1950 sasa yuko Dar es Salaam.

Nimewatia Abdul na Nyerere katika historia ya TANU mwaka wa 1952 baada ya hawa wawili kufahamiana.

Kama kuijua TANU basi Mwalimu hapa ndipo alipojua kuwa ipo mipango ya kuunda chama cha siasa.

Sasa mimi niwazulie watu maneno kwa kutafuta nini?

Haya yote yanafanyika babu ya na baba yangu wako Mtaa wa Kipata jirani na nyumba ya Kleist Sykes na baba yangu na Abdul wanasoma shule moja darasa moja Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Muslim School.

Wala simlazimishi yeyote kuamini niliyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes.
 
Mokaze,
Kuna mengi najizuia kuyasema kwa kuchelea isionekane mie nimeghadhibishwa na hizi "provocations."

Chuo Cha CCM Kivukoni walitamani sana kuanza historia ya TANU na Julius Nyerere na wakafanya hivyo wakiamini kuwa historia hiyo itasimama.

Kitabu kikatoka mwaka wa 1981.

Kwa hakika kitabu hiki ni kichekesho na hawajaweza kuchapa toleo jingine la pili.

Hakuna mhadhiri yeyote Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Idara ya Historia anaefanya rejea ya kitabu hiki kwa wanafunzi wake.

Mimi nikaamua kukijibu kitabu hiki kwa namna nyingine na yenye ushahidi ambao Kivukoni hawataweza kuupata popote.

Nikaamua kutumia "biographical approach," yaani kuiandika historia ya TANU kupitia maisha ya viongozi wa African Association na TANU.

Hapa ndipo pagumu sana kwa yeyote ambae ana hamu ya kunipinga.

Tayari nilikuwa na mswada wa Kleist alioandika mwenyewe kwa mkono wake kabla hajafa mwaka wa 1949.

Mswada huu nimeshaueleza mara nyingi hapa jamvini ni mashuhuri.

Historia ya vipi yeye Kleist alihusika kama katibu katika kuunda African Association imo ndani ya mswada.

1950 Abdul Sykes akachukua uongozi wa TAA mwaka mmoja baada ya kifo cha baba yake.

Hapa napo nikawa na Nyraka za Sykes kila kitu kimo humo.

Utaona hapa baba na mwanae wote wamehusika na mwamko huu wa Waafrika wa Tanganyika kujitambua kati ya 1929 hadi uhuru unapatikana 1961.

Kivukoni wao kwa bahati mbaya sana historia yao ya TANU imeanza mwaka wa 1954 na Nyerere na kwa makusudi wakafuta historia ya Abdul Sykes.

Historia ya Mohamed Said inaanza na Kleist 1929 na kuendelea na Abdul 1950.

Hapa ndipo nilipovutia wanafunzi wa African History na historia hii ikamgusa Mwalimu Nyerere na hili ni jina kubwa sana.

Kitabu kilipotoka kiliwastua watu wengi sana kwani mengi waliyokutananayo ndani ya kitabu cha Abdul Sykes walikuwa hawajapata kuyasikia na kubwa zaidi lililowapa tabu ni mchango wa Waislam katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Tusimame hapa.
I think, this is the agenda. MS hakuna anayebisha ushiriki wa mtu mmoja mmoja ktk Uhuru wa Tanganyika. Inshu kubwa hapa Nguruvi aliipambanua ni wewe kumpa jina baya Nyerere!
 
Aende akawaulize wakiwa hai hataki anasubiri mpaka wafe,unfortunately siku wakitutoka Mzee Mwinyi au Dk Jakaya tuyategemee haya yakitokea laah haijawa hivi basi zitakuwa zimewabeba imani zao coz huyu ataandika anavyoandika but akiwa ni mrengo anaoamini yeye hutamuona akiwazungumzia vibaya wahusika kasheshe uwe upande wa pili basi utajuta.
Sir...
Fanya staha.

Mama Maria hakuna haja ya kumuingiza katika kuitafuta historia ya TANU.

Ikiwa kama yeye mwenyewe anapenda kukumbuka historia ya siku za mwanzo walipofahamiana na Abdul Sykes, Mama Daisy, Bi. Chiku bint Said Kikusa na wanae Bi. Sakina na Bi. Fatna ataeleza.
 
I think, this is the agenda. MS hakuna anayebisha ushiriki wa mtu mmoja mmoja ktk Uhuru wa Tanganyika. Inshu kubwa hapa Nguruvi aliipambanua ni wewe kumpa jina baya Nyerere!
James...
Wahariri wasingethubutu kuniachia nimpe Nyerere, "jina baya."

Hiki kitabu walishakiona umuhimu wake, "as corrective history."

Kitabu kinasahihisha history ya uhuru wa Tangamyika kitasomwa na kufundishwa vyuo vikuu.

Kuandika upuuzi kitaua kitabu chao.
 
James...
Kuna mambo inaelekea huyajui katika uandishi wa historia ya.TANU.

Mimi nimeanza kuandika historia hii kuanzia mwaka wa 1929.

Nyerere hayuko Dar es Salaam.

Nimemtia Abdul Sykes katika historia ya TANU 1942 wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia yuko Burma 6th Battalion na yuko Kalieni Camp Bombay mwaka wa 1945 baada ya vita kumalizika.

Abdul hajafahamiana na Nyerere.

Nimemtia Abdul katika historia ya TANU mwaka wa 1950 sasa yuko Dar es Salaam.

Nimewatia Abdul na Nyerere katika historia ya TANU mwaka wa 1952 baada ya hawa wawili kufahamiana.

Kama kuijua TANU basi Mwalimu hapa ndipo alipojua kuwa ipo mipango ya kuunda chama cha siasa.

Sasa mimi niwazulie watu maneno kwa kutafuta nini?

Haya yote yanafanyika babu ya na baba yangu wako Mtaa wa Kipata jirani na nyumba ya Kleist Sykes na baba yangu na Abdul wanasoma shule moja darasa moja Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Muslim School.

Wala simlazimishi yeyote kuamini niliyoandika katika.kitabu cha Abdul Sykes.
Asante.
Mzee Mohamedi niseme kwanza ni kweli mengi siyajui na kiukweli huwa ninajitajidi kufatilia maandiko yako humu. Lakini kuna vitu vinabangua bongo zangu. Nguruvi ameuliza juu ya kupokelewa Nyerere na Sykes ? Kuwa umempa jina baya Nyerere kwanini useme alipokelewa na Sykes wakati alifundisha Pugu siku nyingi ?

Hapa mtu anaweza kusema vile vile kama ulivyosema kwa Mkapa kuwa mwandishi nguli wa historian ya Tanganyika usingeweza kusahau taarifa muhimu kama hiyo juu ya rais wa kwanza wa Tanzania kwa kuwa wewe siyo zuzu.
Au kubali kuwa ulifanya kosa
 
Mimi si mtu wa ubishi kwani ubishi haujengi mjadala bali unabomoa.

Hivi kwa nini wewe ushughulishwe na jambo la kupokelewa?

Kwani lina kipi kikubwa sana?

Kubwa kwa Nyerere wakati ule ni yeye kupelekwa na kujulishwa kwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na Abdul Sykes.

Hili ndilo kubwa katika historia ya Nyerere.
 
Tumefika huku kote kwa sababu ya Mzee Said. Laiti kama angezileta hizi historia za Wazee hawa bila ajenda fiche kila kitu kingebaki sawa.

Kila Mtu abaki na heshima yake kwa mchango wake lakini kamwe mambo yasipindishwe maana yanaibua hasira za wengine.
MS kama akibadilisha mrengo wa maandishi yake atapata recognition kubwa sana.... lakini kwasababu yuko kwenye mission ya kupush ajenda ngoja tuone ..... mi nashangaa kweli ilikuwaje tena Mkapa akaja kwenye ajenda hizi.... au ndio kutafuta uhalali wa ajenda zenyewe
 
James...
Mimi si mtu wa ubishi kwani ubishi haujengi mjadala bali unabomoa.

Hivi kwa nini wewe ushughulishwe na jambo la kupokelewa?

Kwani lina kipi kikubwa sana?

Kubwa kwa Nyerere wakati ule ni yeye kupelekwa na kujulishwa kwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na Abdul Sykes.

Hili ndilo kubwa katika historia ya Nyerere.

Mwezi October 1999 nilikuwa Dubai na nikikaa Carlton Hotel.

Siku moja jioni simu yangu ikalia.

Walikuwa BBC London Idhaa ya Kiswahili wanataka kunihoji kuhusu Mwalimu Julius Nyerere ambae wakati ule alikuwa amelazwa St. Thomas Hospital, London.

Ulikuwa mwaka wa pili toka kitabu changu, ‘’The Life and Times of Abdulwaid Sykes (1924- 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,’’ kichapwe na kitabu hiki kikawa kimenifanya nifahamike na sababu kubwa ni kuwa kilikuja na historia mpya ya yeye Mwalimu Nyerere mwenyewe, historia ya TANU na historia nzima ya kudai uhuru wa Tanganyika.

Kitabu kilimweeleza Mwalimu Nyerere kwa namna ambayo hakuna mwandishi alipatapo kufanya hivyo.

Hii nadhani ndiyo ikawa sababu ya BBC kutaka kunisikia nikimzungumza Mwalimu Nyerere.

BBC wakawa wanataka tuzungumze kidogo kuhusu Mwalimu na jinsi Watanzania walivyoathirika na ile hali ya Mwalimu kuwa kwenye matibabu Uingereza.

Katika kipindi kile cha maradhi ya Mwalimu akiwa hospitali kila siku habari ya hali yake ilikuwa inatolewa na kwa kweli sote tukifuatilia kwa karibu sana hadi pale alipofariki tarehe 14 Oktoba 1999.

Kishindo chake kilikuwa kikubwa hakijapatapo kutokea na mazishi ya Mwalimu hayapata kutokea halikadhalika simanzi iliyoonyeshwa na Watanzania haijapatapo kutokea.

Umma mkubwa usio na kifani ulijitokeza kupokea jeneza lake Uwanja wa Ndege na maelfu ya watu walijipanga pembeni ya barabara kutoa heshima zao wakati jeneza lake lilipokuwa linapita kuelekea nyumbani kwake Msasani.

Mimi nilikuwa Tanga nikifuatilia kwenye TV na binafsi fikra nyingi zilipita katika kichwa changu.

Mimi sikupata kujuana na Mwalimu lakini katika utafiti wangu wa maisha ya Abdul Sykes na harakati za uhuru nimemjua kwa karibu Mwalimu Nyerere kushinda wale waliokuja kuwa karibu na yeye baada ya uhuru.

Katika utafiti nimekutana na Mwalimu Nyerere ndani ya Nyaraka za Sykes na ndani ya nyaraka hizi nimesoma barua zake akiwa Rais wa TAA na kisha TANU katika miaka ya mwanzoni ya 1950, nimezungumza na Ally Sykes na Dossa Aziz na Mama Daisy (mke wa Abdul Sykes) watu waliokuwanae toka siku ya kwanza wanaanza mapambano ya kudai uhuru.

Katika mikoa ya Tanzania nilikokwenda kwa utafiti nimekutana na kuzungumza na watu waliokuwanae bega kwa bega katika siku hizo za mwanzo wakati Mwalimu Nyerere ndiyo anaanza harakati za kudai uhuru wa Tanganyika akiwa kijana wa miaka 30.

Wakati naangalia TV usiku mmoja wakionyesha ndege ya Air Tanzania Corporation (ATC) iliyokwenda kuchukua mwili wa Mwalimu Nyerere London camera ikapita kwa Abbas Sykes kwa haraka lakini nilimtambua bila wasiwasi wowote kuwa ndiye yeye.

Wakati ule yeye alikuwa ndiye Mwenyekiti wa ATC nafasi aliyoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa.

Nilikuwa na kawaida kila nikija Dar es Salaam kutoka Tanga lazima nipite ofisini kwa Bwana Ally Sykes kumjulia hali kisha niende nyumbani kwa Balozi Abbas Sykes.

Safari hii nilikwenda kwa Balozi Sykes kwa nia khasa ya kutaka kujua safari yake ya London kwenda kuchukua mwili wa Mwalimu Nyerere.

Bwana Abbas tukiwa mimi nimekaa kwenye kiti changu ninachokipenda ndani ya ukumbi wake, kiti ambacho kinanipa mandhari ya mchanga mweupe wa bahari na bahari yenyewe na yeye kama kawaida amekaa kwenye kiti cha baba mwenye nyumba kwani huwa siku zote ndicho kiti chake nilianza mazungumzo kwa kumpa pole kwa msiba wa Mwalimu Nyerere.

Balozi Sykes akaitikia ile pole yangu kisha akasema, ‘’Unajua mimi kama Mwenyekiti wa ATC nilitiwa katika msafara wa kwenda kuuchukua mwili wa Nyerere.

Ingekuwa si hii nafasi yangu ya uenyekiti nisingepata fursa na heshima ile kwani hawa viongozi walioko madarakani hawajui kuwa Nyerere sisi ni ndugu yetu.’’

Nilijua bila ya kuuliza kuwa ile, ‘’sisi,’’ Balozi alikusudia wao Sykes Brothers.

Nilikuwa sijapatapo kumsikia Bwana Abbas akijinasibisha udugu na Nyerere.

Mara zote alipokuwa akieleza harakati za kudai uhuru alikuwa akimweleza Nyerere katika nafasi ya urafiki wake na kaka yake Abdul na kama kiongozi wa TANU, hili la udugu ndiyo siku ile nalisikia kwa mara ya kwanza.

‘’Mimi nimejaaliwa kumuona Nyerere siku ya kwanza kaja kwetu pale Mtaa wa Stanley na Sikukuu kaja kumuona Bwana Abdul akiwa kaongozana na Joseph Kasella Bantu na kuanzia hapo tukawa kama ndugu mama yake Bi. Mugaya akafahamiana na mama yetu na akawa anamtembelea mama nyumbani kwake pamoja na Sophia dada yake Nyerere.

Nikajuana na Joseph mdogo wake na Mama Maria Nyerere ambae alikuja kuwa shoga mkubwa wa Mama Daisy.’’

Bwana Abbas alipomaliza utangulizi huu na hapa alinistua kwani ingawa vifo siku zote vinatokea lakini huwa hatupendi kusikia vile vitu vya karibu vinavyomgusa maiti kama jeneza sanda na kadhalika.

Bwana Abbas akanieleza hali ilivyokuwa ndani ya ndege, ‘’Mohamed Nyerere nimejuananae kuanzia mwaka wa 1952 mimi kijana wa miaka 23 mdogo sana hata Bwana Abdul alikuwa mdogo kwa Nyerere.

Ndani ya ndege tuliweka sanduku lililokuwa na mwili wake mbele kabisa tumelifunika na bendera ya Tanzania.

Ilikuwa tabu sana kwangu kukwepa kulitazama sanduku lile lenye mwili wa Nyerere.

Kila mara fikra zinakwenda mbele na kurudi nyuma zinakwenda mbele zinarudi nyuma namkumbuka Nyerere kijana na Bwana Abdul kijana wote vijana wako pale nyumbani kipindi kile ameacha kazi na siku za mwanzo za TANU.

Endapo mtu angelinambia kwa wakati ule kuwa Nyerere atakuja kuwa kiongozi mkubwa barani Afrika ingekuwa tabu kwangu kuamini kuwa mambo yale waliyokuwa wanayanzungumza wakipanga na kupangua yatakuja kuwa makubwa kwa kiasi kile kilichofikia.

Nimekuwa na Nyerere kwingi Ulaya katika mikutano na nimeshuhudia kwa macho yangu viongozi wenzake na watu maarufu duniani wanavyokuwa wakiwa mbele yake.

Kwangu mimi ile ilikuwa historia inafunguka mbele ya macho yangu ya mtu niliyemuona akitembea kwa miguu mitaa ya Gerezani akiwa na mimi au na Bwana Abdul wakienda kumuona huyu au yule.
 
MS kama akibadilisha mrengo wa maandishi yake atapata recognition kubwa sana.... lakini kwasababu yuko kwenye mission ya kupush ajenda ngoja tuone ..... mi nashangaa kweli ilikuwaje tena Mkapa akaja kwenye ajenda hizi.... au ndio kutafuta uhalali wa ajenda zenyewe
Matu...
Umeeleza sivyo ungeniuliza kama nimepata ''recognition,'' nikuambie kuwa sijapata ndiyo unipe ushauri uliokusudia.
''Recogntion,'' nimepata.

Mkapa kaingia kwa kuwa baada ya kufa Abdul Sykes kukawa katika duru za rafiki zake masikitiko jinsi magazeti ya TANU yalivyoshindwa kumuadhimisha Abdul Sykes.

Mhariri wa magazeti yake alikuwa Benjamin Mkapa kwa hiyo lawama zote zikaelekezwa kwake.

Ndipo katika kuandika taazia yake nikauliza vipi Mkapa alishindwa kuchapa taazia ya Abdul Sykes katika ''The Nationalist?''
 
Mohamed ukiulizwa kitu unajibu ulichoulizwa. Nadhani hili halina shida labda kama tunalifanya shida bila sababu

Ukiniuliza, Abdul Sykes alikuwa mtoto wa Kleist? Jibu langu ni ndiyo au hapana kutegemeana
Ukiniuliza Sheikh Chambera anafahamiana na Abdul Sykes? Nitakujibu sijui au najua abcd

Nitakuwa wa ajabu kidogo ukiniuliza habari za Sheikh Chambera na Abdul halafu nikakuletea maelezo mengi na marefu ya uhusiano wa Chambera na Nyerere na alivyokwenda Lindi baada ya mwaliko.

Umeona kwanini ninashangaa? Mfano mzuri huu hapa. Mimi sijahoji source ya taarifa zako na kwamba zimepatikana wapi.
Nilichokihoji ni kitu kimoja, niwapi na ni lini Abdul Sykes alihutubia mkutano nje ya Tandamti na Kipata? Sijauliza aliwahi kusafiri kwenda wapi kumbuka hilo

Nikauliza, kadi ya Kleist Sykes ya AA ilikuwa namba ngapi? Sijauliza special branch wanasemaje
Nikauliza kadi ya Abdul Sykes ya TAA ilikuwa namba ngapi? Sijauliza special branch wanasemaje

Nimeuliza haya kwasababu wewe umebahatika kusoma makabrasha kwa mujibu wako.

Halafu nikauliza, kama TANU iliundwa 1929 na Familia ya Sykes na nadhani Nyerere alikuwa na miaka 7 Butiama, iweje basi kadi yake ya TANU iwe namba 1 na Abdul Namba 3.Sawa sawa wanatoka Ulaya, sisi ni wa hapa nyumbani na unaweza kuwatumia kutusaidia ndio maana tunahitaji ufahamu.
Kutokujua haijawa dhambi au kosa lakini kutotaka kujua au kujua kwa kububusa ni hatari kuliko kutojua.
Tuache ya Ulaya tuendelee na mnakashaHakuna aliyeyahitaji.Hapana sina husda kabisa na sina sababu za kuwa na husda, nina sababu za kukemea husdaHapana si kwenu, ni mnakasha tu. Sifa moja ya usomi ni uvumilivu wa kazi unazofanya. ukishajipambanua kama mwana historia basi daraja lako ni la juu, lakini pia daraja hilo haliji bila chujio.

Na si wote tunaoweza kumeza bila kutafuna, la hasha! si wote tunaovumilia kusikia mpapai unazaa maembe. Tutauliza, umepandikizwa ? na kwa njia gani maana chungwa na limao ni ndugu! Hapana usiwe na shaka hawezi kufutwa, mbona umejitahidi kumdunisha na kumdhalilisha Nyerere lakini kila siku anazungumzwa? Hata wangeungana woote wa Mzimama kila mmoja ana nafasi yake, na hili la husda dhidi ya Mwalimu linakera. Najiuliza hivi husda dhidi ya Nyerere ni kwa lipi?

Hii mada si ya Mkapa, Marehemu ametumika kama daraja.

mlengwa hapa ni mzee mla Mayai kwa Sykes, Mwl Nyerere! Kambarage anayekwenda sokoni bila pesa
Muheshimiwa una ujasiri mzuri wa kuhoji japo intention yako sijajua, isije kuwa ndio hidden agenda kama anayotuhumiwa Mohamed said ya kutetea dini yake "jambo ambalo sioni ubaya wake". Hivi kweli hushangazwi na ziada ya majibu ya bwana moh
 
Wanajamvi, hapa MS anasema ameandika historia ya Wazee wake. Hilo si tatizo kabisa na ni haki yake na awaye akitaka naye pia atende.
Mohamed anasema hakuandika historia ya Watu wa Tanganyika, bali sehemu ya watu ambao ni wazee wake.
Sina shaka ulizisoma zote na hakuna mahali ulipata ushahidi wa uwepo wa katiba ya AA au TAA.

Je, kadi ya uanachama ya Kleist ya AA 1929 ilikuwa namba ngapi?
Je, kadi ya uanachama wa Abdul Sykes ya TAA ilikuwa namba ngapi?
Umetueleza kadi ya Abdul ya TANU ni Namba 3, Nyerere ni 1. Jitihada za kum-sideline Nyerere zinaanza.
MS anaonyesha kuwa TANU iliundwa na Familia ya Sykes.
Ukweli ni kuwa TANU iliundwa na watu wengi akiwemo Nyerere.
Kama Nyerere hakuwepo Mohamed thibitisha

Lakini pia ni makosa kusema Familia ya Sykes iliyoingia nchini kama Mamluki wa kupigania na si kupinga ukoloni ilipigania Uhuru. Tunaweza kuona haya kwa ushahidi kuwa hakuna mahali popote Abdul Sykes au baba yake Kleist walikwenda mikoani kwa shughuli za siasa ukiacha Tandamti, Agrey , New street na kidongo chekundu. Well, nyaraka nyingi zinamusu Nyerere wakati akisambaza TANU.Huenda Mohamed ukawa na nyaraka za Kleist na Abdul Sykes mikoani, na hilo lingetufariji tukiziona
Ni sawa na kuhoji kuonekana kwa Philip mangula majukwaani ili kuvunja hoja ya anae eleze umashuhuri wake kwenye siasa kwa miongo hii, kisha badae ukaja kuwapa mfano wa bashiru Ally kakulwa anavyo spit majukwaani
 
Muheshimiwa una ujasiri mzuri wa kuhoji japo intention yako sijajua, isije kuwa ndio hidden agenda kama anayotuhumiwa Mohamed said ya kutetea dini yake "jambo ambalo sioni ubaya wake". Hivi kweli hushangazwi na ziada ya majibu ya bwana moh
Mkwavingwa,
Tatizo ni kuwa namna yangu ya kujibu maswali ni kuongeza mengi ambayo wao hawayajui.

Hiki kitu kinawapa sana shida wangependa nijibu swali kwa namna ya wao majibu yangu tayari wanayo vichwani mwao.
 
Mokaze,
Angalia hiyo hapo chini:

file:///C:/Users/Administrator/Pictures/KLEIST%20SYKES%20DICTIONARY%20OF%20AFRICAN%20BIOGRAPHY.pdf_RFd14c353.TMP

Shukrani mkuu, lakini kwenye Cm yangu hiyo link haifunguki.
 
Mkwavingwa,
Tatizo ni kuwa namna yangu ya kujibu maswali ni kuongeza mengi ambayo wao hawayajui.

Hiki kitu kinawapa sana shida wangependa nijibu swali kwa namna ya wao majibu yangu tayari wanayo vichwani mwao.
Lakini naona ni prestige kwako kwani mijadala yako ni ya wazi na huwafokei kama namna ya wao wakufokeavyo kiasi unatambua kabisa wamekasilishwa either na ukweli au jingene
 
Mkwaviga,
Tatizo ni hili.

Uhuru ulipokuwa unakaribia kupatikana baada ya Uchaguzi wa Kura Tatu mwaka wa 1958, waliingia katika TANU watu wengi wapya na katika hawa wako waliokuja kushika nafasi za uongozi katika chama na wengine kushika nafasi za juu katika serikali iliyokuwa inaongozwa na Nyerere.

Kundi hili halikuwa linajua historia ya TANU na lilianza kuwapiga vita wale waliowakuta katika chama.

Tatizo hapa ndipo lilipoanza.

TANU haikuwa tena inahitaji msaada ule uliokuwa ukipokea kwa watu kama Abdul, Dossa, Rupia na wengine.
 
Back
Top Bottom