Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?

Na hili ndo linamfikirisha kila mtu. Kwa mfano kila mtu ambaye fimilia yake ilihusika ktk Uhuru leo wadai national recognition hii nchi itakalika?

Kuna sehemu MS anadai Kleist Sikes hakupewa umuhimu ktk msiba wa Nyerere ila alienda tu akiwa kama mkurugenzi wa ATCL. Sasa unajiuliza ina maana familia zote zilizoshiriki ktk Uhuru zinatakiwa zipate upendeleo wa kitaifa?

Jibu la mwerevu ni hapana. Hivyo anachofanya MS ni kuilinda mada ya Nyerere kuishi kwa Sykes na kuthibitisha kwa sarakasi nyingi kuwa familia ya Sykes ina mchango mkubwa kuliko familia za akina Mangi au za machifu na ma Mwami ambao wao hawakuishi na Nyerere nyumbani kwao au kumlisha Nyerere mayai.
Hizi ni identity politics tu.

Francis Fukuyama kaandika kitabu kizuri sana kuhusu identity politics.

Kinaitwa "Identity: The Demand for Dignity and the Politics of Resentment"

Baada ya kukisoma, namuelewa vizuri zaidi Mohamed Said.
 
Mzee Saidi mimi sikupingi katika uandikaji wa historia ya wazee wako. Ila naona kama unawapa umuhimu sana kuliko watu wengine waliokuwa na umuhimu sawa au kuwazidi wazee wako. Hapa unasema kubwa kwa Nyerere ni kutambulishwa kwa wazee wako. Hapa mtu anayesoma kwa kufikiri kama asemavyo Nguruvi lazima atang'amua au atahisi una ajenda. Kwa mfano hiyo sentensi moja umeipa para nzima. Kwa mtu anayejiita au kuitwa muandishi nguli kama wewe ukitumia paragraph kwa sentensi moja maana yake unaweka uzito unaostahili kwa kusudio fulani.
James. ..
Kama hukupendezwa jinsi ninavyowadhimisha wazee wangu sawa sina tatizo na hilo.
 
Na hili ndo linamfikirisha kila mtu. Kwa mfano kila mtu ambaye fimilia yake ilihusika ktk Uhuru leo wadai national recognition hii nchi itakalika?

Kuna sehemu MS anadai Kleist Sikes hakupewa umuhimu ktk msiba wa Nyerere ila alienda tu akiwa kama mkurugenzi wa ATCL. Sasa unajiuliza ina maana familia zote zilizoshiriki ktk Uhuru zinatakiwa zipate upendeleo wa kitaifa?

Jibu la mwerevu ni hapana. Hivyo anachofanya MS ni kuilinda mada ya Nyerere kuishi kwa Sykes na kuthibitisha kwa sarakasi nyingi kuwa familia ya Sykes ina mchango mkubwa kuliko familia za akina Mangi au za machifu na ma Mwami ambao wao hawakuishi na Nyerere nyumbani kwao au kumlisha Nyerere mayai.
James...
Abdul Sykes alifutwa katika historia ya TANU na si yeye peke yake.

Mimi nimewarudisha ili historia ya TANU ikamilike.
 
Hapa nimekaa nikifikiria nani yupo ktk list za article za Mzee Saidi kiasi kwamba mtu huyo akifa tutapata andiko la mabaya yake. Je ni Warioba? Joseph Butiku? Pius Msekwa? Maria Nyerere ? Mwinyi? Kikwete? And the list goes on... Ni heri uandike ili tuweze kuuliza nasi tusikie wanasemaje. Kwa mfano hiyo nukuu inayomtaja Nyerere kupokelewa na akina Sykes hapa Dar ktk hizi volume mpya za prof. Shivji, Shivji aulizwe huko twitter source yake ni nani ?
James...
Yote niliyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes sijaandika lile ambalo halikufanyika.

Nimemtaja Mama Maria hapa kama sehemu ya historia ya Abdul Sykes, Mama Sakina na mumewe Shariff Abdallah Attas mabinti zao Mwalimu Sakina na Mwalimu Fatna.

Nimeweka picha Mama Sakina, Bi. Titi Mohamed na Bi. Tatu bint Mzee wako na Nyerere uwanja wa ndege wanamsindikiza safari ya kwanza UNO 1955.

Nyerere Day Mzee Msekwa aliandika makala ambayo haikuwa sawa kuhusu historia ya TANU nimeijibu makala ile na ipo hapa In Shaa Allah nitaiweka hapa muisome.

Mimi sina sababu ya kuzua chochote katika yale waliyofanya wazee wangu.

Sasa wataalamu wa historia ya Afrika baada ya kuona haya yote ndiyo wakanitafuta na kunishirikisha katika miradi ya uandishi na kazi zangu zote wamezichapa.
 
MZEE PIUS MSEKWA HAIFAHAMU HISTORIA YA TANU

Katika gazeti la Tazama la leo tarehe 14 Oktoba 2019 kuna makala iliyoandikwa na Pius Msekwa yenye kichwa cha habari, ‘’Mwalimu Nyerere kama nilivyomfahamu (2),’’ ambamo ameandika maneno haya yafuatayo kuhusu Mwalimu Nyerere kuwa:

‘’...alifanikiwa kuwaridhisha kwa nguvu za hoja zake, wanachama wa iliyokuwa asasi ya kupigania maslahi ya wafanyakazi wa Kiafrika katika Serikali ya Kikoloni, iliyokuwa inaitwa ‘’Tanganyika African Association’’ (TAA).

Alifanikiwa kuwashawishi wanachama wa asasi hiyo kukubali wenyewe kuvunja chama chao hicho, na badala yake kuunda chama kipya cha siasa cha, ‘’Tanganyika African National Union (TANU), mnamo mwezi Julai, 1954, ili kiwe chombo cha kisiasa cha kupigania uhuru wa Tanganyika.’’

Mzee Pius Msekwa amekosea hii si historia ya kweli ya TANU na kwa bahati mbaya Mzee Msekwa hakutaja majina ya hao walioshawishiwa na Nyerere, ‘’ kuvunja chama chao.’’

TAA hakikuwa chama cha kupigania maslahi ya wafanyakazi wa Kiafrika katika serikali ya kikoloni.

TAA kilikuwa chama cha Waafrika kikipigania maslahi zaidi ya hayo ya wafanyakazi na kilifika wakati kikawa kinakidhi mahitaji ya Waafrika wa Tanganyika kama chama cha siasa kisichokuwa na katiba ya siasa na kwa ajili hii kikawa kinagongana na serikali ya kikoloni TAA ikishutumiwa kuwa ilikuwa inajihusisha na siasa dhahiri.

Gavana Twining alipata kutoa Government Circular kadhaa kuionya TAA kati ya mwaka wa 1951 hadi 1953 kuhusu kujihusisha na siasa.

Mzee Msekwa anaweza kuanza kuisoma historia ya African Association kutoka kwa kalamu ya mmoja wa waasisi wa chama hicho Kleist Sykes aliyoiandika kabla ya kufariki mwaka wa 1949 na mswada huu ukawa mikononi kwa mwanae Abdulwahid Sykes hadi mwaka wa 1968 pale bint yake, Daisy alipoutoa hadharani akiwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki, Dar es Salaam kama mada katika semina ya Idara ya Historia ya chuo hicho.

Wakati huo Daisy alikuwa mwanafunzi chini ya mwalimu bingwa wa historia ya Tanganyika, John Iliffe.

Matokeo ya mada hii ni sura katika kitabu alichohariri John Iliffe, (Daisy Sykes Buruku, ‘’The Townsman: Kleist Sykes’’ Moderm Tanzanians, Nairobi 1973, pp 95 – 114).

Laiti angesoma kitabu hiki Mzee Msekwa angeijua historia ya si tu TAA na TANU pia.

Hakuna popote katika sura hii ambamo imeelezwa kuwa TAA kilikuwa chama kinachopigania maslahi ya wafanyakazi wa serikali ya kikoloni.

Katika kitabu hiki anaweza pia kusoma maisha ya Hassan Suleiman na Ali Juma Ponda.

Hawa walikuwa viongozi wa TAA (''The Politicians Ali Ponda and Hassan Suleiman,'' pp. 227 – 253) na hakuna popote viongozi hawa walishughulika na maslahi ya wafanyakazi wa serikali wakiwa viongozi wa TAA.

Ningependa kuhitimisha nukta hii kwa kumfahamisha Mzee Msekwa kuwa huyu Abdul Sykes niliyemtaja hapa ni mtoto wa Kleist Sykes na ndiye baba yake Daisy alikuwa kiongozi wa TAA 1950 na ni mmoja wa wale wazalendo 17 walioasisi TANU mwaka wa 1954 na imesadifu kuwa nimeandika kitabu cha maisha yake, ‘’The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 – 1954) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,’’ Minerva Press, London 1998.

Mzee Msekwa akipenda anaweza kuisoma historia ya TANU kutoka kwa wenyewe waliounda African Association 1929 na wakaja kuunda TANU 1954 kutoka TAA Abdul akiwa na mdogo wake Ally, Julius Nyerere, Dossa Aziz, John Rupia na wazalendo wengine kutoka katika majimbo ya Tanganyika kama Japhet Kirilo, Joseph Kimalando, Saadan Abdu Kandoro kwa kuwataja wachache.

Kuwa Nyerere ndiye aliyewashawishi wazalendo hawa kuunda TANU hii si kweli.

Ikiwa utasoma kitabu cha maisha ya Abdul Sykes utaona mle mabadiliko yaliyotokea ndani ya TAA kuanzia mwaka wa 1950 baada ya Mwalimu Thomas Plantan kama Rais wa TAA na Katibu wake Clement Mtamila kuondolewa madarakani kwa mapinduzi na uongozi wa TAA ukachukuliwa na Dr. Vedasto Kyaruzi kama Rais na Abdul Sykes Katibu.

Abdul Sykes alikuwa na fikra ya kuunda chama cha siasa toka yuko Burma wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 – 1945) na alipoingia katika uongozi wa TAA na kuwa mjumbe katika TAA Political Subcommitee ambao wajumbe wengine walikuwa: Dr. Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Churembo, Steven Mhando na John Rupia na nia ya kuunda hii kamati ikiwa kuunda chama cha siasa.

Itamshangaza mtu yoyote kusikia kuwa Nyerere aliyepokelewa ndani ya TAA na Abdul Sykes 1952 tena wakati huo Abdul akiwa Kaimu Rais na Katibu TAA, iwe Nyerere ndiye aliyemshawishi Abdul na wenzake katika uongozi wa TAA ati wavunje TAA waunde TANU.

Mzee Msekwa anazungumza historia ambayo yeye haijui.

Ukweli ni kuwa kulikuwa na mazungumzo kabla na nyuma sana kati ya Abdul Sykes na Hamza Mwapachu kuhusu kuunda TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.

Abdul alishaanza mazungumzo na Chief Kidaha Makwaia achaguliwe Rais wa TAA na mwaka unaofuatia TANU iundwe na Chief Kidaha aongoze harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Kuna mengi hapa hadi Nyerere akaja kuchaguliwa kuwa Rais wa TAA mwaka wa 1953 na Abdul Sykes akawa makamu wake katika uchaguzi uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo.

Kikao cha kumpa Nyerere uongozi wa TAA kilifanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu, Nansio Ukerewe katika miezi ya mwanzoni 1953 kati ya mwenyeji Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ally Mwinyi Tambwe aliyekuwa Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) chama ambacho aliasisi baba yake Abdul mwaka wa 1933 na chama hiki ndicho kilichotoa wanachama na viongozi wa mwanzo wa TANU mwaka wa 1954.

Kwa kumalizia ningependa kumweleza Mzee Msekwa ni chama gani kilikuwa kinashughulika na maslahi ya wafanyakazi Waafrika katika serikali ya kikoloni.

Chama hiki hakikuwa TAA.

Chama kilichoshughulika na maslahi ya wafanyakazi Waafrika kilikuwa kinaitwa, ''Tanganyika Government Servant Association (TAGSA).''

Chama hicho kiliasisiwa mwaka wa 1927 kwa lengo la kuendeleza maelewano mazuri baina ya serikali ya Mfalme na watumishi wake Waafrika ili kuboresha huduma na kuendeleza maslahi na ustawi wa waajiriwa Waafrika.

Katika kipindi hiki cha mwanzoni mwa mwaka wa 1950 viongozi wa TAGSA walikuwa Thomas Marealle kama Rais na Ally Sykes Katibu.

Rashid Kawawa, Dr. Wibard Mwanjisi, Steven Mhando, Dr. Michael Lugazi walikuwa wanakamati na hawa wote walihusika sana katika kuunda TANU na wakiishi na fikra ya kuunda chama cha siasa kudai uhuru wa Tanganyika wala hawajasikia jina la Julius Nyerere.

Huu ndiyo ukweli wa historia ya TANU.
 
African Association, kama ilivyokuwa asili ya kilabu iliyotokana nayo, ilishikwa na Wamanyema.

Hivi ndivyo Wamanyema walivyokuja kuongoza siasa Tanganyika. Julius Nyerere, wakati huo akifundisha St. Mary's School, alishuhudia sherehe za uzinduzi wa African Association.

Nyerere hakutambua hata kidogo wakati huo kuwa alikuwa akishuhudia sehemu ya historia kazi yake mwenyewe ikijifungua mbele ya macho yake.

Mwaka 1946 wasomi wa Makerere walianza kujishughulisha na African Association pale Hamza Mwapachu na Julius Nyerere walipochaguliwa Katibu na Katibu Msaidizi na nafasi nyingine za uongozi zikishikwa na Wamanyema.
Wanajamvi, nipo Tingeni bado naangua nazi, imekuwa tabu kidogo kila janguo ni vidaka.
Ngogwe nazo zimeibwa na vijana kutoka kibanda na makinyumbi! hili nimemuachia Mzee Akida
Nitakapofika Mabawa Polisi nitanunua bundle, kuna yakuzungumza.

Ahsanteni
 
Nguruvi...
Wewe ndiyo unaetuchangamsha hapa barzani.

Pole kwa mkasa uliokufika.

Mwakinyumbi ndipo Kleist na Schneider chini ya Von Lettow Vorbeck wakiwa katika jeshi la Wajerumani walipopigana kwa mara ya kwanza na majeshi ya Waingereza yaliyovuka mpaka kutokea Kenya.

Haya kaeleza katika mswada wake ambao uko Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam East Africana toka mwaka wa 1968.
 
Hapa sasa sawa umemkosoa mtu angali hai. Hii inaweza kumfikia na yeye Msekwa akaitolea majibu.
Sasa mzee wangu hapa nilibahatisha tuu kuotea wale ambao wakifa unaweza kuwaandikia andiko hapa Jf. Nikuombe kama inawezekana kadri itakavyokupendeza tuwekee hapa baadhi ya article za kukosoa za watu ambo wangali hai ili waweze kadri watakvyoona inafaa kutolea majibu
James. ..
Kama hukupendezwa jinsi ninavyowadhimisha wazee wangu sawa sina tatizo na hilo.
MS,
Sina shida na jinsi unavyowaadhimisha wazee wako, hapana. Nina shida jinsi unavyohitaji wazee hao wapate national recognition. Najiuliza kuna nini? Mbona historia inatufundisha kuvumiliana. Leo hii na sisi wengine tuibuke tudai kutambulika kitaifa kisa mababu zetu walipigana na mjerumani katika majeshi ya akina mangi? jibu la mwerevu ni hapana. Tukitaka kuandika kama ufanyavyo wewe ni sawa. Shida ni kurudia rudia kudunisha baadhi ya viongozi na kuadhimisha kama unavyoita hao wazee wako.
 
James,
Hapa tunazungumza kuhusu historia ya TANU kama ilivyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni mwaka wa 1981 kitabu ambacho hakikuandika ukweli.

Mimi mwaka wa 1998 nikaandika kitabu cha historia ya TANU nikitumia vyanzo vikuu viwili

Kwanza mswada wa Kleist Sykes (1949) na Nyaraka za Sykes.

Kitabu kipo na hakuna popote nilipomdunisha yeyote.

Ikiwa kuna sentensi umeisoma ambayo inamdhalilisha yeyote tafadhali ilete hapa kama ushahidi.

Wala sijasema mimi kuwa wazee wangu nataka wapate chembelecho, "national recognition."

Kutambuliwa hakuji kwa mtu kutaka.

Naam baada ya kutoka kitabu changu watu wametambua upungufu uliokuwapo katika historia ya TANU na matokeo yake ni kuwa Abdul na Ally Sykes wametunukiwa Medali ya Mwenge wa Uhuru na serikali hii ya CCM.

Hili la kwanza.

Pili.

Kleist Sykes ametiwa katika Dictionary of African Biography (2011).

Haya yote yamepatikana baada ya mimi kuandika historia ambayo haikuwa imeandikwa.

Kama wewe ndugu yangu unaona huku ni kudunisha hiyo ni bahati mbaya sana kwako.
 
African Association, kama ilivyokuwa asili ya kilabu iliyotokana nayo, ilishikwa na Wamanyema.

Hivi ndivyo Wamanyema walivyokuja kuongoza siasa Tanganyika. Julius Nyerere, wakati huo akifundisha St. Mary's School, alishuhudia sherehe za uzinduzi wa African Association.

Nyerere hakutambua hata kidogo wakati huo kuwa alikuwa akishuhudia sehemu ya historia kazi yake mwenyewe ikijifungua mbele ya macho yake.

Mwaka 1946 wasomi wa Makerere walianza kujishughulisha na African Association pale Hamza Mwapachu na Julius Nyerere walipochaguliwa Katibu na Katibu Msaidizi na nafasi nyingine za uongozi zikishikwa na Wamanyema.
Kuna msemo usemao ''Uzee ni dawa'' na mwingine 'kuishi kwingi ni kuona mengi''
Wanajamvi, rejeeni nyuma katika bandiko moja la Mag3 akieleza mahusiano ya hadithi za Mohamed, Umanyema, Uzulu na Ushemeji miongoni mwao.
Kwamba, Mohamed anaandika habari za wajomba zake.

Wengi hawakumwelewa, walidhani Mag3 kachachawa tu na kuandika.
Hata 'wino' haujauka tunaona haya ya Wamanyema.
Kwa muda mrefu sana Mohamed Said amekwepa kuwaweka mbele, kadri muda unavyosonga hana jinsi

Lakini pia Mohamed akamdhihirisha Mag3 ukweli, pale aliposema Maulid ya 1960 yalisusiwa na wakazi wa Dar es Salaam kwasababu yaliandaliwa na Wazulu na Wanamnyema. Hata hivyo Sykes alihakikisha yanafanyika

Wazulu ndio hao wanaosemwa kuwaandamana Wazawa na kwamba sasa Watanganyika wanataka msamaha
Mohamed kaona bora awaadhimishe nduguze wa Kimanyema

Soma habari hiyo, MS anakuonyesha huyu Nyerere aliwakuta watu wakiwa na AA na ni Wamanyema

Halafu anaendelea kusema Makerere wakaanzisha chama na kutaja vyeo viwili, wengine ni Wamanyema

Hizi ni lugha laini sana lakini sisi watu wa pwani tunazijua.
Hatumwwambia mtu ''wewe wa kuja'' hapana, tunasema huyu ni mgeni, tukiwa wenyewe tunasema

Ndiyo yale yale ya Kambarage kula Mayai kwa Abdul Sykes, kwamba, hakuwahi kula kingine chochote isipokuwa mayai. Neno mayai linabeba uzito wake.

Au ni yale ya Nyerere kwenda sokoni bila pesa, huku pwani hatusemi hohe hahe, aa a! hiyo karha, tunasema hakuwa na senti.

Sasa Wazaramo walipokataa Maulid, walijua kilichopo nyuma ya Uzulu na Umanyema.
Hata leo si kuna mskiti wa Manyema! Lipi la ajabu hapo?

Tunapowaambia msome maandishi katikati ya mistari na yobi moja hadi nyingine hii diyo maana tuliyokusudia.

Muda mrefu mumeaminisha Waislam hawatajwi katika harakati za uhuru, hapana! hao ni Pazia tu, wasiotajwa ni Wazulu na Wamanyema.

Kwani Wazaramo hawakuwa Waislam?hawatajwi akina Ramadhani Ali.
Hawa si wenzetu wa kizulu au Kimanyema

Haya, alifajr njema, napeleka tenga la ngogwe Ngamiani, mashallah si kidogo.
 
Nguruvi,
Mjadala ulianza hapa na kurahisisha mambo naweka mwanzo wake kisha In Shaa Allah nitaendelea kujibu hayo uliyoandika:

KWA NINI BENJAMIN MKAPA ALISHINDWA KUCHAPA TAAZIA YA ABDUL SYKES KATIKA THE NATIONALIST BRENDON GRIMSHAW AKACHAPA "OBITUARY" YA ABDUL SYKES KATIKA SUNDAY NEWS (TANGANYIKA STANDARD)?

''Mgogoro wa EAMWS nimeueleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Vyombo vilivyohusika katika mgogoro ule kuanzia gazeti la Uhuru na The Nationalist Mkapa akiwa Mhariri, Radio Tanzania Dar es Dalaam Martin Kiama akiwa Mkurugenzi, Polisi Geofrey Sawaya akihusika na Usalama wa Taifa alikuwapo Rashid Kayugwa.

Wote hawa walikuwa wakiamrishwa kutoka juu wengine wameyasema haya kwa kujuta kabla ya kufa kwao.

Hakika ni mkasa wa kusisimua.

Nataka nikupe mfano mmoja.

Kifo cha Abdul Sykes katikati ya mgogoro wa EAMWS maziko yake yalikuwa hayajapata kuonekana Dar es Salaam.

Mazishi yale yalikuwa habari kubwa kutokana na mchango wa Abdul Sykes katika TANU na uhuru wa Tanganyika achilia mbali kuwa yeye ndiye aliyempokea Nyerere Dar es Salaam na kuishinae nyumbani kwake Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Haya hakuna aliyekuwa hayajui haya na hii ndiyo ilikuwa sifa yake kubwa akitambulika kama mwezeshaji wa mambo yote ya TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.

Sasa jiulize vipi magazeti ya TANU chama alichounda Abdul yasimwandike inavyostahiki?

Mkapa kama mwandishi bila shaka alijua uzito wa stori iliyokuwa mbele yake na pengine kwa kufahamu uhusiano wa Abdul na Nyerere alimtaka Nyerere mwenyewe amwandikie rafiki yake taazia kwa mkono wake au amhoji (exclusive interview).

Yawezekana kuwa Mkapa aliyataka yote haya kwa Mwalimu na yeye akakataa?

Hapa ndipo panapoumiza kichwa.

Kuamini kuwa Mkapa kwa kutaka kwake tu aliamua kupuuza kifo cha Abdul Sykes huu ni muhali mkubwa sana.

Mwandishi mpumbavu peke yake.ndiye anaeweza kuchagua uamuzi wa kijinga kama huu.

Benjamin Mkapa hakuwa mtu zuzu.

Kama ulivyohitimisha kuwa Allah ni mjuzi wa siri na dhahiri nami nasema hivyo hivyo.

Yapo mengi Mkapa aliyafanya hata alivyokuwa rais lakini kwa hali ya siasa zetu Tanzania, alijikuta mikono yake imefungwa na si kufungwa tu bali imefungwa nyuma ya mgongo wake.

Hapo chini ni taazia ya Abdul Sykes katika Sunday News la 20 October, 1968.

Lakini taazia hii ilileta mgogoro mkubwa ofisi ya TANU New Street.

Kuna baadhi ya viongozi ndani ya TANU walikerwa na taazia hii.

Hapo chini kuna Kumbukumbu ya Abdul Sykes kama zilivyochapwa na magazeti ya Chama na Serikali Uhuru na Daily News ya tarehe 12 Oktoba 1988.

Kumbukumbu hizi nazo zikafikwa na mkasa pia.
Wahariri walitishika na waliyoyasoma wakasema hawatachapa hadi wamepata kibali kutoka Dodoma.

Walipopewa ruhusa ya kuchapa Kumbukumbu ya Abdul Sykes yale yote muhimu katika kumuelewa Abdul Sykes yaliondolewa.''

Naanza na hili la Wamanyema.

Soma hapo chini:

WAMANYEMA WA DAR ES SALAAM KATIKA TANU NA SIASA ZA KUDAI UHURU

Iddi Faiz Mafongo TANU Card No. 24 Iddi Tosiri TANU Card No. 25 Ndugu Wawili Katika Kupigania Uhuru wa Tanganyika, 1954

Wamanyema wanajulikana kama watu wenye harara na ya ushujaa.

Mmanyema anaweza kuulipia fedha ugomvi ili na yeye awemo, na kadri mpinzani anavyokuwa na nguvu na hodari, ndivyo Mmanyema anavyofaidi ugomvi wake.

Katika siku hizo Wamanyema walikuwa wameshikwa katika magomvi.

Katika mwaka wa1941 ilibidi serikali, maimamu na masheikh wa msikiti mingine mjini Dar es Salaam kuingilia kati ili kuamua ugomvi uliowakumba Wamanyema kuhusu msikiti wa Manyema.

Msikiti huu Wamanyema waliujenga mwaka wa 1912.

Wamanyema hawakumstahi mtu yeyote, waligombana hata wenyewe kwa wenyewe.

Hamaki hizi zilipoelekezwa kwa serikali ya kikoloni zilikuja kuwa na manufaa sana.

Kwa kuwa walikuwa ni kabila la Waislam watupu, Wamanyema hawakuweza kufaidika na elimu iliyokuwa ipo mokononi mwa wamishionari.

Hata hivyo Wamanyema walipiga hatua kubwa katika elimu ya dini yao na hii ndiyo sababu kuwa hadi leo utamaduni wa Kiislamu umeenea katika kila familia ya Mmanyema iwe nyumbani Kigoma au huko pwani.

Mmanyema hayupo mbali sana na utamaduni wa Kiislam.

Wamanyema, Warufiji na Wadigo ni katika makabila ambayo ni tabu sana kumpata Mkristo.

Iddi Faiz alikuwa Mmanyema.

Hadhi yake iliongezeka zaidi kwa kuwa alikuwa mweka hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na TANU.

Vilevile aliifanyia kampeni TANU, akifuatana na Nyerere katika safari za awali za kukitangaza chama, akihutubia mikutano jukwaa moja na Nyerere.

Ilikuwa ni Iddi Faiz na kaka yake Iddi Tosiri ndiyo waliompeleka na kumtambulisha Nyerere kwa binamu yao Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo.

Ilikuwa ni baada ya utambulisho huu kwa Sheikh Ramia ndipo urafiki ukajengeka kati ya Sheikh Ramia na Nyerere na ndiyo Nyerere akakubalika Bagamoyo.

Sheikh Ramia akiwa khalifa wa tariqa ya Qadiriya alikuwa na murid wengi waliomfuata katika TANU kama kiongozi wao.

Juu ya hayo alikuwa miongoni mwa wanachuoni walioheshimiwa sana.

Hakuna kilichoweza kusimama na kuota mizizi Bagamoyo bila kupata ridhaa ya Sheikh Mohamed Ramia na hii ilikuwa toka wakati wa TAA.

Akiwa khalifa wa tariqa ya Qadiriya ambayo ilianzishwa na kustawishwa Bagamoya na baba yake, Sheikh Yahya Ramia, mwanzoni mwa karne ya ishirini, nguvu za Sheikh Ramia zilikuwa hazisemeki.

Alichosema sheikh ndicho hicho kilichofuatwa.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba IddI Faiz Mafongo alihudhuria mkutano wa uzinduzi wa TANU katika Ukumbi wa Arnautoglu mwezi Agosti 1954.

Haifahamiki kwa hakika hasa ni lini Iddi Faiz alijiunga na TANU kwa sababu kadi yake ya kwanza ya uanachama ilipotea na akapewa kadi nyingine iliyokuwa na namba 915 iliyotolewa tarehe 28 Agosti, 1954.

Lakini kwa kukisia tu kutokana na kadi ambayo Iddi Faiz mwenyewe aliitoa kwa kaka yake Iddi Tosiri ambayo ilikuwa kadi namba 25 na yenye saini yake kama afisa aliyetoa kadi hiyo, inaweza kuchukuliwa kwa uhakika kuwa Iddi Faiz alikuwa miongoni mwa wale watu wa mwanzo kabisa kuingia TANU na huenda akawa miongoni mwa wanachama ishirini wa mwanzo.

Ukichukua katika fikra ukweli kwamba Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa katibu wa Al Jamiatul Islamiyya aliingizwa TANU na Mtemvu katikati ya mwezi Agosti, 1955, huenda Ali Mwinyi kama katibu wa Al Jamiatul Islamiyya na Idd Faiz akiwa mweka hazina, wote wawili waliingia TANU wakati mmoja.

Iddi Faiz na nduguye Idd Tosiri, muasisi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika, walikuwa Wakusu, moja ya makabila ya Kimanyema, kwa upande wa baba yao; na Wabwali kwa upande wa mama yao.

Wote wawili walikuwa katika Batetera Union (Congo Association), chama kilichokuwa kikiwaunganisha Wamanyema wa Tanganyika.

Mzee bin Sudi alikuwa rais muasisi wa chama hicho na baada ya kifo chake Sheikh Hussein Juma alichaguliwa kushika nafasi hiyo.

Batetera Union (Congo Association) kilikuwa chama kilichoshikamana na chenye nguvu sana miongoni mwa vyama vya kikabila vilivyokuwapo wakati wa ukoloni.

Wamanyema ni kabila la Waislam watupu na kwa sababu hii hakukuwa na pingamizi katika kuunga mkono TANU.

Batetera Union kilikuwa na nguvu sana kiuchumi kwa kuwa kilikuwa katika wafuasi wake, watu waliomiliki majumba na walihodhi takriban nusu ya nyumba zilizojengwa mjini Dar es Salaam kati ya vita kuu mbili za dunia.

Uwezo huu wa kiuchumu uliwafanya Wamanyema kuwa wapinzani wagumu wa serikali ya kikoloni na uliwanyanyua hadi kufikia kuwa mbele katika siasa mjini Dar es Salaam na katika miji mingine ya Tanganyika.

Umoja wa Wamanyema ndiyo uliojenga msikiti maarufu wa Wamanyema mwaka wa uliokuwa karibu na makao makuu ya African Association.

Mzee bin Sudi alikuwa pia ni muasisi wa African Association mwaka wa 1929 pamoja na Kleist Sykes.

Batetera Union kilikuwa chama kilichoshikamana na chenye nguvu sana miongoni mwa vyama vya kikabila.

Umoja wa Wamanyema ndiyo uliojenga msikiti maarufu wa Wamanyema mwaka wa 1912 uliokuwa karibu na makao makuu ya African Association.

Kubwa ambalo Iddi Faizi alifanya ni kule kuwa mratibu wa safari ya kwanza ya Julius Nyerere UNO mwaka wa 1955.

Iddi Faizi ndiye aliyekuwa musanyaji wa fedha za safari hii na kama Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya alitoa fedha za jumuiya hiyo na kuzitia katika mfuko wa safari ya Nyerere UNO.

Picha: Iddi Faizi Mafongo Aliyevaa Kanzu Koti na Tarabush Uwanja wa Ndege Dar es Salaam Akimsindikiza Nyerere Kwenda New York, UNO 1955 wengine kuanzia kushoto ni Rashid Sisso, Robert Makange, Iddi Faizi Mfongo Julius Nyerere, John Rupia na Bi. Titi Mohamed

Habari zaidi za Iddi Faiz Mafungo ingia hapa:
http://www.mohammedsaid.com/2014/02/idd-faiz-mafongo-mweka-hazina-wa-safari.html

Sasa tuje katika Maulid ya Mfungo Sita ya mwaka wa 1963.

Kleist Sykes alikuwa katika Maulid Committee kuanzia mwaka wa 1926 hadi 1940.

Kleist Sykes na baadhi ya Wazulu, Wamanyema na Wanubi walijitoa katika kamati hii kwa hoja kuwa watashughulika na shule ya Al Jamiatul Islamiyya.

Hiki ni kisa kirefu hatuwezi kuyaongea yote hapa.

Mwaka wa 1963 Mwenyekiti wa Maulid Committee alikuwa Sheikh Abdallah Iddi Chaurembo aliyepata kuwa mwanafunzi wa Sheikh Hassan bin Ameir.

Hayo hapo chini ndiyo yaliyokuwapo wakati ule:

''Wakazi wa Dar es Salaam kila mwaka walikuwa wakifanya maulidi katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW).

Huu ndiyo toka asili ulikuwa uwanja ambao TANU ilifanya mikutano yake yote wakati wa kupigani uhuru.

Mwezi Juni 1968 maulidi mbili katika usiku mmoja zilisomwa kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume (SAW). Maulidi moja ilisomwa Mnazi Mmoja na nyingine Ilala.

Chanzo cha haya yote ni kuwepo kwa kutoelewana kati ya viongozi wa Waislam waliokuwa wanajiona kuwa ni wazalendo wafuasi wa TANU na wale viongozi wa EAMWS ambao kambi nyingine ilikuwa ikiwaona kama wapinzani wa TANU.

Yale maulidi yaliyosomwa Ilala yalihudhuriwa na viongozi wa EAMWS na yalipata watu wengi na yakafana sana ukilinganisha na yale maulidi ya Mnazi Mmoja, ya wafuasi wa TANU.

Uongozi wa TANU ulitishika na hali hii iliyokuwa ikijitokeza kwa maana ilikuwa inaonyesha kuwa chama kilikuwa kinapoteza wafuasi ambao walikuwa wakijiunga na kambi ya Tewa na Titi iliyokuwa ikisemekana ipo dhidi ya Nyerere. ''

Baada ya maulid haya haikupita miezi mitatu mgogoro wa EAMWS ukazuka na baada ya miezi mitatu serikali ikaivunja EAMWS kuunda BAKWATA.

Ninachojaribu kueleza ni kuwa historia hii si ya kufanyia utani na maskhara kama unavyofanya hapa ni kitu muhimu sana na nyeti kwa kuelewa mengi katika historia ya Waislam, TANU na uhuru wa Tanganyika.

Ndiyo maana unaona kitabu cha Abdul Sykes kimekamata fikra ya kila aliyekisoma na mwandishi bila kutegemea amejikuta yupo katika dunia ambayo hakutegemea kama angeingia na kuishi humo.
 
Huna lolote wewe Muddy. Tushajua kila kitu in your bag of tricks za kukwepa hoja au maswali ya msingi na magumu kwa kujaribu kutulisha tena utumbo uleule unaopingwa tena usiyo na uhusiano wowote kabisa na maswali uliyoulizwa, wakati huohuo wewe mwenyewe ukibanwa huchelewi kujibu eti hoja husika ipo nje ya mjadala. Wewe kwa kimarekani unaitwa “intellectual fraud” aka trickster.
 
James,
Hapa tunazungumza kuhusu historia ya TANU kama ilivyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni mwaka wa 1981 kitabu ambacho hakikuandika ukweli.

Mimi mwaka wa 1998 nikaandika kitabu cha historia ya TANU nikitumia vyanzo vikuu viwili

Kwanza mswada wa Kleist Sykes (1949) na Nyaraka za Sykes.

Kitabu kipo na hakuna popote nilipomdunisha yeyote.

Ikiwa kuna sentensi umeisoma ambayo inamdhalilisha yeyote tafadhali ilete hapa kama ushahidi.

Wala sijasema mimi kuwa wazee wangu nataka wapate chembelecho, "national recognition."

Kutambuliwa hakuji kwa mtu kutaka.

Naam baada ya kutoka kitabu changu watu wametambua upungufu uliokuwapo katika historia ya TANU na matokeo yake ni kuwa Abdul na Ally Sykes wametunukiwa Medali ya Mwenge wa Uhuru na serikali hii ya CCM.

Hili la kwanza.

Pili.

Kleist Sykes ametiwa katika Dictionary of African Biography (2011).

Haya yote yamepatikana baada ya mimi kuandika historia ambayo haikuwa imeandikwa.

Kama wewe ndugu yangu unaona huku ni kudunisha hiyo ni bahati mbaya sana kwako.
Mzee Mohamedi,
Sijazungumzia kitabu cha Sykes hasha. Nimezungumzia kile ninachokisoma kutoka kwako hapa JF. Ni mara nyingi unawapa ukuu wazee wako, ambao ni wanubi, wamanyema, wazulu na zaidi ya hapo ni waislam kuzidi wengine ambao walifanya mambo sawa au kuwazidi wazee wako. Nikasema sina shida jinsi unavyowaadhimisha wazee wako kitu ambacho ni sawa Mama Maria Nyerere na wakatoriki wanavyomuadhimisha Nyerere kama muumini mwenzao kumpigia chapuo kuwa mtakatifu.

Nilisema shida yangu iko pale unapodunisha wengine na kuonekana hakuna walichofanya pasi na hao wanaoitwa wazee wako. Mbaya zaidi unakuta unaowashutumu hawawezi kukujibu kwa kuwa hawapo.

Kiufupi, maandiko yako mengi huwa yanamshtumu Nyerere moja kwa moja au kwa njia ya mlango wa nyuma na kumfanya duni hasa katika harakati za Uhuru. Na hili wewe na wale wanaowasapoti wazee wako kuna kipindi mlifikia hatua kusema eti hadi kuvaa suruali mlimfundisha nyinyi alivyokuja pwani...sasa mwerevu anaweza kujiuliza mbona hamkufundisha kuvaa kanzu na makubadhi kama wazee wa pwani walivuokuwa wanavaa...

Akina Sykes wana umuhimu sawa kama walivyokuwa Wazanaki, Ma mwami, Watemi, Mtwa, Machief na akina Mangi. Wote walijitoa kwa hali na Mali kwa Uhuru wa Tanganyika
 
Ukweli ni huu kuwa historia niliyoandika ni historia ya pekee ambayo haikupatwa kuandikwa kabla.

Sijamdunisha yeyote.

Ikiwa una ushahidi uweke hapa.
 
Wee Babu wa Urongo bado unajifunuafunua nyeti humu eeh...!

Unazidi kuanika umbea unaoupelekaga huko masjid...uso na haya weye
 
14 October 2020

MZEE ASIMULIA YALIYOJIFICHA ENZI ZA NYERERE "NILIMPOKEA, AKANIWEKA 'KIZUIZINI', ALILALA KWANGU"

Mohamed ana sifa moja kubwa miongoni mwa nyingi.
Ni mtu anayejua kuipeleka hadhra aliyoikusudia kule anakotaka.
Katika kufanisha mipango yake iwe kwa uzuri au ubaya kutegemea hoja, Mohamed hurudi jambo hata mara 1000. Mzee Said anafahamu, kurudia rudia uongo mara nyingi hugeuka kuwa ukweli.
Soma hapa chini
Kwa mtu anayesoma vitu juu juu, au asiye na ufahamu wa kina na mada au mwenye upungufu tu wa kibinadamu wa kuelewa, hoja ya Mohamed inasomeka tofauti lakini kwa mtazamo wa kusudio lake.

Msomaji ataamini kuwa Nyerere alitoka Butiama na kufikia kwa Abdul Sykes.
Na kwamba ujio wa Nyerere ilikuwa zao la juhudi za Abdul Sykes.
Hapo Mohamed atakuwa tayari amempa 'mbwa jina baya ili amuue''

Hapa ieleweke suala si uhusiano wa Nyerere na Abdul unaopingwa.
Nyerere alifika Dar es Salaam kwa mara ya kwanza katika mkutano mwaka 1948 akitokea Tabora.

Baadaye Nyerere alikuja Dar kufundisha kama Mwalimu kule Pugu.

Alipoacha kazi ya Ualimu ndipo alipokwenda kuishi na Abdul

Mohamed hawezi kukueleza mahusiano ya kufahamiana japo kwa juu juu kati ya Nyerere na Abdul

Atakachokueleza ni Nyerere kuishi kwa Abdul na atarudia mara 1000 na inageuka kuwa ''ukweli ''

Tumemueleza Mohamed, haiwezekani Chama kikawa na makao makuu Dar es Salaam chini ya Abdul Kleist Syke Mbuwane, na mwenyekiti huyo asitambue uwepo wa tawi kubwa sana la Tabora likiongozwa na katibu Nyerere.

Haiwezekani kwamba Nyerere alizuka mwaka 1948 kuja katika mkutano ambao watu hawamjui na wala hawakutaka kumjua baada ya hapo.

Ikiwa ni hivyo huyu Abdul atakuwa kiongozi Mpumbavu sana.
Abdul hakuwa mpumbavu! wa kutambua wasomi wachache sana enzi hizo Nyerere akiwa miongoni!

Na ikiwa ilitokea haitakuwa ajabu, Abdul alikuwa Askari na aliwahi kuwafurumusha kwa makonde baba zake katika mapinduzi ya chama, seuse kumtambua Nyerere!

Sina tatizo na mtazamo wa Mohamed wala historia yake.

Nina tatizo na jinsi anavyotumia kalamu yake kuudurusu uongo mara 100 hata kuufanya uwe ukweli kwa sababu rahisi tu '' ukitaka kumuu mbwa mpe jina baya'' na hapa Nyerere hakwepi jina.

Masalaam, narudi viungani kuokota kumbaa !

JokaKuu Pascal Mayalla Mag3
Nimedenda hiii sana yani jf bhana hapaboi hata kidogo. unakosowa kwa hoja na hiii ndio mana halisi ya ufahamu.
"ukitaka kumuuwa mbwa mpe jina baya"
 
Back
Top Bottom