Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?

"Mohamed Said, post: 36197768, member: 12431"]
Nguruvi...
Watu wote wanaijua historia hii kuwa Abdul ndiye aliyempokea Nyerere na wala mimi sijabadilisha kauli yangu.
Mohamed hili ni jibu la kijiweni, halina chembe ya weledi achilia mbali usomi.
Watu wote ni akina nani?
Tueleze Abdul Sykes alimpokea Nyerere akitokea wapi na lini. Hapa ndipo unatakiwa utetee hoja.
La ikiwa nyinyi mnaona hakupokelewa na Abdul ila aliingia Dar es Salaam mwenyewe na hakuwa na mwenyeji kwangu ni sawa pia.
Nyerere hakupokelewa na Abdul, msome Pascal Mayalla amekupa kila nukta ya maisha ya Mwalimu. Abdul Sykes hakuwahi kumpokea Nyerere
Msikilize Daisy nini anaeleza:
Hayo ya Daisy ni nonesense , hayajibu swali la lini Abdul Sykes alimpokea Nyerere na Nyerere alikuwa anatokea eneo gani na mwaka gani!

Mohamed watu hawana interest kusoma vitu bila utaratibu.
Msomi akiulizwa swali anajibu swali, hapa napo pana shaka sana!
 
Umeingia katika mjadala kati kati. soma kuanzia mwanzo utaelewa tunazungumzia nini

Halafu elewa hoja imekuwepo lini na Maprofesa wameandika lini.

Nadhani utulie kidogo ujifunze, hapa ni pakubwa kwa kimo.

Ahsante
 
La ikiwa nyinyi mnaona hakupokelewa na Abdul ila aliingia Dar es Salaam mwenyewe na hakuwa na mwenyeji kwangu ni sawa pia.
Hii mzee wangu katika elimu ya uhakiki wa habari "si sawa" hao wanao ona hivyo wanatakiwa kutupa ushahidi pia.

Ila mzee wangu wewe una busara sana navumilivu,ningekuwa mimi hapa ningekuwa nishamjeruhi mtu, sasa sijui tatizo mimi ni kijana bado au nina maarifa machache, maana naona kuna watu hata misingi ya kuhakiki habari hawana na wanaendekeza ujinga mno.
 
Sir...
Natambua hii historia jinsi inavyowachoma baadhi ya watu.

Ikiwa unaona kuwa kuishi Pugu ni sawa mtu kaishi Dar es Salaam Mtaa wa Stanley kwangu ni sawa.


Mzee,historia inamchoma nani?personally hainichomi maana hakuna siku itanipa kula wala kuninyima kula ila watu tunachokitaka hapa ni maneno yapangwe inavyotakikana kwa manufaa ya vizazi vinavyokuja!

Hiyo paragraph ya pili unaonekana wazi kuikimbia hoja yangu,lengo ni kwamba mimi ni mdogo siijui Dar ya 1940s wala sijawhi kuhadithiwa kama wewe so utanipoteza kuniambia Pugu ya miaka hiyo ikiitwa Mkoa wa Pugu na Dar ilikuwa ni hiko kipande cha Stanley kwa sababu ndipo walipokuwa wanaishi ndugu zako unaowaandika ndika humu.

Swali la msingi hapa ni:Mwl kabla hajaacha kufundisha na kabla ya kufahamiana na Abdul alikuwa akiishi Dar au hakuwahi kabisa kuishi Dar?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeingia katika mjadala kati kati. soma kuanzia mwanzo utaelewa tunazungumzia nini

Halafu elewa hoja imekuwepo lini na Maprofesa wameandika lini.

Nadhani utulie kidogo ujifunze, hapa ni pakubwa kwa kimo.

Ahsante
Sasa hapa ninaweza kukuonyesha kwanini nimeingia katika huu mjadala, kwanza napenda ukweli na kuuchukua popote ulipo. Siyo kweli, mpaka nimeamua kukuuliza swali hilo ujue sijakurupuka nimesoma kwanza kisha nikakuuliza, lakimo kuna tatizo lingine nimeliona kwako, hili kwa kanuni za kuutafuta ukweli nimeamua kwanza kulipa muda mpaka nitakapo ona kuna haja ya kuliweka wazi.

Hoja kuwepo lini si hoja bali hoja ni huo ukweli unaofanya mzozane, hapa unatakiwa uwe makini, hoja hata ingekuwa lini, lakini swalini kuwa kupokelewa unakuelewaje ?

Sasa hivi kwa akili yako tu kaa maprofesa wameandika lini, hii ndiyo itabadilisha ukweli wa kuwa mzee Nyerere amepokelewa na mzee Abdul au hakupokelewa ?

Sasa kama hapa ni pakubwa kwa kimo, mbona umezidiwa wewe na umekimbia swali langu la msingi ?
 
Sir...
Nakusoma naihisi hamaki katika jambo lisilo hamakisha:

HISTORIA YA ALI MSHAM NA JULIUS NYERERE 1955

Kuna picha ya Mtaa wa Jaribu Magomeni iliyowekewa maelezo kuwa ni Mtaa wa Congo.

Picha hii imekuwa ikizunguka sana mitandaoni.

Picha iko hapo chini.

Huu si Mtaa wa Congo wala si mwaka wa 1920.

Huu ni Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa miaka ya katikati 1950s na hapo ni nyumbani kwa Ali Msham aliyehamia Dar es Salaam kutokea Kilwa, aliyefungua tawi la TANU nyumbani kwake mwaka wa 1954 kupigania uhuru wa Tanganyika.

Picha hii ilipigwa siku chache Februari, 1955 kabla Mwalimu Nyerere hajakwenda UNO na siku hiyo Ali Msham na wanachama wa TANU walikusanyika hapo kufanya kisomo na dua kumwomba Allah ajaalie safari njema yenye mafanikio kwa lile walilokuwa wanalipigania.

Ali Msham alikuwa fundi seremala na akifanya shughuli zake Mtaa wa Kariakoo na Kibambawe.

Mimi naishi jirani na hii nyumba.

Watoto wa marehemu Ali Msham ni jirani zangu hapa Magomeni Mapipa na walisikia siku moja nafanya kipindi Radio Kheri kuhusu TANU ndipo waliponiletea picha na wakanieleza historia ya baba yao Ali Msham na Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Baba yao marehemu Ali Msham alifungua tawi la TANU nyumbani kwake na tawi hili lilikuwa na wanachama wengi hasa wanawake.

Mwalimu Nyerere alipohamia Magomeni mwaka wa 1955 Ali Msham alimfungulia Mama Maria kijiduka kidogo hapo kwake cha kuuza mafuta ya taa.

Mama Maria alikuwa pia akiwa dukani kwake akifuma sweta.

Siku moja Ali Msham alikwenda ofisini kwa Mwalimu Nyerere pale New Street akakuta samani alizokuwa akitumia Mwalimu ni duni sana.

Ali Msham alisikitishwa na hali ile.

Ali Msham alitengeneza samani mpya kiwandani kwake na akanunua na saa ya ukutani kwa ajili ya ofisi ya Rais wa TANU na akamuomba Mwalimu Nyerere wamkabidhi samani zile kwenye tawi lake la TANU Magomeni Mapipa Mtaa wa Jaribu katika sherehe maalum.

Angalia picha hapo chini Ali Msham ni wa kwanza kulia na Mwalimu Nyerere amekaa kwenye meza.

Picha ya sherehe hii na nyingine za harakati za baba yao katika TANU watoto wa Ali Msham wamezihifadhi kuanzia mwaka wa 1955 hadi leo.

Nilichofanya mimi niliaandika historia ya Ali Msham na nikaiweka katika blog yangu mohamedsaidsalum.blogspot.com pamoja na picha zile.
 


Kaka inawezekana wewe ndio haupo makini, na mara zote tulipojadiliana mambo mbalimbali ulionaonekana kuwa "dogmatic" na mchache wa elimu.

Wewe huoni Mohamed said kaelewa!!--- sasa umekuja wewe mwenye vituko kujaribu kunikosoa kwa kitu usichokuwa na elimu nacho.

Neno "Taazia" ni kiarabu (تعزية), [Taa'ziyah], usiseme kwamba hilo neno linayo asili ya kiarabu, ni neno la kiarabu pure. Mtohoo wake kwa kiswahili ndiyo maneno Tanzia au Tazia inategemea na mahali gani mtu unatokea, sisi kutoka bara (kama alivyosema Mohamed said) tunapenda kutumia Tanzia, na kwa mswahili kutoka popote Tz atakuekewa tu.

Kifupi ni kwamba "Taazia" ni kiarabu na hayo mengine ni ya kiswahili yaliyotoholewa kutoka hilo neno.

Sasa misuli ya shingo na povu lisikutoke kaka ukawa kituko- kitokeo
 
je uliwahi kumhoji Mzee Mkapa?

familia ilipeleka tangazo la taazia?

na kama kwa Mzee Mwinyi, Jakaya kuna shida na ww ufanye uwahoji..

siyo wamalize mwendo uje pia kushutumu na kuchonganisha famila zao na familia ya Sykes
 
kwenye QUR'AN pia HADITHI za mtume MUHAMMAD rehma na amani ziwe juu yake. mmeelekezwaje juu ya kuueleza wasifu na tabia za marehemu?
 
Neno likishatoholewa linakuwa na lugha iliyotohoa na kupokea neno husika. Hivyo katika lugha sahihi kiswahili sanifu ni Tanzia. Hakuna haja ya kusema ni neno la kiarabu, arabuni hakuna neno Tanzia. Ukitaka kujua asili yake ndio tunasema lina asili ya kiarabu.
 
Naona unaendelea kukosea, niliposema una matatizo ya kutokuwa makini sikukudhulumu, japo tamko umeliandika mwenyewe tena kwa kiarabu lakini bado huoni kama "Taazia" ni tamko lenye asili ya Kiarabu, ukisoma tamko kwa Kiarabu kuna (ع) ila kwa Kiswahili kuna (a) sasa unapokosolewa kubali kukosolewa sababu unapozidi kujitutumua unakosea zaidi.

Lakini jambo lingine linaonyesha kutokuwa makini zaidi, mzee Muhammed Said amemnukuu msomi mashuhuri wa Kiswahili mzee Abdulatif Abdallah, lakini hili hukuliona kwamba huyo aliyenukuliwa ni msomi mkubwa na amepatia ya kuwa tamko "Taazia" ni lenye asili ya Kiarabu, na umeweka matini ya Kiarabu, sisi Waswahili hatuna (ع) kijaba ndiyo maana hilo tamko hata ukilimtaka haliwi la Kiarabu, na ukisoma vitabu vya Kiarabu kwao wao tamko ili liwe la Kiarabu shati liabdikwe kwa Kiarabu ba litamkwe kwa Kiarabu, rejea kitabu "Durrat al Yatima" utaliona hili.

Sasa tunapo kukosoa ujue katika hilo tunalo kukosoa kwalo tumekuzidi elimu. Sasa acha ubishi wa kitoto.

Sasa nasisitiza ya kuwa una tatizo la kutokuwa makini. Ukija tena kuijibu kauli yangu hii lazima utakosea tena.
 
M...
Zamani nikiandika tanzia. Abdilatif Abdallah mtaalamu wa Kiswahili akaniambia hicho ni Kiswahili cha bara.

Sisi watu wa pwani tunasema "taazia," kwa kuwa neno lenyewe asili yake ni Kiarabu.
Inamaana huyo Abdilatif Abdallah akikuambia chochote unakubali tu......

Ni busara na ni hekima kukubali makosa kwa kutumia neno ambalo sio la Kiswahili....
 


wewe andaa hii mada (tengeneza post) na unikaribishe tujadiliane, maana katika ukumbi huu sisi ni wageni na hii sio mada kuu ya kujadiliwa hapa. Kwa heshima ya Mohamed said itakuwa sio vyema kuingiza mada nje ya mada.
 
Kuna wakati unajiuliza ni kwa nini Mzee Said huwa "anajitoa ufahamu?"
 
asante wakongwe kwa kubishana kwa hoja na kwakutotumia lugha ya utusi licha ya kurushiana maneno...kwangu huu ni uzi bora sana..

mabishano yamenifanya nijifunze mengi sana..

Mohamed Said wewe ni mwandishi bora kwa upande wangu ...asante kwa elimu
 
wewe andaa hii mada (tengeneza post) na unikaribishe tujadiliane, maana katika ukumbi huu sisi ni wageni na hii sio mada kuu ya kujadiliwa hapa. Kwa heshima ya Mohamed said itakuwa sio vyema kuingiza mada nje ya mada.
Hili halina haja ya mada sababu nimeshalimaliza, na huna hoja ya kupinga hili, na jambo kwa ujumla wake huna elimu nalo.

Hili kadhalika haliko nje ya mada, sababu wewe umeleta ujinga, lazima tukukosoe hapa hapa.

Nimecheka sana, yaani kitu unakiandika mwenyewe lakini unashindwa kutofautisha, sasa sisi tunaandika elimu, tunakukanya uache ubishi wa kijinga kwa jambo ambalo huna elimu nalo.
 
Naam

Hoja kwa hoja kama hivi jamii inakua forum kweli kweli
 
Nyerere kaja Dar na kafikia kwa Abdul Sykes na wapo walioishi nae ndani ya nyumba moja.

Hivi ili kupata ushahidi wa Nyerere alivyofika Dar tumfuate aliyeishi Tandahimba? Na sio aliyemkaribisha kwenye Nyumba yake?

Ikiwa harakati za Uhuru zilianzia Dar kwa nini iwe vibaya kuwauliza watu wa Dar?

Kama nawe una taarifa za harakati za eneo lako tuwekee tusome. Sio kubisha tu.

Mzee Mohamed Said anazungumzia harakati za Uhuru zilizokuwepo Dar na kwa wazee wake.

Kama na ninyi mna historia za harakati za Uhuru za wazee wenu sehemu zingine tuleteeni tusome tujue.

Lakini hamleti isipokuwa kupinga tu na mkipinga hamleti zilizo sahihi.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…