Yaani huyo
Mohamed Said asivyokuwa na aibu, hata sina muda wa kuzijibu upuuzi wake. Inaonekana ndivyo alivyolelewa, kuishi kwenye uongo. Uongo unaonekana umemnufaisha kwa kiwango kwamba bila uongo hawezi kumudu maisha. Bahati mbaya anao wawezeshaji, ambao kwa makusudi wanameza hizi ngano zake za kutunga akiamini akizirudiarudia zitakuwa za kweli. Siku hizi nikiona mada yoyote humu imeanzishwa na huyo anayejiita
Mohamed Said hata sisumbuki kuisoma...sina muda huo!
Mkuu si kwamba nimekualika kuna jambo jipya, la hasha.
Nimekualika kwa 'new development''. Sina shaka unajua ngano marejeo uongo. Labda nikupe geni kidogo.
Nimefuatilia nyuzi zake baada ya kifo cha Mkapa nijue kuna lipi jipya katika ngano.
Ukisoma Tanzia utagundua tatizo si Mkapa, huyo ametumika tu kupumua (vent) chuki zake dhidi ya Nyerere.
Kaandika Mohamed ''... achilia mbali kwamba Abdul Sykes ndiye aliyempokea Nyerere Dar es Salaam''
Katika maandishi hayo kwa mtu asiyeweza kupambanua mambo au mgeni wa mada ni rahisi kuamini ujio wa Nyerere Dar ni matokeo ya kazi ngumu sana aliyofanya Abdul Sykes mwana wa Kleist Mbuwane.
Pascal Mayalla kamtembeza Mohamed jinsi na mara ngapi na kwanini Nyerere alikuja Dar, akishadidia hoja yangu kuwa mwaka 1948 katibu wa Tawi la TAA Tabora alikuja Dar, na ni wendawazimu kuamini hakuna mtu wa makao makuu akiwemo Sykes aliyemjua Julius Nyerere, mmoja wa wasomi wachache sana Tanganyika na katibu wa Tawi.
Mohamed akaja na majibu yafuatayo
1. Andikeni vitabu mueleze historia yenu. Of course tumemuelimisha kuwa hatuwezi kudurusu kazi za kisomi kwa kuandika vitabu, kama hilo linatokea duniani basi kila mwenye hoja lazima aandike kitabu!
2. Akasema watu wengi wanajua Abdul amempokea Nyerere.
Tumemjibu hayo ni majibu ya vijiweni, msomi hathubutu kuandika hivyo.
Ilimradi watu wengi wanasema basi kwake ni proof, tena akiwa ameandika vitabu!!
3. Akaja na hoja kuwa Prof Shivji na Prof Saida wameandika hivyo.
Tumemueleza kuwa kitabu chao cha wasifu wa Mwalimu kina mwaka tu.
Kuanzia 2010 Mohamed ameaminisha umma, leo anatumia kitabu miaka 9 baada ya kuhubiri uongo! Tukamwambia hata maprofesa tunawaalika hapa, ukweli utabaki kuwa hivyo!
4. Kilichonishtua na kukualika ni hoja kuwa, Abdul Sykes alimpokea Nyerere kutoka Pugu kuja mtaa wa Stanley Dar es Salaam. Kwamba, Pugu haikuwa sehemu ya Dar
Mohamed hana habari na East province , na kwamba barua kwenda St Francis zilikuwa na address ya Dar es Salam. Mohamed haelewi lini Dar es Slaam iliondolewa na kuwa cost region na Pugu kuwa kisarawe.
Sasa utetezi kama huu baada kushindwa kufinyanga uongo ni ushahidi wa wazi kwamba, mzee wetu anatengeneza majungu na kuayaita historia.
Haiwezekani Hisia zikawa sawa na historia na historia haindikwi kwa majungu.
Ukimsoma zaidi hana majibu, yeye anachotaka ni kupoteza mada na kuendelea kupotosha umma.
Kinachochagiza upotoshaji ni mahaba yasiyo na kifani kwa Abdul Sykes na chuki iliyotitia dhidi ya Nyerere.
Mkuu ni hayo tu, nikasema nikujulie hali mkubwa