Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #261
Tom...Ilikuwaje ukashindwa kuuliza mhusika akiwepo?
Kumuuliza muhusika yupi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tom...Ilikuwaje ukashindwa kuuliza mhusika akiwepo?
Horse...Sheikh Mohamed Said kwa faida ya vizazi vilivyozaliwa era ya mzee Mwinyi kupanda juu unaonaje ukawafanyia hisani ya kuweka kitabu cha kina Sykes na Historia ya TANU ktk PDF form ili wenye kupenda kuchimbua wapate mwanga halisi na kuepuka hii mikanganyiko isiyokua ya lazima ambayo wenye kuuibua ni wachanga wa historia? Asante
Noted Chief.Horse...
Kitabu kimechapwa na publisher Minerva Press London (Kiingereza) na Phoenix Publishers Nairobi (Kiswahili)kwa nia ya kukiuza.
Hawezi wakakitoa bure kwa PDF.
Ninachokiona kwenye uzi huu ni ubinafsi uliopitiliza. Pande zote hazitumii hoja bali ni hisia zimewatala. Kila mtu anataka kuona kile anachodhani ni ukweli kinawateka wasomaji. Hili si jambo zuri sana katika uanazuoni.
Umeshasoma mada ngapi za huyu Mzee? Nahisi humfahamu huyu mfia dini wa pwaniNinachokiona kwenye uzi huu ni ubinafsi uliopitiliza. Pande zote hazitumii hoja bali ni hisia zimewatala. Kila mtu anataka kuona kile anachodhani ni ukweli kinawateka wasomaji. Hili si jambo zuri sana katika uanazuoni.
Unampa jukumu zito sana huyu Mzee na asiyoiweza, anachoweza ni kutunga stories za uongo na kupost humu.Hatuhitaji nyaraka za vikao au mialiko n.k
Tuletee nyaraka moja tu, Katiba. Iwe ya AA ya Kleist au TAA ya Abdul
Kama kuna kipande cha karatasi iwe robo au nusu tuwekee hapa
2. Tuonyeshe kiongozi mwingine wa siasa zaidi ya Mwl Nyerere aliyewahi kutangaza katiba achilia mbali kuwa nayo
3. Tuonyeshe ushiri wa Abdul kuandika katiba ya Seaton! kwa maana kama Abdul alikuwa na 'mkono' ukiachilia urafiki wake na Seaton katika chai na makaimati.
Hatuhitaji kitu kingine chochote kile, ni hayo matatu tu hapo juu
Zamani nikiandika tanzia. Abdilatif Abdallah mtaalamu wa Kiswahili akaniambia hicho ni Kiswahili cha bara.
Sisi watu wa pwani tunasema "taazia," kwa kuwa neno lenyewe asili yake ni Kiarabu.
Kasha...Kwahiyo wewe unaona Kiswahili cha bara ni haramu bali kile unachokiita cha Pwani, ilimradi kwa asili ni Kiarabu!!!
Wanajamvi, hapa MS anasema ameandika historia ya Wazee wake. Hilo si tatizo kabisa na ni haki yake na awaye akitaka naye pia atende."Mohamed Said, post: 36271731, member: 12431"]
Nimeandika historia ya wazee wangu katika kukabiliana na ukoloni.
Sina shaka ulizisoma zote na hakuna mahali ulipata ushahidi wa uwepo wa katiba ya AA au TAA.Pamoja na mswada huo nilifunguliwa Sykes Papers zenye historia ya TAA na TANU kuanzia miaka ya 1920 hadi uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961.
Jitihada za kum-sideline Nyerere zinaanza.Pamoja na hao tena nilifanya mazungumzo marefu familia ya Sykes na wakanieleza yale waliyofanya wakati wa kuunda TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.
Well, nyaraka nyingi zinamusu Nyerere wakati akisambaza TANU.Huenda Mohamed ukawa na nyaraka za Kleist na Abdul Sykes mikoani, na hilo lingetufariji tukizionaNilipita mikoani ambako nilizungumza na wazalendo waliokuwa hai na nilikusanya nyaraka na picha na kupata maelezo ya historia ya uhuru.
Nguruvi...Wanajamvi, hapa MS anasema ameandika historia ya Wazee wake. Hilo si tatizo kabisa na ni haki yake na awaye akitaka naye pia atende.
Mohamed anasema hakuandika historia ya Watu wa Tanganyika, bali sehemu ya watu ambao ni wazee wake.
Sina shaka ulizisoma zote na hakuna mahali ulipata ushahidi wa uwepo wa katiba ya AA au TAA.
Je, kadi ya uanachama ya Kleist ya AA 1929 ilikuwa namba ngapi?
Je, kadi ya uanachama wa Abdul Sykes ya TAA ilikuwa namba ngapi?
Umetueleza kadi ya Abdul ya TANU ni Namba 3, Nyerere ni 1. Jitihada za kum-sideline Nyerere zinaanza.
MS anaonyesha kuwa TANU iliundwa na Familia ya Sykes.
Ukweli ni kuwa TANU iliundwa na watu wengi akiwemo Nyerere.
Kama Nyerere hakuwepo Mohamed thibitisha
Lakini pia ni makosa kusema Familia ya Sykes iliyoingia nchini kama Mamluki wa kupigania na si kupinga ukoloni ilipigania Uhuru. Tunaweza kuona haya kwa ushahidi kuwa hakuna mahali popote Abdul Sykes au baba yake Kleist walikwenda mikoani kwa shughuli za siasa ukiacha Tandamti, Agrey , New street na kidongo chekundu. Well, nyaraka nyingi zinamusu Nyerere wakati akisambaza TANU.Huenda Mohamed ukawa na nyaraka za Kleist na Abdul Sykes mikoani, na hilo lingetufariji tukiziona
Mimi ninapokushangaa ni pale unapoulizwa jambo halafu unajibu kitu kingineNguruvi...
Unanifurahisha sana kwa maswali yako kwa kweli unanifanyia ikhsani kubwa sana.
Ningeweza kukuwekea mengi hapa lakini natayarisha kipindi cha kesho asubuhi na nimeweka hapa tangazo.
Naingia break kwa muda In Shaa Allah kukuwekea haya:
Sijui kama umepatapo kusoma habari hizi hapo chini:
Mohamed Said: TANGANYIKA POLITICAL INTELLIGENCE SUMMARY, MARCH 1952
"Tanganyika Political Intelligence
Summary, March 1952":
"...it is reported that the Secretary of the Association, Abdul Wahid Sykes has
dispatched letters to all branches asking members for suggestions under
the following heads for a memorandum to be prepared for the Royal
Commission..."
“...Abdul Wahid Kleist Sykes, Secretary of the African Association who, as
reported in last month's summary (paragraph 20) was going on safari up
country, visited Mwanza, where he met Paul Bomani, President of the
Bukoba African Association, and accompanied him to Bukoba. Sykes then
visited Kampala alone.....on 8th March, a secret meeting was held, attended
by leading members of the Mwanza Branch...”
(Hizi ni taarifa kutoka Rhodes House Library, Oxford kutoka majalada ya
kikachero ya Waingereza baada ya miaka 50 yanawekwa wazi kwa mtafiti
yeyote kuyasoma na kufanya nakala akipenda).
Nguruvi...Mimi ninapokushangaa ni pale unapoulizwa jambo halafu unajibu kitu kingine
Mara nyingi nimekuwa najiuliza, hivi unaelewa swali au huelewi au swali halieleweki?
Kusafiri si kufanya mkutano, mbona Abdul alikwenda Ukerewe kama unavyosema na sijawahi kukuuliza?
Pili, nimekuuliza katika mkabrasha ya AA kadi ya Kleist ilikuwa namba ngapi?
Tatu, katika TAA, kadi ya Abdul sykes ilikuwa namba ngapi?
Nne, Je, TANU ikiundwa Nyerere hakuwepo? Alipataje kadi namba 1 kwa chama kilichoundwa mwaka 1929?
Ofisa...hivi mwaks 1929 nyerere alikuwa na miaka mingapi?
MOHAMED NA MOHAMED SOMO NA SOMO: GUMZO LA MOHAMED GHASSANINguruvi...
Ahsante ndugu yangu.
Sote tunashangaana.
Katika kitabu "Ben Hur The Tale of the Christ" kilichoandikwa na Lew Wallace, Messala anamwambia Juda Ben Hur, "Nakuonya."
Ben Hur akamjibu, "Tunaonyana."
Unanishangaa mimi kuwa sijibu maswali yako wakati mimi najibu zaidi ya maswali yako.
Hizo nilizokuwekea ni taarifa za Special Branch.
Hizi taarifa ninazo kadhaa nimeletewa na vijana kutoka Ulaya na Marekani wanaokuja kunihoji kwa ajili ya thesis zao za Ph D na wao kwa kule sasa kumjua Abdul Sykes wamefanya utafiti zaidi juu yake.
Hayo niliyokuwekea hayamo katika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.
Kwa upande wangu mimi pia hujiuliza kuhusu wewe kuwa hii ni hasad au kitu gani?
Ni hasad kwangu au kwa Abdul Sykes?
Ndipo nikauliza vipi mzalendo kama Abdul Sykes na yake yote yale akafutwa katika historia ya TANU?
Mohamed ukiulizwa kitu unajibu ulichoulizwa. Nadhani hili halina shida labda kama tunalifanya shida bila sababu"Mohamed Said, post: 36275788, member: 12431"]
Unanishangaa mimi kuwa sijibu maswali yako wakati mimi najibu zaidi ya maswali yako.
Mfano mzuri huu hapa. Mimi sijahoji source ya taarifa zako na kwamba zimepatikana wapi.Hizo nilizokuwekea ni taarifa za Special Branch.
Sawa sawa wanatoka Ulaya, sisi ni wa hapa nyumbani na unaweza kuwatumia kutusaidia ndio maana tunahitaji ufahamu.Hizi taarifa ninazo kadhaa nimeletewa na vijana kutoka Ulaya na Marekani wanaokuja kunihoji kwa ajili ya thesis zao za Ph D na wao kwa kule sasa kumjua Abdul Sykes wamefanya utafiti zaidi juu yake.
Hakuna aliyeyahitaji.Hayo niliyokuwekea hayamo katika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.
Hapana sina husda kabisa na sina sababu za kuwa na husda, nina sababu za kukemea husdaKwa upande wangu mimi pia hujiuliza kuhusu wewe kuwa hii ni hasad au kitu gani?
Hapana si kwenu, ni mnakasha tu. Sifa moja ya usomi ni uvumilivu wa kazi unazofanya. ukishajipambanua kama mwana historia basi daraja lako ni la juu, lakini pia daraja hilo haliji bila chujio.Ni hasad kwangu au kwa Abdul Sykes?
Hapana usiwe na shaka hawezi kufutwa, mbona umejitahidi kumdunisha na kumdhalilisha Nyerere lakini kila siku anazungumzwa? Hata wangeungana woote wa Mzimama kila mmoja ana nafasi yake, na hili la husda dhidi ya Mwalimu linakera. Najiuliza hivi husda dhidi ya Nyerere ni kwa lipi?Ndipo nikauliza vipi mzalendo kama Abdul Sykes na yake yote yale akafutwa katika historia ya TANU?
Nguruvi..Mohamed ukiulizwa kitu unajibu ulichoulizwa. Nadhani hili halina shida labda kama tunalifanya shida bila sababu
Ukiniuliza, Abdul Sykes alikuwa mtoto wa Kleist? Jibu langu ni ndiyo au hapana kutegemeana
Ukiniuliza Sheikh Chambera anafahamiana na Abdul Sykes? Nitakujibu sijui au najua abcd
Nitakuwa wa ajabu kidogo ukiniuliza habari za Sheikh Chambera na Abdul halafu nikakuletea maelezo mengi na marefu ya uhusiano wa Chambera na Nyerere na alivyokwenda Lindi baada ya mwaliko.
Umeona kwanini ninashangaa? Mfano mzuri huu hapa. Mimi sijahoji source ya taarifa zako na kwamba zimepatikana wapi.
Nilichokihoji ni kitu kimoja, niwapi na ni lini Abdul Sykes alihutubia mkutano nje ya Tandamti na Kipata? Sijauliza aliwahi kusafiri kwenda wapi kumbuka hilo
Nikauliza, kadi ya Kleist Sykes ya AA ilikuwa namba ngapi? Sijauliza special branch wanasemaje
Nikauliza kadi ya Abdul Sykes ya TAA ilikuwa namba ngapi? Sijauliza special branch wanasemaje
Nimeuliza haya kwasababu wewe umebahatika kusoma makabrasha kwa mujibu wako.
Halafu nikauliza, kama TANU iliundwa 1929 na Familia ya Sykes na nadhani Nyerere alikuwa na miaka 7 Butiama, iweje basi kadi yake ya TANU iwe namba 1 na Abdul Namba 3.Sawa sawa wanatoka Ulaya, sisi ni wa hapa nyumbani na unaweza kuwatumia kutusaidia ndio maana tunahitaji ufahamu.
Kutokujua haijawa dhambi au kosa lakini kutotaka kujua au kujua kwa kububusa ni hatari kuliko kutojua.
Tuache ya Ulaya tuendelee na mnakashaHakuna aliyeyahitaji.Hapana sina husda kabisa na sina sababu za kuwa na husda, nina sababu za kukemea husdaHapana si kwenu, ni mnakasha tu. Sifa moja ya usomi ni uvumilivu wa kazi unazofanya. ukishajipambanua kama mwana historia basi daraja lako ni la juu, lakini pia daraja hilo haliji bila chujio.
Na si wote tunaoweza kumeza bila kutafuna, la hasha! si wote tunaovumilia kusikia mpapai unazaa maembe. Tutauliza, umepandikizwa ? na kwa njia gani maana chungwa na limao ni ndugu! Hapana usiwe na shaka hawezi kufutwa, mbona umejitahidi kumdunisha na kumdhalilisha Nyerere lakini kila siku anazungumzwa? Hata wangeungana woote wa Mzimama kila mmoja ana nafasi yake, na hili la husda dhidi ya Mwalimu linakera. Najiuliza hivi husda dhidi ya Nyerere ni kwa lipi?
Hii mada si ya Mkapa, Marehemu ametumika kama daraja.
mlengwa hapa ni mzee mla Mayai kwa Sykes, Mwl Nyerere! Kambarage anayekwenda sokoni bila pesa